Wazanzibari wanataka nini? What do Zanzibaris want? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari wanataka nini? What do Zanzibaris want?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Falconer, Apr 25, 2011.

 1. F

  Falconer JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Sisi hatuna makubwa. Kwa kuwa ni watutunao tawaliwa(kikoloni) na Tanganyika kwa kisingizio cha muungano, tunachotaka ni "independence", "Freedom" and "Democracy".
  Sina haja kuchambuwa kila kimoja lakini nafikiri wakuu munanifahamu vizuri tu. Matatizo makubwa ni kuwa pale wazanzibari wanapo jaribu kuwaeleza matatizo yao, wenzetu munafunga masikio. Kwa kejeli munatwambia, "mayakhe hao kubwa wakaimbe taarabu". Siku hizi naona taarabu munaimba nyinyi maana mumewasikia wazanzibari kwa sauti moja kabisa kuwa "HATUUTAKI MUUNGANO".

  Hatima ya muungano soote tunaijuwa na CCM na vikaragosi wake, wanachotumia ni ubabaishaji tu. Ni mfano wa "mbuni anapo tia kichwa chake mchangani akihisi amesalimika kwa kuwa hamuoni adui yake kumbe vile mwili wake wote uko nje".

  Wazanzibari wamekwisha kuchoka na usaniii ndio maana tunasema,"IT'S OVERRRRR".
   
 2. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Je una maana

  1) Nchi mpya kama Sudan kusini inayojitegemea
  2) Muungano lakini uhuru zaidi? (kama ni hili tueleze uhuru gani unaoutaka)
  3) Muungano lakini Zanzibar ikipata mafuta yawe ya zanzibar tu?
  4) Zanzibar wawe na uhuru wa kwenda bara bila passport lakini wabara wahitaji passport kuja zanzibar?

  Nilazima muueleze kiundani mimi bado sijajua vizuri ni kitu gani hata Wanzanzibar wanahitaji kama unavyosema uhuru una maana gari? naona kuna raisi na wabunge waliochaguliwa!!! tueleze kiundani tuelewe.
   
 3. U

  Uswe JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wengi wanataka kujitenga. Ninaisubiri hiyo siku kwa hamu, maana mi nawaona wazinzabari ni watu wa kulalamika tu, very lazy halafu wanategemea kila kitu kitakuja mezani.

  Anasema tunawatalawa kikoloni na anadai indepence, freedom and democracy, sasa mkipata hiyo mnayoita 'independence' bado mnataka tuwape na freedom na pia tuwape democracy? i mean hivo navyo mnasubiri sisi tuwape?
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ile Zanzibar huru mlioikuta mkaiunganisha na Tanganyika na baadae mkajidai kuiua Tanganyika huku mkiichakachua Zanzibar na kuimg'angania mpaka leo.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mim kila siku nasema na naendelea kusema kwamba kwakua wenzetu wa visiwan wanadai chao,baaas tuachane nao,maana inawezekana wao wnaamin kua umaskin wao unatokana na watanganyika,so its better tukivunja muungano wabak na mambo yao,maana ukilala muungano,ukisinzia muungano,ukiwa usingzin muungano,ajira muungano,mapato muungano,soka muungano,kiiiila kitu muungano,jaman wa,euchoka waacheni watembee wenyewe,
   
 6. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kina bakharesa watauza unga wao wapi na wazanzibari hawajui ugali? ok watauza urojo, lakini pia bado viazi vitahitajika kwa urojo, hizo meli za kila siku asubuhi zinavusha nyanya, viazi, vitunguu na vyakula vingine vyote kwenda zanzibar vikilipishwa kodi ya juu kama kuuza nje? yaani zanzibar itakuwaje? pia umeme wakiuziwa bei ya juu? hiyo ndoto ya mafuta hamna, yapo kama vile ambavyo vipo kila sehemu, lakini madogo hayachimbiki kibiashara hayalipi hata mtambo mwenyewe.
  watasota sana wazanzibari. wakianza mikwara mbuzi yao watalii watakimbia, hapo wataomba tuwatawale kama wilaya ya Tanzania, eti ujinga wao watasaidiwa na waarabu au nchi za kiislamu? mbuzi kweli hao jamaa, kwani COMORO, UGANDA, SOMALIA, MAURITANIA, AFGHANISTAN, YEMEN, BANGLADESH pamoja na nyingine nyingi wamepewa nini? waarabu mnaowaabudu nao wako foleni moja na nyinyi sasa, mnataka mkae mpewe nao? wao wakishapata marekani, ulaya au china ndiyo mletewe kwenye mkeka?
  nawapa pole
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  ujumbe murua kabisa watafakari mara mbili au zaidi kabla hata kufukiria...wasije baadae wakaja mbio kutaka tena Muungano kwa kisingizio kuwatosa wapemba..
   
