Barubaru
JF-Expert Member
- Apr 6, 2009
- 7,161
- 2,323
hoteli zote zinajulikana na ni kweli wengi ni wabara ila hawana maisha, mishahara haifiki laki 2 kwa mwezi. huwezi linganisha na wapemba wa kariakoo wenye mtaji wa zaidi ya Trilioni. hawa ni watu wa njaa tu ninawajua asilimia kubwa. hao wamasai wanasaidia kukuza zaidi utalii maana ni kivutio na pia wengi ni walinzi tu hawaelewi wanachofanya zaidi ya kusuka rasta na kuruka ruka.
Ndio maana nasema ije Tanganyika. wa znz waendeshe utalii wao wenyewe.
Mtu yoyote mwenye akili na ufahamu akikusoma hapa ataona kabisa wewe ni Low profile.
Ina maana ujui kuwa mishahara inapangwa kutokana na Kisomo chako, kazi unazofanya. Na ukimuona mtu amekubali kufanya kazi basi ujue ameona kuna maslahi kinyume cha hapo angeondoka kurudi kwake. Kwani mkataa kwao mtumwa.
Kumbuka kuwa TGK kuna wachina, wahindi,wazungu, wakenya na mataifa mengine kibao wanaofanya biashara na wengine wawekezaji. Hivyo hata ukiwa nje ya muungano hao waZnz wataendelea na biashara zao kama wawekezaji wa kigeni kwa kufuata tartibu za kiuhamiaji.
Us'tie shaka kuwa na amani kwani hakuna kitu bora kama uwekezaji wa ndani na ndio huo unaoinua uchumi wa nchi.
Pole sana