mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Pamoja na kiwango kikubwa walichoonyesha kupambana na mabingwa hao watetezi na kutoka suluhu watoto wetu walionekana wenye maumbile madogo madogo sana ukilinganisha na mahasimu wao wenye umri Sawa.
Kuna tafiti kadhaa zimefanyika na kuhitimisha kuwa watoto wetu wengi wana kimo kilichochini ya wastani.
changamoto hii iwaendee wazazi na wote wanaotarajia kuwa na watoto kwamba ni afadhali mzazi ulale njaa kuliko mtoto kukosa mlo kamili kipindi anapouhitaji zaidi. Ikishindikana basi tujitahidi watoto wapate kikombe cha maziwa kwa siku.