 8. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jina lako na lugha yako mnalingana sana na sijashangaa sana.

  Hizi lugha za matusi, kejeli na dharau za nini tena.

  Kama sisi unasema yatatukuta hayo yote, tena kwanini mnatung'ang'ania kama kupe?

  Hapana shaka kuna faida mnapata kuikalia Zanzibar.

  Kwani kabla ya nyie kuja na fitna zenu, tumewaomba nini?

  Hebu ingieni akili na sio kupayuka kama mtu alieanguka mtoni?

  Mkituachia na kwa kuendekeza kwenu ufisadi, baada ya miaka 10, nyinyi ndio mtakuja kutuomba.

  Zanzibar for Zanzibaris and we cant wait to see your backs.
   
 9. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wishful thinking indeed.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Zanzibar inachotaka wewe unakijuwa! Kwani katika utawala wa CCM huko Tanganyika mnakosa nini? mnakula, mna safiri umnakotaka, mnaweza kusema sasa sio kama wakati wa Haambiliki na mengi mengine. Sasa sijui mnataka nini hata mnataka kuwaangusha kina magamba!
   
 11. K

  KAMBOTA Senior Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mbona hoja dhaifu zote! yaani huyo jamaa aliyeanzisha hii thread anakunywa chang'aa au pombe ya mnazi? mbona sijamwelewa kabisa, Zanzibar ifanyeje.....? kwani Zanzibar ipo wapi? au ni nchi ya kufikirika tu? mimi navyofahamu Shamsi Vuai Nahodha na Mizengo Pinda wote watanzania tu, sijui nani kati yao mzanzibaar wala mtanganyika, watu waache upumbavu wanadhani wakiwarudisha waarabu ndio maendeleo yatakuja? teh teh teh! hawajui hao waarabu wenyewe wanapigana na kuandamana hovyo ? na wewe Administrator wa JF unaacheje upuuzi kama huu? hapa ni home of Great Thinkers Bwana mambo ya vijiwe vya kahawa hapa sio mahali pake, mban kabisa huyu jamaa , tunaacha kujadili mambo ya msingi kama kukomesha umasikini au huyu mtu hajui kuna watanzania wanalala pembeni ya barabara? wengine hawamudu hata milo mitatu? tujadili hoja za msingi sio story za juma na uledi na hadith za pwagu na pwaguzi......SORRY NAWAZA TU KWA SAUTI WADAU!
   
 12. Katambala

  Katambala Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Chanzo cha muungano ni shinikizo la mabeberu kwa mchonga kuiunganisha zenji kwasababu waliiona kama tishio kwao. Ndio maana hata viongozi wenyewe hawataki tujadili kwasababu yalikuwa ni mawazo ya mtu mmoja na si matakwa ya sisi wadang'anyika na wazanzibari.Tusome historia ndipo tutoe majibu na siyo ushabiki. Cha msingi kura za maoni zipigwe wananchi tujiamulie kama tunaka huu muungano au la na sio kulazimisha tu
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Kwani kina Lowassa na Rostam hawajui kuuza unga huko? Hii ujuwe si sifa nzuri kama unavyojifikiria kuona Mzanzibari (kama unavyombaguwa) anakusaidieni kwa maisha na hukju nyie wenye nchi mnafisidiana!
  Kuhusu eti viazi, vitunguu na vyengine hilo si tatizo kwa vile ni biashara ambayo tunaweza kununua popote kwa vile hamtowi sadaka1 Hili la umeme nalo si kitu tulishawahi kuishi zaidi ya miezi mitatu bila ya umeme wenu. Kipindi hicho ni kirefu sana kupata utatuzi wa suala hilo iwapo tutakapojuwa kuwa umeme wenu hamuuzi tena!
  Kwani nyie mna kitu gani cha kujidai wakati mnakufa kwa njaa na hamna njia ya kuzuia vifo hivyo. Ni ujinga kufikiri kuwa kwako kuomba ni halali na jambo tukufu na kuona mwenzako kufanya hivyo ni fedheha. Ni miaka 50 sasa lakini ndoto ya kujitegemea bado hamjaifikia juu ya kuwa huru wa kufanya mnavyotaka kinyume na hali ya Zanzibar inayolazimishwa kutofanya chochote cha maendeleo yake bila ya kuingiliwa nanyi. Turuhusuni basi ili baada ya miezi sita turudi kuwapigia magoti!
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona usiseme Pinda na Rostam na badala yakke ukachaguwa watu wanaotoka pande mbili tofauti?
   
