Wazanzibari wanataka nini? What do Zanzibaris want?

Hakuna kitu kama hicho eti muungano kuvunjwa, ni ujuha tu, matumizi mabaya ya uhuru wa kutoa maoni. Asiyetaka muungano na ahame tz aende nchi ambayo haina muungano. Zanzibar ni sehemu ya muungano hata kama ikibidi nguvu zitatumika juu ya hao wanao dai kujitenga, hatuwezi kurudishwa nyuma na watu wachache ambao hawajui watakalo wala wasemalo.Sasa hivi issue ya kuzungumzia ni East African Federation siyo upuuzi wa zanzibar kujitenga kwa kuwa haiwezekani, tayari ni ndugu, kama isivyowezekana kukana undugu na ndugu yako wa tumbo moja ndio na muungano haukaniki japo unaweza kurekebishika.
 
mbona hoja dhaifu zote! yaani huyo jamaa aliyeanzisha hii thread anakunywa chang'aa au pombe ya mnazi? mbona sijamwelewa kabisa, Zanzibar ifanyeje.....? kwani Zanzibar ipo wapi? au ni nchi ya kufikirika tu? mimi navyofahamu Shamsi Vuai Nahodha na Mizengo Pinda wote watanzania tu, sijui nani kati yao mzanzibaar wala mtanganyika, watu waache upumbavu wanadhani wakiwarudisha waarabu ndio maendeleo yatakuja? teh teh teh! hawajui hao waarabu wenyewe wanapigana na kuandamana hovyo ? na wewe Administrator wa JF unaacheje upuuzi kama huu? hapa ni home of Great Thinkers Bwana mambo ya vijiwe vya kahawa hapa sio mahali pake, mban kabisa huyu jamaa , tunaacha kujadili mambo ya msingi kama kukomesha umasikini au huyu mtu hajui kuna watanzania wanalala pembeni ya barabara? wengine hawamudu hata milo mitatu? tujadili hoja za msingi sio story za juma na uledi na hadith za pwagu na pwaguzi......SORRY NAWAZA TU KWA SAUTI WADAU!

Ukiona mtu anatoa matusi basi ujue hana hoja huyo.

Unamfananisha Pinda na Nahodha?

Hao ni watu tofauti na hata ukilazimisha, bado wanatoka sehemu tofauti. Usidhani kuwa Zanzibar ni kama Mkoa au Wilaya ya Tanganyika hata kidogo.

Administrator akuzuie wewe kwa matusi yako na kukosa hoja na sikuzuia watu kutoa maoni yao.

"Ikiwa watu wa Zanzibar, bila ya kuingiliwa na watu wa nje na ikiwa wana sababu zao, wakaamua kuwa Muungano umekuwa kero kwa maisha yao, na kwamba hauna maslahi na wao sitowalazimisha kubakia na Muungano huo. Muungano huu utasita pale tu NCHI shiriki itakapoamua kujitenga" by Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Zanzibar for Zanzibaris
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom