Wazanzibari wameamka?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
WAZANZIBARI WAMEAMKA?

Toka ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ghafla Zanzibar imebadilika na kuwatia matumaini makubwa Wazanzibari.

Yanayoonekana katika mitandao ya kijamii katika maandishi, picha na sauti yalikuwa tabu hata kufikirika kwa mbali majuma machache yaliyopita.

Waliokuwa wakitazamana kama maadui kiasi cha kufikia kusababisha watu kuteswa na kuuliwa sasa wamekuwa ndugu wanaonekana pamoja wakiwa na tabasamu huku wakipeana mikono.

Hii ni faraja kubwa kwa Wazanzibari wengi ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Dr. Martin Luther King katika hotuba yake ya mwisho kabla hajauawa alisema maneno haya, ''I've been to the Moutaintop and I've seen the promises land.''

Martin Luther King anasema amefika juu ya kilima na ameiona nchi ya ahadi akiwa na maana kuwa kwa yale aliyokuwa anashuhudia juu kilimani, basi huko waendako kutakuwa na nema.

Jana katika kusherehekea mapinduzi bendera za ACT Wazalendo na bendera za CCM zimeonekana katika viwanja zikipepea bega kwa bega.

Lakini binafsi lililokamata fikra yangu zaidi ni kuona video ya wanafunzi wa Muslim University of Morogoro (MUM) Chuo Cha Kiislam Morogoro wamekusanyika katika ukumbi wakisheherekea mapinduzi kwa kuimba nyimbo maarufu inayoimbwa sana katika sherehe za CCM Zanzibar.

Nyimbo hii ina umri sawa na mapinduzi yenyewe.
Haya yote yanaashiria kitu gani?

Haya yanaashiria kuwa Wazanzibari wameamua kusonga mbele katika udugu wao kwa maslahi ya nchi yao.
Ikiwa Wazanzibari wameamua kuwa kitu kimoja hii nini maana yake?

Maana yake ni kuwa Wazanzibari wameondoa uhasama baina yao.
Ikiwa uhasama umeondoka Wazanzibari wategemee nini?

Kubwa ni kuwa utakapofika In Shaa Allah uchaguzi mwaka wa 2025 halitaingia jeshi Zanzibar kutoka Tanganyika kama ilivyokuwa kawaida miaka yote wakati wa uchaguzi.

Ulazima huu hautakuwapo.

Hili nalo nini maana yake?
Hili likipatikana maana yake ni kuwa Zanzibar itakuwa imekomboka na Wazanzibari watafanya uchaguzi huru na wa haki.

Vikosi vya kukamata Wazanzibari kuwapiga na kuwatesa katika kila uchaguzi itakuwa ni ndoto mbaya ya jinamizi.
Hili likipatikana kura itapoteza thamani ya damu ya Mzanzibari.

Katika utulivu na amani visiwani nini hali ya baadae ya Ubao wa Kisonge na waandishi wake?
Labda tulitengeneze vyema zaidi swali hili.

Hii hali ya utengamano inayoshuhudiwa hivi sasa Zanzibar imewafurahisha Wazanzibari wote?
WanaKisonge na Mazombi wamefurahi?

Wapo ambao walikuwa wananufaika sana na uadui baina ya Wazanzibari na wamenufaika kwa miaka mingi kiasi jambo hili likawa kwao wao ni ajira ya kudumu.

Wakilala wanawaza Ubao Mweusi wa Kisonge wakiamka wanawaza kazi na shughuli za Uzombi.

Hawa ghafla wamejikuta hawana tena ajira iliyokuwa ikiwaingizia kipato.
Hawa ghafla wamejikuta hawa kazi ya kufanya.

Huenda, haijulikani, huenda hawa waandishi wa Ubao wa Kisonge wakatungua ubao wao na kugawa chaki zao kwa waalimu wa madrasa.
Huenda pia na Mazombi wakatupa nondo na marungu yao kwani hakuna wa kupiga wala kutesa.

Dr. Martin Luther King alisema amefika juu ya kilima na kaiona nchi waliyoahidiwa na Mungu.
Maalim Seif wanahistoria watakapokuja kumuandika watakuwa na mengi sana ya kumuelezea.

Maalim wasaidie wanahistoria kwa wewe mwenyewe kunyanyua kalamu na kuandika kumbukumbu zako kwani jina lako limetawala Zanzibar katika kipindi kirefu na muhimu sana cha historia yake.

Walter Cronkite anasifika kuwa yeye ndiye mtangazaji wa televisheni pekee ambae amepata kuwahoji marais wa Marekani wengi kupita mtangazaji yeyote wa wakati wake.

Maalim umesimama kulikabili sanduku la kura na kila rais aliyetawala Zanzibar.
Hii ni rekodi tabu kuvunjwa.

Ulimwengu ungependa kuisikia historia hii kutoka kinywani kwako.

=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']0:00 / 0:40

Hii kitu tunahitaji Bara. Japo itakuwa inaiba lakini basi chama cha kikuu cha upinzani na chenyewe kipate kula itasaidia kupunguza kelele na manung'uniko.
 
"Nyimbo hii ina umri ......"!!!! usahihi ni " Wimbo huu una umri...." .Hata nyie Wazee mnaendeshwa na swaga za Bongofleva! Bure kabisa!
Halafu wewe Mzee Mohamed Said ni mbaguzi na mdini sana!

Kauli ya kwamba Jeshi kutoka Tanganyika kuingia Zanzibar! Ni kauli ya kijinga na kibaguzi sana kutoka kwa mtu mpuuzi!

Suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano,sasa unaletaje kauli za kijinga kama hizi?

Kwani huwezi kuelezea mafanikio ya Zanzibar bila kuchochea ubaguzi ndani ya Muungano.

Utaendelea kusikilizwa na wapuuuzi wenzako!
 
WAZANZIBARI WAMEAMKA?

Toka ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ghafla Zanzibar imebadilika na kuwatia matumaini makubwa Wazanzibari.

Yanayoonekana katika mitandao ya kijamii katika maandishi, picha na sauti yalikuwa tabu hata kufikirika kwa mbali majuma machache yaliyopita.

Waliokuwa wakitazamana kama maadui kiasi cha kufikia kusababisha watu kuteswa na kuuliwa sasa wamekuwa ndugu wanaonekana pamoja wakiwa na tabasamu huku wakipeana mikono.

Hii ni faraja kubwa kwa Wazanzibari wengi ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Dr. Martin Luther King katika hotuba yake ya mwisho kabla hajauawa alisema maneno haya, ''I've been to the Moutaintop and I've seen the promises land.''

Martin Luther King anasema amefika juu ya kilima na ameiona nchi ya ahadi akiwa na maana kuwa kwa yale aliyokuwa anashuhudia juu kilimani, basi huko waendako kutakuwa na nema.

Jana katika kusherehekea mapinduzi bendera za ACT Wazalendo na bendera za CCM zimeonekana katika viwanja zikipepea bega kwa bega.

Lakini binafsi lililokamata fikra yangu zaidi ni kuona video ya wanafunzi wa Muslim University of Morogoro (MUM) Chuo Cha Kiislam Morogoro wamekusanyika katika ukumbi wakisheherekea mapinduzi kwa kuimba nyimbo maarufu inayoimbwa sana katika sherehe za CCM Zanzibar.

Nyimbo hii ina umri sawa na mapinduzi yenyewe.
Haya yote yanaashiria kitu gani?

Haya yanaashiria kuwa Wazanzibari wameamua kusonga mbele katika udugu wao kwa maslahi ya nchi yao.
Ikiwa Wazanzibari wameamua kuwa kitu kimoja hii nini maana yake?

Maana yake ni kuwa Wazanzibari wameondoa uhasama baina yao.
Ikiwa uhasama umeondoka Wazanzibari wategemee nini?

Kubwa ni kuwa utakapofika In Shaa Allah uchaguzi mwaka wa 2025 halitaingia jeshi Zanzibar kutoka Tanganyika kama ilivyokuwa kawaida miaka yote wakati wa uchaguzi.

Ulazima huu hautakuwapo.

Hili nalo nini maana yake?
Hili likipatikana maana yake ni kuwa Zanzibar itakuwa imekomboka na Wazanzibari watafanya uchaguzi huru na wa haki.

