Wazazi wamalizana kimtindo na watiaji mimba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
WANAFUNZI 30 wa kike wanaosoma katika shule za sekondari wilayani hapa, wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kupata ujauzito kati ya Januari hadi Novemba mwaka jana.

Akizungumza na wadau wa elimu wilayani humo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Haruna Mwenda alisema vitendo hivyo viliwalazimu wanafunzi hao kukatisha masomo yao, jambo linalosababisha kukosa haki ya msingi ya kupata elimu.

Mwenda ambaye pia ni Ofisa Elimu Sekondari wa wilaya hiyo alisema uchunguzi umebaini kwamba, baadhi ya wazazi ni chanzo kikubwa cha watoto wao kupata ujauzito kutokana na kuficha siri iwapo mtoto wake anapopatwa na tatizo hilo.

Alisema hali hiyo husababisha wanafunzi wengi kupata ujauzito na kukatisha masomo kienyeji huku shule zikikosa ushirikiano kwa wazazi hao ambao asilimia kubwa hutatua kesi hizo kwa kutoza faini za kimila badala ya kulifikisha katika vyombo vya sheria.

“Pamoja na yote hayo, lakini baadhi ya wanafunzi hupata ujauzito kutokana na hali ya umasikini wa familia zao na wengine wazazi kukwepa majukumu yakiwamo ya kutimiza mahitaji muhimu na uhuru wa wanafunzi usio na mipaka,” alisema.

Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo amevitaka vyombo vya dola kushirikiana na maofisa watendaji wa serikali za vijiji kutokomeza vitendo hivyo kwa kutekeleza sheria zilizopo na kuachana na mifumo ya kutatua kesi hizo kwa njia za kimila.

Hata hivyo alisema ili kutokomeza vitendo hivyo ni vyema wanafunzi wanaokataa kuwataja watu waliowapa mimba nao waadhibiwe hadi watakapowataja watu hao ambao watachukuliwa hatua za kisheria.

HabariLeo | Wazazi wamalizana kimtindo na watiaji mimba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom