Wazanzibari wakesha kuiombea dua Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazanzibari wakesha kuiombea dua Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 25, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on April 25, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Masheikh wakiomba dua ya pamoja kumuomba Mungu ili kujenga nia moja katika mambo yote, baada ya kumalizika kikao hicho leo jioni kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi kati ya viongozi wa dini, jeshi la polisi, wanasiasa na serikali ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Abubakari Khamis alizungumza na pande zote hizo kuelezea mchakato wa Katiba mpya na mihadhara inayofanywa sehemu mbali mbali za Zanzibar huku akisistiza uhuru wa kutoa maoni usivuke mipaka na kusababisha machafuko. lakini alisema maoni yalenge kuimarisha mfumo tuutakao na sio kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

  Wazanzibari nyote ulimwenguni wa kike na kiume, wakubwa na wadogo mnatakiwa kukaa na kusoma kisomo hichi maalumu cha leo ambacho huku Zanzibar kinakaliwa katika Masjid Afraa wa Kidongo Chekundu kwa wanaume na Masjid Jibril kwa wanawake lengo ni kumkabidhi Mwenyeenzi Mungu (s.w) shida zetu pia kumuomba na kumuelekea kwake Mwenyeenzi Mungu katika mambo yote. Rehma na Amani zinatokana na yeye hivyo hatuna budi kumtegemea na kumuomba sana katika kikao hichi cha leo. Kwani kama alivyoahidi mwenyewe Subhannah aliposema Niombeni nitakupeni basi nasi tunainua mikono yetu kwako ya Yarabbi na hatuna mwengine wa kumuomba zaidi yako tutakabalie dua yetu hizi na utufungulie mambo yetu na utunyooshee kwa baraka na utukufu na usiku huu hakika ulitakalo wewe huwa. Baada ya hapo tia nia yako na usome kama utaratibu wa dua hii unavyoelekeza:
  Dua ya kuiombea nchi yetu salama na amani na kuiepusha na shari na hasad
  Nia yake ni kumuomba Mwenyeenzi Mungu aungo’e mfumo huu wa dhulma unaoitwa Muungano na kila anayeikusudia Zanzibar na wazanzibari na waislamu wote duniani uhasidi na ufisadi tunamkabidhi Mwenyeenzi Mungu (s.w) awarudi.
  Visomo hivi vitafanywa kwa mujibu wa watu na hali zao. Na katika nyakati tofauti na mwahala tofauti. Waislamu hii ndio nguvu yetu, silaha yetu, mabomu yetu tusifanyie mzaha.
  Mtume (s.a.w) amesema dua ndio ubongo wa ibada. Mambo yetu ili yafanikiwe lazima tuyafunganishe na dua, na sadaka, maombi yetu tumkabidhi Mfalme wa watu mwisho wa Majabari, Asiyeshindwa na kitu na anapoamua lake husema Kun Fayakun, baina ya Kaf wa Nun. Kuwa limekuwa hakuna wa kulizuwia.
  Vinapofanywa visomo hivi mtu ahusishe nia iliyopo hapo juu, pamoja na matatizo yake binafsi inshallah faraja kubwa itapatikana.
  Visomo hivi vinahitajika kufanywa vyuoni, misikitini, majumbani na kwenye hadhara mbali mbali za kheri, mtu peke yake au kikundi na watafanya kwa idadi ndogo ndogo au idadi kubwa pia inakubalika.
  Idadi kubwa kuanzia 313-1,000, 3,000, mpaka 50,000 idadi hii ni idadi ya malaika aliowateremsha Allah katika vita tofauti kuwanusuru waislamu kwa mujibu wa nususi ya Qur-an Kareem.
  Idadi ndogo ni kuanzia 70, 40, 21, 11, 5, 3, 1 na katika hali nyengine ya witri muhimu mtu achunge nidhamu ya usomaji na idadi yake tunapendekeza kwa kila chuo kiwe na utaratibu huu wakifika asubuhi na ikiwezekana miskitini kila baada ya sala kwa wakati huu tulokuwa nao wakasoma japo mara moja moja mpaka Mwenyeenzi Mungu atakapotupa lile tulokusudia.
  Visomo hivi viendelezwe ndani ya nchi na nje ya nchi mpaka waislamu wapate ushindi na visomo vimaliziwe kwa dua ya Qunut.
  Utaratibu wa kusoma kama ifuatavyo:
  Istaghfar 100 kumuomba Mwenyeenzi Mungu msamaha kwa makosa yetu
  Sala za Mtume 100 kupata rehemu kutoka kwa Mwenyeenzi Mungu. Mpaka 1,000
  Surat Raad aya ya 13 mara 70
  Tafsiri ya aya ni hii hapa: “Na Radi inamsabihi Allah kwa kumshukuru na (pia) Malaika (husabihi) kwa kumuogopa, na (Allah) hupeleka mapigo ya radi na kumpiga nayo amtakaye. Na hao (Makafiri) wanabishana juu ya Allah (kuwa yuko kweli au hayuko) na hali (ya kuwa yuko na) yeye ni mkali wa kuadhibu”. Mwisho wa Aya hiyo.
  Sura nyengine zitakazosomwa kama ufuatavyo:
  Alamtara mara 70 kwa ajili ya kupiga ubaya na kudhalilisha vitimbi vya makafiri
  Idhaa Dhuldhilat mara 70 kwa ajili ya kung’oa na kutawanya
  Tabatyadaa mara 70 kwa ajili ya kuangamiza na kila kitu chake
  Kulhuwallahu na kul-adhu birabbi Naas mara 70 kwa ajili ya kumtakasa Mwenyeenzi Mungu (s.w)
  Falaq mara 70 kwa ajili ya kutakasa ulinzi na kujilinda na hasadi na shari za watu.
  Lahaula wala quwwaata illa Billahi Aliu—Ladhiym Ni kumpa Mwenyeenzi Mungu mamlaka yake hakuna hila wala nguvu isipokuwa kwake.
  Almnashrah mara 70 ni kwa ajili ya kuwepesisha na kufungua yale mazito tunayoyataka kama Mwenyeenzi Mungu alivyomfungulia Mtume wetu Muhammad (s.a.w).
  Alhamdu mara 70 Ni kumtegemea Allah (s.w) na kufungua na kumuomba atuelekeze katika njia iliyonyooka kufika katika lengo letu.
   
 2. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on April 25, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar khamis Bakari akifafanua jambo katika mkutano na Baadhi ya Masheikh wa Jumuia za mbali mbali Kiislamu za Kiislam kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na Mihadhara inayofanywa sehemu tofauti Unguja na Pemba. Kulia yake ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed na kushoto yake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.
   
 3. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Waoga wakubwa nyie Wazenji. Badala ya kuchukua hatua za kuvumja muungano huu wa kidhalimu eti mnakaa kufanya swala, mnasalia nini sasa? Mungu huyohuyo mnaemuomba ndio amewapa ubongo wa kufikiri na nguvu za kufanya.
  Acheni uadealism na mfanye vitu kwa kutumia uwezo mliopewa na Mungu siyo mnakaa eti mnamsubiri Mungu afanye. Mtangoja milele na mtakufa bila kelele woga wakubwa.
   
Loading...