Vikosi vya kukamata Wazanzibari kuwapiga na kuwatesa katika kila uchaguzi itakuwa ni ndoto mbaya ya jinamizi.
Hili likipatikana kura itapoteza thamani ya damu ya Mzanzibari.

Katika utulivu na amani visiwani nini hali ya baadae ya Ubao wa Kisonge na waandishi wake?
Labda tulitengeneze vyema zaidi swali hili.

Hii hali ya utengamano inayoshuhudiwa hivi sasa Zanzibar imewafurahisha Wazanzibari wote?
WanaKisonge na Mazombi wamefurahi?

Wapo ambao walikuwa wananufaika sana na uadui baina ya Wazanzibari na wamenufaika kwa miaka mingi kiasi jambo hili likawa kwao wao ni ajira ya kudumu.

Wakilala wanawaza Ubao Mweusi wa Kisonge wakiamka wanawaza kazi na shughuli za Uzombi.

Hawa ghafla wamejikuta hawana tena ajira iliyokuwa ikiwaingizia kipato.
Hawa ghafla wamejikuta hawa kazi ya kufanya.

Huenda, haijulikani, huenda hawa waandishi wa Ubao wa Kisonge wakatungua ubao wao na kugawa chaki zao kwa waalimu wa madrasa.
Huenda pia na Mazombi wakatupa nondo na marungu yao kwani hakuna wa kupiga wala kutesa.

Dr. Martin Luther King alisema amefika juu ya kilima na kaiona nchi waliyoahidiwa na Mungu.
Maalim Seif wanahistoria watakapokuja kumuandika watakuwa na mengi sana ya kumuelezea.

Maalim wasaidie wanahistoria kwa wewe mwenyewe kunyanyua kalamu na kuandika kumbukumbu zako kwani jina lako limetawala Zanzibar katika kipindi kirefu na muhimu sana cha historia yake.

Walter Cronkite anasifika kuwa yeye ndiye mtangazaji wa televisheni pekee ambae amepata kuwahoji marais wa Marekani wengi kupita mtangazaji yeyote wa wakati wake.

Maalim umesimama kulikabili sanduku la kura na kila rais aliyetawala Zanzibar.
Hii ni rekodi tabu kuvunjwa.

Ulimwengu ungependa kuisikia historia hii kutoka kinywani kwako.

=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']0:00 / 0:40

Usiwaamini ccm
1. Subiri uchaguzi mwingine uje utaona rangi halisi za jinamizi ccm na najisi iliyopakwa rangi ya amani kwa ghiliba.

2. SUK sio mara ya kwanza, ni ainaflani ya ufedhuli inayotumika na ccm kwa maalim na wazanzibar wanaoamini katika haki, ukweli na demokrasia halisi.

3. Kunamifano mingi sana ya udhalili wa ccm kwa wapinzani
A. CUF
B. ACT

Lakini ccm inafahamika tangu enzi zile za mwalimu
Maalimu Seif anafaham
Abdul Jumbe anafaham
Wale wa shimoni wanafahamu

Kifupi sioni jipya ila ninachhoona ni kiini macho kufubaza malengo ya kundi la maalimu Seif kuitafuta haki kamili ya mzanzibar. Kinachoonekana sasa ni ghiliba na utapeli wa kisiasa.

Ukweli utajulikana uchaguzi mkuu ujao 2025
 
WAZANZIBARI WAMEAMKA?

Toka ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ghafla Zanzibar imebadilika na kuwatia matumaini makubwa Wazanzibari.

Yanayoonekana katika mitandao ya kijamii katika maandishi, picha na sauti yalikuwa tabu hata kufikirika kwa mbali majuma machache yaliyopita.

Waliokuwa wakitazamana kama maadui kiasi cha kufikia kusababisha watu kuteswa na kuuliwa sasa wamekuwa ndugu wanaonekana pamoja wakiwa na tabasamu huku wakipeana mikono.

Hii ni faraja kubwa kwa Wazanzibari wengi ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.

Dr. Martin Luther King katika hotuba yake ya mwisho kabla hajauawa alisema maneno haya, ''I've been to the Moutaintop and I've seen the promises land.''

Martin Luther King anasema amefika juu ya kilima na ameiona nchi ya ahadi akiwa na maana kuwa kwa yale aliyokuwa anashuhudia juu kilimani, basi huko waendako kutakuwa na nema.

Jana katika kusherehekea mapinduzi bendera za ACT Wazalendo na bendera za CCM zimeonekana katika viwanja zikipepea bega kwa bega.

Lakini binafsi lililokamata fikra yangu zaidi ni kuona video ya wanafunzi wa Muslim University of Morogoro (MUM) Chuo Cha Kiislam Morogoro wamekusanyika katika ukumbi wakisheherekea mapinduzi kwa kuimba nyimbo maarufu inayoimbwa sana katika sherehe za CCM Zanzibar.

Nyimbo hii ina umri sawa na mapinduzi yenyewe.
Haya yote yanaashiria kitu gani?

Haya yanaashiria kuwa Wazanzibari wameamua kusonga mbele katika udugu wao kwa maslahi ya nchi yao.
Ikiwa Wazanzibari wameamua kuwa kitu kimoja hii nini maana yake?

Maana yake ni kuwa Wazanzibari wameondoa uhasama baina yao.
Ikiwa uhasama umeondoka Wazanzibari wategemee nini?

Kubwa ni kuwa utakapofika In Shaa Allah uchaguzi mwaka wa 2025 halitaingia jeshi Zanzibar kutoka Tanganyika kama ilivyokuwa kawaida miaka yote wakati wa uchaguzi.

Ulazima huu hautakuwapo.

Hili nalo nini maana yake?
Hili likipatikana maana yake ni kuwa Zanzibar itakuwa imekomboka na Wazanzibari watafanya uchaguzi huru na wa haki.

Vikosi vya kukamata Wazanzibari kuwapiga na kuwatesa katika kila uchaguzi itakuwa ni ndoto mbaya ya jinamizi.
Hili likipatikana kura itapoteza thamani ya damu ya Mzanzibari.

Katika utulivu na amani visiwani nini hali ya baadae ya Ubao wa Kisonge na waandishi wake?
Labda tulitengeneze vyema zaidi swali hili.

Hii hali ya utengamano inayoshuhudiwa hivi sasa Zanzibar imewafurahisha Wazanzibari wote?
WanaKisonge na Mazombi wamefurahi?

Wapo ambao walikuwa wananufaika sana na uadui baina ya Wazanzibari na wamenufaika kwa miaka mingi kiasi jambo hili likawa kwao wao ni ajira ya kudumu.

Wakilala wanawaza Ubao Mweusi wa Kisonge wakiamka wanawaza kazi na shughuli za Uzombi.

Hawa ghafla wamejikuta hawana tena ajira iliyokuwa ikiwaingizia kipato.
Hawa ghafla wamejikuta hawa kazi ya kufanya.

Huenda, haijulikani, huenda hawa waandishi wa Ubao wa Kisonge wakatungua ubao wao na kugawa chaki zao kwa waalimu wa madrasa.
Huenda pia na Mazombi wakatupa nondo na marungu yao kwani hakuna wa kupiga wala kutesa.

Dr. Martin Luther King alisema amefika juu ya kilima na kaiona nchi waliyoahidiwa na Mungu.
Maalim Seif wanahistoria watakapokuja kumuandika watakuwa na mengi sana ya kumuelezea.

Maalim wasaidie wanahistoria kwa wewe mwenyewe kunyanyua kalamu na kuandika kumbukumbu zako kwani jina lako limetawala Zanzibar katika kipindi kirefu na muhimu sana cha historia yake.

Walter Cronkite anasifika kuwa yeye ndiye mtangazaji wa televisheni pekee ambae amepata kuwahoji marais wa Marekani wengi kupita mtangazaji yeyote wa wakati wake.

Maalim umesimama kulikabili sanduku la kura na kila rais aliyetawala Zanzibar.
Hii ni rekodi tabu kuvunjwa.

Ulimwengu ungependa kuisikia historia hii kutoka kinywani kwako.

