VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Wakaazi wa Zanzibar wapo kwenye mkwamo na mgagaziko mkubwa. Huku wakiwa kwenye giza totoro juu ya sintofahamu ya uchaguzi wa Urais,Wawakilishi na Madiwani,bei ya vyakula nayo yawa pigo lingine. Wanajutia demokrasia.
Taarifa za kuaminika toka Zanzibar zinaonesha kuwa bei za vyakula zimepaa na kufanya maisha ya Wazanzibari kuwa magumu. Kilo ya nyama ya ng'ombe na mbuzi,kwa mfano ni kati ya 12000 na 15000 tofauti na 8000-9000 iliyokuwa mwanzoni.
Bei za vyakula vyote zimepanda maradufu. Kupanda kwa bei kumechagizwa na kupungua kwa bidhaa za vyakula kuingizwa kutoka Tanzania Bara kutokana na hali isiyoeleweka wala kutabirika huko Zanzibar. Wazanzibari ni ndugu zetu,wasaidiwe kisiasa na kiuchumi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam