Wazazi wenzangu tuchague shule bora

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
998
Siku chache zilizopita darasa la saba wamemaliza mitihani yao mwisho. Hongereni watoto wote na pia wazazi na walimu. Hongera kubwa kwa jamii yote iliyowapa nafasi watoto kusoma kwa utulivu.
Wazazi wengi watakuwa busy kutafuta shule zenye majina makubwa na zenye ufaulu mkubwa.
Ni jambo jema sana. Lakini ningependa pia wazazi wenzangu mjue mambo machache:

1. Shule nyingi zenye majina makubwa zinafanya usahili kwa ajili ya kuchukua *very smart and talented kids.* Yani wale wenye akili .
Hivyo kama mtoto wako ana akili sana. Ni sehemu sahihi kumpelekeka.

2. Kwa kuwa wanachukua very smart pupils, na wanataka kushindana, mbio zao ni kumaliza syllabus mapema, unakuta mwezi wa nne syllabus ya mwaka mzima imeisha.
Wanaanza marudio ya papers etc. kwa mtoto avarage au mwenye uwezo wa kawaida hapa ndio anapata shida na confusions. Hawezi kaenda na speed hizi.

3. Zipo shule za kawaida, wanachukua watoto wa kawaida kabisa. Wana wafundisha taratibu pamoja na maswali. Wanatumia muda mrefu kumaliza syllabus lakini inawawezesha watoto kuelewa na kuvishika vyema.

Mwisho wa Mwaka wote wanakuwa wamemaliza syllabus na wote wanapata A au B.
Shule inayowapeleka watoto taratibu na kwa kufuata syllabus pia zina tabia ya kuwabeba wasiojiweza mpaka mwisho, kwa kuwa fahari yao ni kufundisha na kubadili, shule zenu hizi zinazochuja watoto kila muhura fahari yao kubwa ni kushindana. Kuitwa wa kwanza.

Kwao kuwa wa kwanza ni kuwashindilia watoto material kwa haraka na kuwafanyisha maswali mengi. Na matokeo yake watoto wengi wa shule hizi wakihama au kwenda vyuoni unawakuta wanakuwa wa kawaida sana.

Na wengi wanakosa GPA nzuri. Kwa kuwa kufundisha watoto kwa ajili hii ya fasta ni nzuri kwa mitihani ya hapo kwa hapo lakini haijawahi kuwa bora kwa kubakiza maarifa ya muda mrefu na ukuaji wa akili.

Nchi za ulaya ziliacha siku nyingi sana kushindilia watoto sylabus ya Mwaka mmoja kwa miezi mitatu. Kwa kuwa haijawahi kuwadanya watoto kuwa bora zaidi ya kuwapa msongo wa mawazo.

Kumbuka maisha bora kabisa unayoweza kuishi duniani ni ya utoto. Watoto wapewe nafasi ya kusoma, kucheza na kufurahi. Wafundishwe na kucheza kwa kiasi.

Kwa Wazazi walioko tayri kuanza kuambiwa Mwezi March kuwa mtoto wako atarudia au mtafutie shule nyingine, basi ndio hizo shule za kushindana. March ni miezi miwili toka mtoto kaanza kufundishwa, kuna miezi nane mbele. Kwa nini mtoto hawezi, au walimu ndio hawawezi kwa kuwa hawako tayari kufundisha Bali wanataka kushindana.

*Wazazi tafuteni shule bora* na sio shule za kwanza, ukwanza wao ni kuwarudisha home wasioweza kusoma kwa haraka na kubakia na wanaoweza kushindana. *Usikubali kumfanya mwanao aamini hawezi wakati anaweza.*
Nawatakia Wazazi wote selection njema ya shule za watoto wetu.
 
HAKIKA MKUU MTOTO APEWE MUDA MREFU WA KUJIFUNZA KWA HATUA STAHIKI... PIA UTENGWE NA MUDA WA KU REFRESH NA MICHEZO PIA
 
Kumbuka maisha bora kabisa unayoweza kuishi duniani ni ya utoto. Watoto wapewe nafasi ya kusoma, kucheza na kufurahi. Wafundishwe na kucheza kwa kiasi.
Watoto wa sasa hivi wamepoteza hii nafasi. Enzi zetu darasa la kwanza unatoka saa tano unarudi home, kuanzia hapo unacheza hadi dada akufuate mkimbizane kwanza ndio urudi nyumbani. Sasa hivi kitoto cha darasa la kwanza kinasoma 'tuition' hadi saa moja jioni!
 
Sielewi dhumuni la kufanya interview kwenye hizi shule za private hata kwa mtoto wa STD1.

Mtoto wangu alienda kufanya interview akiwa na binamu yake wote walikuwa waanze primary shule hiyo lakini yule binamu yake amesema inabidi asome nursery kwanza mwaka mmoja ili wamuandae kwa ajili yamwaka unaofuata lakni binti yangu alifaulu vizuri.

Nikaona isiwe shida yule binamu yake nikampeleka Diamond P/S ila anaendelea vizuri tu na masom yake.

Walisema yule binamu yake hajui kiingereza vizuri ila hesabu anajua kusoma na kuandika Kiswahili anajua.
 
Back
Top Bottom