Samawia
JF-Expert Member
- Dec 6, 2017
- 592
- 466
Ushauri wa mlio wengi nitauzingatia,hata Kama utatofautiana na maamuzi ya wazazi wangu,Nafahamu na wao ni binadamu wakati mwingine wanakosea.
Baba yangu ni mzaliwa wa kwanza kwa wazazi wake,miaka nyuma alikuwa msaada mkubwa kiuchumi kwa nduguze,miaka kadhaa baadae mambo yakamwendea kombo maisha yakabadilika tukaanza kuishi maisha duni sana,Sasa Kati ya wale nduguze(baba zangu wadogo)aliokuwa akiwa akiwasaidia mke wake alifurahia Sana kuzorota kiuchumi kwa baba yangu,hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba wale aliokuwa akiwasaidia walikuwa na maisha mazuri kuliko sisi,sisi watoto tuliitwa nguruwe na Yule mama,alikuwa anasema hawa watoto hata wasichokula mbwa wao wanakula tu,nifupishe.
Baba yetu mdogo(mume wa yule mama) alifariki miaka nane iliyopita ,maisha ya Yule mama yamekuwa magumu kupita maelezo,watoto wake ambao walikuwa hawali wasivyokula mbwa hawana msaada wowote kwake nao wanapambana na hali zao,Mama Yule kasahau udhalilishaji aliokuwa anaifanyia familia yetu,wiki jana alipigia simu ananiomba msaada nimsaidie jambo fulani,nikamwambia hata mimi hali yangu kiuchumi sio nzuri ila siku yoyote mambo yakikaa sawa nitamkumbuka,baada ya kukata simu nikawapigia simu wazazi wangu nikawaambia kila kitu,majibu yao ni kwamba hata Kama nina pesa zimejaa mabenki dunia nzuri basi afadhali zinginge nikazitumbukize baharini lakini sio kumpa Yule mama,binafsi nimeshamsamehe nasukumwa kumsaidia pale uwezo wangu ulipokomea lakini maamuzi ya wazazi ndio hayo,je mnanishauri nini wakuu?
Sent using Jamii Forums mobile app