Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 559
Wazazi wa mwanamume mmoja wa umri wa miaka 30 wametumia mbinu zisizo za kawaida kumlazimisha mto wao huyo kuhama nyumba yao.
Nyaraka za mahakama zinasema kuwa Michael Ratondo halipi kodi ya nyumba wala hasaidii na kazi za nyumbani na amepuuza msaada wa kifedha wa wazazi kutaka kumwezesha apate nyumba yake ya kuishi.
Licha ya kumuandia barua mara tano kumtaka ahame nyumba yao Christina na Mark Rotondo wanasema mtoto huyo wao amekataa kuhama.
View attachment 784886
Michael Rotondo (30) (pichani) ndiye jamaa aliyetimuliwa na wazazi wake kwa kutofanya kazi yeyote na kuendelea kung'ang'ania kuishi nyumbani kwao.
View attachment 784887
Wazazi wa Kijana Michael na Picha ya chini ni nyumbani kwao alipokuwa akiishi na wazazi wake hao.
View attachment 784888
Michael anasema kisheria hakupewa muda wa kutosha kumwezesha kuondoka.
Bi na Bw Ratondo walipeleka kesi kwenye mahakama ya Onondaga karibu na Syracue, New York tarehe saba mwezi Mei baada ya miezi kadhaa ya jitihada za kumshawishi mtoto huyo kuhama kufeli.
"Tumeamua kuwa ni lazima uondoke nyumba hii mara moja," barua moja iliyokuwa imeandikwa Februari tarehe 2 ilisema.
Wakati Michael alipuuza barua hiyo, wazazi wake waliandika tena barua ya kumuagiza ahame kwa msaada wa wakili wao. Source: Bbc Swahili Wazazi wamshtaki mtoto wao kwa kukataa kuhama nyumbani