Wazaramo acheni ukabila kwenye mambo ya maendeleo

Wazaramo acheni ukabila kwenye mambo ya maendeleo

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,598
Reaction score
2,905
Hi, GTs!

Nilkuwa Kisarawe Kijiji fulani. Mara kipaza sauti kikasikika kikisema "Tangazo Tangazo! Wananchi wote wa Kijiji cha (....) mfike katika viwanja vya Shule ya Sekondari (....), kuna ugeni umeleta msaada.

Tukaenda, tukakuta mkutano umekwishaanza. Kumbe kuna kikundi kinachojiita cha Kizalendo kinachotekeleza Kampeni ya TOKOMEZA 0 cha DC Jokate Mwegelo na kimeleta Photocopy Machine & Computer shuleni hapo. (Ni jambo jema).

Cha kushangaza wana kauli mbiu isemayo "Uzalendo, kunogile ukae" halafu Kizaramo kingi, mara ngoma asili yao mara sijui nini (yaani wanajizungumzia wao tu) kana kwamba hakuna watu wa jamii nyingine.

Harambee ikapita kwa viongoz n.k. Baadae MC akamuona jamaa yangu fulani aliyevaa kijadi akasema "Oh namwona Masai" akamfuata, akampa mic akamwambia "Unatoa Sh ngapi" Jamaa akajibu "Mimi ni mgeni tu"

Kiukweli hakuchangia chochote. ALIHISI KUTENGWA!
 
Ulitaka waongee lugha gani wakati asilimia kubwa ya wanakiji ni Wazaramo?..

Una bahati wamekuachia uishi Daresalam!!
Kuna mwaka nilitembelea Ngorongoro chini kule nikakutana na kikundi cha Jamii ya kimasai, nilijipendekeza kuzungumza nao kiswahili hamna hata mmoja aliejua kuzungumza kiswahili, Je Masai nao walikuwa WAKABILA??
 
Chabuso said:
Hamna hata mmoja aliyejua kuzungumza Kiswahili

Mkuu... umeshasema "HAKUNA ALIYEJUA" kwa hyo wale Wamasai hawakuongea kwa vile HAWAJUI na si vinginevyo!

Sasa hawa tulitegemea labda wananchi wangeleta ukabila, lakn imekuwa kinyume. Viongozi tunaotegemea kuwa ni kioo cha jamii ambao ndio wa kutuweka pamoja, kudumisha umoja na pengine kutoa elimu kwa wananchi, ndio hao hao wanakuwa mstari wa mbele kuleta ukabila.

Kwa hvyo wananchi wafanyeje?
 
Chupayamaji said:
Ukitaka kuona ukabila nenda usukumani utaleta mrejesho

Ukabila utokee labda kwa wananchi tunaweza kuzingizia labda elimu hakuna mtaani.

Ila ni aibu kuona hayo yanatokea kwa viongozi na wasomi.
 
Mirlz B Matthew said:
Unawazingizia wazaramo. Ukikutana na wasukuma ukiongea kiswahili wanakuita mswahili (Jinsi wanavyokuita ni kama dharau fulani hivi)

Mkuu... tunaweza kusema labda elimu hawana. Ikitokea kwa viongozi na wasomi tutasemaje? Huo si ndio ukabila?
 
Kuzu
Mkuu... umeshasema "HAKUNA ALIYEJUA" kwa hyo wale Wamasai hawakuongea kwa vile HAWAJUI na si vinginevyo!

Sasa hawa tulitegemea labda wananchi wangeleta ukabila, lakn imekuwa kinyume. Viongozi tunaotegemea kuwa ni kioo cha jamii ambao ndio wa kutuweka pamoja, kudumisha umoja na pengine kutoa elimu kwa wananchi, ndio hao hao wanakuwa mstari wa mbele kuleta ukabila.

Kwa hvyo wananchi wafanyeje?
Mkuu, Mimi sioni ukabila uko wapi hapo, kuzungumza kilugha sio ukabila, kwenye daladala nakutana na watu wanaongea lugha zao lakini siwachukulii kama wao Wakabila
 
Ni kweli mkuu chabuso kwamba kuzungumza kilugha si ukabila. Ila tunazungumzia pale unapoongea kilugha ni mahali gani. Chukulia mfano tuna kikundi chetu ambacho kuna labda wamasai, wazaramo, wagogo n.k. Halafu tukakutana kujadili mambo yahusuyo kikundi chetu, halafu mimi nasimama hapo hapo kwenye kikao kuchangia hoja halafu naanza kuongea kimasai.

Hivi ninyi wengine mtanielewaje?
 
Back
Top Bottom