=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']=AZW0iGr_6_KW1300ZjYuurjs0la-NTNJf7CP6Kchqm5pnC7EeQNUucVzcfK-slSWu1uX3U1f_jf1am8v5y-eb5uZnZT2dGi1CD_dpHQAPX541KKe9O19thDHDJ8ppWvshlU&tn=*bH-R']0:00 / 0:40

Wanalumumba mnajitejenya na kukenua , nyie mbwa mliotumia Hadi bomu kurushwa kwa mkono kwa raia, inhumane savages
 
Mohamed Said na ww pia umekamatika kwenye hiyo ghiliba ya ccm? Au kwakuwa Maalim Seif kapata mlo kwako unaona ni sawa? Kwahiyo hapo umehalalisha wapinzani waendelee kuuwawa kisha baada ya uchaguzi wataelewana kwa viongozi kupewa vyeo? Nimesikitika kwa bandiko hili kutoka kwa nguli kama wewe!
 
"Nyimbo hii ina umri ......"!!!! usahihi ni " Wimbo huu una umri...." .Hata nyie Wazee mnaendeshwa na swaga za Bongofleva! Bure kabisa!
Halafu wewe Mzee Mohamed Said ni mbaguzi na mdini sana!

Kauli ya kwamba Jeshi kutoka Tanganyika kuingia Zanzibar! Ni kauli ya kijinga na kibaguzi sana kutoka kwa mtu mpuu.zi!

Suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano,sasa unaletaje kauli za kijinga kama hizi?!

Kwani huwezi kuelezea mafanikio ya Zanzibar bila kuchochea ubaguzi ndani ya Muungano.

Utaendelea kusikilizwa na wapuuuzi wenzako!
Hil.mbn lipo mkuu ubaguz tenh kwa wazanzbar
 
Mohamed Said na ww pia umekamatika kwenye hiyo ghiliba ya ccm? Au kwakuwa Maalim Seif kapata mlo kwako unaona ni sawa? Kwahiyo hapo umehalalisha wapinzani waendelee kuuwawa kisha baada ya uchaguzi wataelewana kwa viongozi kupewa vyeo? Nimesikitika kwa bandiko hili kutoka kwa nguli kama ww!
Tindo,
Huenda umesoma kwa haraka.
Jitulize usome upya.
 
Hata baada uchaguzi wa 2010 tulizishuhudia sinema mfano wa hizo lakini baada ya kuja mchakato wa katiba mpya kila upande ulishikilia maslahi yake ya kisiasa.
  1. wengine waliimba serikali mbili kuelekea moja
  2. wengine waliimba mkataba
baadae wote wanakutana kwenye baraza la mapinduzi
 
Hii kitu tunahitaji Bara. Japo itakuwa inaiba lakini basi chama cha kikuu cha upinzani na chenyewe kipate kula itasaidia kupunguza kelele na manung'uniko.
Kwahiyo wapinzani wao kumbe wanataka kula tu
 
"Nyimbo hii ina umri ......"!!!! usahihi ni " Wimbo huu una umri...." .Hata nyie Wazee mnaendeshwa na swaga za Bongofleva! Bure kabisa!
Halafu wewe Mzee Mohamed Said ni mbaguzi na mdini sana!

Kauli ya kwamba Jeshi kutoka Tanganyika kuingia Zanzibar! Ni kauli ya kijinga na kibaguzi sana kutoka kwa mtu mpuu.zi!

Suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano,sasa unaletaje kauli za kijinga kama hizi?!

Kwani huwezi kuelezea mafanikio ya Zanzibar bila kuchochea ubaguzi ndani ya Muungano.

Utaendelea kusikilizwa na wapuuuzi wenzako!

Ni kweli jeshi limetoka Tanganyika na vifaru, na wengine wamekodiwa kitoka Rwanda au Burundi wakapelekwa Pemba.

Wameuwa bila hata kifikiri kuwa hawa ni ndugu zetu, wameuwa kama vile wanauwa nyumbu.

Ipo siku ina mwisho
 
Cha ajabu wauwaji na waliouliwa ndugu na jamaa wameungana.

Sasa inashangaza kidogo.
 
Back
Top Bottom