 15. F

  Ferds JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mi nadhani ni mzanzibari ndio kamnganda mtanganyika, maana anapata Dual Rights, ndani ya zanzibar anahaki yake pekee maana mtanganyika hana haki huko, mfano haki ya kumiliki ardhi ni ya mzanzibari tu zenji mbara mpangaji, huku jamaa wanamiliki maana ni ardhi ya watanzania wote- sasa nani nafaidi ktk huu muungano
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,802
  Likes Received: 5,093
  Trophy Points: 280
  ..aiitishwe kura ya maoni ili tuweze kujua wa-Zanzibar waliowengi wanataka nini.

  ..kila Mzenji, kulingana na nafasi na shughuli zake, ana mtizamo/malalamiko yake kuhusu muungano.

  ..kuna wanasiasa walionyimwa ulaji kutokana na ushiriki wa Tanganyika ktk siasa za Zanzibar. hawa hawataki kuusikia muungano.

  ..wako wengine waliopata madaraka huku Tanganyika na wanatajirika kutokana na nafasi zao ktk serikali ya muungano. hawa wako tayari kutoa mtu roho kuulinda muungano.

  ..wako wafanyabiashara ambao wanadhani Tanganyika inawanyima fursa ya kufanya watakavyo haswa ktk masuala ya ukwepaji kodi. hawa wanataka muungano usitishwe hata leo hii.

  ..i can go and on....

  ..KURA YA MAONI NDIYO NJIA YA UHAKIKA NA MUAFAKA KUJUA MTIZAMO WA WAZANZIBAR WALIO WENGI KUHUSU MUUNGANO.
   
 17. F

  Falconer JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Haina haja ya matusi. Si mueona kwamba hamuna isipokuwa matusi. Kama ni Bakhressa, ile ni juhudi yake kujiendeleza maisha. Alishindwa Mkapa kummaliza kwa kuwa Mwenyezi Mungu anamlinda. NYinyi munataka kuikana historia. Munajuwa historia ya Zanzibar au munapayuka tu.
  Sisi hatutaki kutawaliwa. Tunataka taifa letu huru. Wengi wenu mulionishambulia munaonyesha udhaifu wenu. Hamuna hoja ya kunipinga. Muna "inferiority complex" inawasumbua.
  Jibuni kwa "points" sio matusi.
   
 18. S

  Sheba JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono! Hao waarabu walisaidia nchi gani? Hivi sasa waarabu wenyewe wanakabiliwa na machafukoi ya ndani na wanaelekeza rasilimali zao kutuliza hali ya siasa ndani yao. Oman pale nchi ambayo wanaitegemea sana yenyewe imekumbwa na msukosuko, Sultan ameahidi ajira mpya 50,000 na kuongezeka kwa marupurupu, huyo ndio wanamtegemea akasaidie Zanzibar? Isitoshe, mfano mzuri wa msaada finyu wa waarabu upo pale Comoro. Nchi ile ambayo ni visiwa vyenye watu wachache kama Zanzibar na wengine wamejificha ughaibuni kule, wameamua kuongea kiarabu kama mojawapo ya lugha ya taifa, wamejiunga na OIC na pia ni wanachama wa Arab League lakini hali yao bado dhoofu tu. Hao waarabu wamewapa nini cha maana? Hiyo OIC imewapa nini cha maana? Ndio ije kuwa Wanzanzibar?

