Wazazi na ndugu wa mke wangu wananikosesha raha

Kubalababaake... Yani mama mkwe kaingia on target"""" sema chamsingi ni kukaa na mkeo kumwambia hali kwasasa ni ngum sasa cha kufanya aongee na nduguze warudi kwao kama awataki piga taraka wote 9
Wakuu mimi ni mkazi na mzaliwa wa Dar es Salaam maeneo ya Tegeta, tatizo langu kuu mpaka nimekuja kuomba ushauri ni mke wangu kawakusanya ndugu zake na wazazi wake toka kijijini huko Mpwapwa. Yani imekua kero mi mwenyewe ndio natafuta maisha lakini nyumbani tupo jumla watu tisa pamoja na wazazi wake, nyumba yenyewe nimepanga nyumba viwili na sebule.

Sina raha hata kujiachia na mke wangu siwezi, mwezi wa nne huu hata mzigo sijala maana asubuhi nimeenda kazini, nikirudi jioni watu wamejaa na usiku wanalala sebuleni wengine chumbani.

Nimevurugwa kijana mwenzenu pesa yote ninayopata ambayo tungenunua hata kiwanja inaishia kwenye chakula na wanakula mno. Mke wangu nimejaribu kumwambia awambie ndugu zake na wazazi warudi kijijini lakini hataki eti anatamani awe nao karibu ili akibahatika kupata mtoto wamsaidie kulea.

Ndugu zangu naomba ushauri nifanye nini, nikimbie nyumba au niwafukuze mimi mwenyewe.

Rafiki yangu mmoja alinishauri labda nimtongoze mama mkwe lengo achukie aondoke na mmewe lakini cha ajabu amekubali 😥😥😥😥

MNISHAURI SANA🙏🙏🙏🙏NASOMA COMMENTS ZOTE.
 
Kubalababaake... Yani mama mkwe kaingia on target"""" sema chamsingi ni kukaa na mkeo kumwambia hali kwasasa ni ngum sasa cha kufanya aongee na nduguze warudi kwao kama awataki piga taraka wote 9
Acha mkuu. Saivi hawapo walienda kwao kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka sijatuma nauli ya kurudi mpaka leo
 
Back
Top Bottom