  Mi nadhani imefika mahala waachiwe waende zao na sie huku tuchukue viwanja vyetu, wakajiandikishe TIC kama wawekezaji, umeme ule ambao tunawapelekea kwa bei ya chini tena ambayo pia hawalipi tuwapelekee wananchi wetu ambao hawana umeme. Kisha turudishe jeshi letu na polisi waanze kujilinda wenyewe kwa gharama zao. Aidha tutakuwa tumepunguza gharama ya kuendesha Bunge kwa kupinguza wabunge 50 ambao jumla yao wanawakilisha watu wasiozidi laki 3 ambao ni chini ya wapigakura wa jimbo la Ubungo na jumla yao wote ni chini ya wakazi wa wilaya ya kinondoni. Kisha tutaongeza ajira nyingi tu kwa kuwaondoa Wazanzibar wote katika nafasi za muungano zikiwemo mawaziri, makatibu wakuu, mabalozi nk.

  Hakuna kikubwa cha mno tutakachopoteza zaidi ya mazoea tu kuwa tumekuwa na wenzetu, tena tutakaohisi hivyo ni wananchi wa pwani wala si wa kigoma au tabora. Mbara anaweza kuishi miaka kumi bila kulazimika kwenda zanzibar wakati mzanzibar hana ujanja wa kuishi miaka 5 bila kufika bara kwa Ami au shughuli nyingine yoyote kama kununua bidhaa nk.

  Inasikitisha kuwa wanasiasa na middle class wachache wa Zanzibar kwa kutaka tu kupanua wigo wa maslahi yao dhidi ya wazanzibar walio wengi wanajificha katika wigo wa kutaka kuvunja muungano. Wanadhani wakuvunja watapata fursa zaidi za vyeo na itifaki. Wanasahau kuwa, gharama kubwa ya amani yao na ustawi wao inabebwa na Wabara kwa kuwapa ardhi, fursa ya kucheua population yao ya ziada, ulinzi na usalama, uwakilishi nje na fursa za biashara.

  Wakiendelea na hali hiyo wataamsha hasira zetu tuvunje muungano. Yawezekana tuliwahitaji sana huko nyuma wakati tunaungana, na kwa wakati huo, sisi na wao wote tulikuwa na mahitaji. Mazingira yamebadilika, they are no longer that relevant, they can go to hell. Wanasahau kuwa even geoghraphy inawapa sababu kubwa ya kutaka wawe katika muungano kuliko sisi. Umbali kati ya Pemba na Tanga na Zanzibar na Bagamoyo ni fupi zaidi kuliko distance kati ya pemba na unguja.

  Don't push us to the limits.......!
   
 19. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Watanganyika wengi wanarubuniwa akili zao ndio mana babu wa loliondo aliwauwa sana kule kwa kisingizio kikome kimoja kinatibu maradhi sugu ambayo mzungu halali usiku mchana ametumia science na technology kutafuta dawa hiyo ya babu wameshindwa leo babu uwoteshwe wewe kikombe utibu mamilioni ya watu kwani wewe mtume ? astaghfir wallah,,,acheni ujinga

  Hawa walokole wote mameshiba kikombe cha babu wanakuja hapa kuropoka tu,hivi hamuelewi kile tunachodai wazanzbari mika arubani na 47 ya muungano ? Samueli sita tulisha muambia its over kama hamukijui muulizeni.

  Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi,tunachodai na mamlaka yake,ambayo yamevaliwa na muungano na kuidhoofisha muungano mbona hamuelewi kila siku tunawaletea mada ? Tunawaletea sheria tunawachambulia bado hamuelewi watanganyika ?

  Ikiwa kikombe hakiwatoshi basi kuna maji ya zamzam nafikiri yatawatibu akili zenu,,,,
   
 20. A

  Albimany JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Mbona mazingira ya kijografia ya Uganda,Kenya,na Msumbiji yanawaruhusu zaidi kuliko ya Zanzibar? sijui mutaungana nao kwastail ya muungano huu?

  Wewe unajiita mtu wa pwani kama ni kweli itakua hujashau pale mulipo kua mukikesha na meli kuja zanzibar kuchukua bidhaa halafu mukienda kulanguana.

  Kwahiyo uwezekano upo bado wa watangnyika kurudi tena.na wazanzibari tutakuja kuwaletea bidhaa na kuchukua hio michele.

  Na jengine husikia sana mukitaja UMEME hivyo munajua kua zanzibar wananunua umeme mara mbili ya bei ile inunuliwayo T,nyika?
   
Loading...