Samia Suluhu Hassan: The economy architect

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Wakati Rais Samia anapokea kijiti nchini yetu ilikuwa kwenye mkwamo tunaweza sema hali ilikuwa ni mbaya sana, Virusi vya Corona vilikuwa vimeshika kasi tulikuwa hatuna option zaidi ya kupiga nyungu na watu wengi walipoteza maisha.

Tatizo la ajira lilikuwa ni kama limekolezwa moto zaidi maana Biashara nyingi zilifungwa na matokeo yake vijana walipoteza ajira, Moto juu ya kidonda.

Balaa la mabadiliko ya tabia ya nchi kupungua na kupata mvua za wastani kusababisha mavuno kidogo kusababisha upungufu wa chakula nchini.

Ni wazi Rais Samia alipokea kijiti huku uchumi wa nchi ukiwa unakimbia shimoni kutoka kwa mtangulizi wake. Miradi mikubwa yenye kuhitaji gharama kubwa kiutekelezaji. Hata uzalishaji viwandani ulishuka kutokana na kuwepo kwa wasiwasi mwingi kwa wawekezaji na wengi walikimbia nchi kutokana na sera mbovu ya kidplomasia.

Ni takribani siku mia tano na sitini 560 za utawala wa Rais Samia amelipa Taifa sura mpya kizungu tunasema set our Nation on a new course.

Agenda ya Rais Samia ameitransform nchi kwenye uchumi wa kuridhisha na kurejesha matumaini mapya ya Ujenzi mpya wa Demokrasia, Maridhiano, na utekelezaji ambao umetoa sura nzuri kwenye uwekezaji, ubunifu na future ya maendeleo kama nchi wapi tunakwenda.

Through bold and decisive action, Agenda ya Uchumi ya Rais samia imetengeneza uimara na usawa kwenye kufufua uchumi wetu ambao ulikuwa unakwenda shimoni. Ilifika mahali nchi ilikuwa haikusanyi tena zaidi ya kunyang’anya, kuteka na kukwapua kwa wafanyabiashara.

Rais Samia ameandika historia kwenye kizazi cha uwekezaji na diplomasia ametengeneza nafasi za ajira nje ya mfumo rasmi kupitia sera ya mashiriakiano na Sekta binafsi kuhakikisha watanzania wengi wanapata ajira nzuri leo na kesho.

Tumeuona Uimara wa Rais samia kwenye mzozo wa vita vya Ukraine kupanda kwa bei ya mafuta kuliko sababisha Dunia uchumi wake ucheze hili ni janga la Dunia ndiyo maana waswahili wanasema kipimo cha unahodha si kutia nanga ufukweni bali akiwa amevuka mawimbi mbalimbali baharini, yanatoa picha ya aina ya nahodha uliyenaye.

Mawimbi ya uchumi yalipo kuja Samia alikuwa amekwisha jiandaa moja kupunguza bei ya mafuta kwa kutoa ruzuku ya bilioni 100 kila mwezi kupunguza ukali wa bei kuweka ruzuku katika bei ya mbolea zipatikane kwa nusu bei na tatu kuondoa kodi ya zuio kwenye viwanda vya ndani vinavyozalisha mafuta ya kula.

Top priority kubwa ya Rais Samia ni kuhakikisha mfumuko wa bei unapungua si jambo la usiku mmoja lakini unaweza kuona ni kwa jinsi gani amewekeza kwenye Bajeti ya kilimo 2022/23 kushusha mfumuko wa bei kunahitaji kufunga mkanda kwenye uzalishaji.

Mfumuko wa bei ni janga la kidunia kwasasa hapa kwetu japo si kwa ukubwa hii inatokana na upungufu wa bidhaa muhimu hususani vyakula kutokana na upungufu wa bidhaa hizo. Kuliko sababishwa na mismatches between supply and demand pamoja na bei ya nishati hususani mafuta ya kuendeshea mitambo na magari kwenye usafiri kuwa juu na
bei ya vyakula kupanda. Kuondoa hili hatuna budi kupandisha uzalishaji wetu.

Lengo la kuongeza bajeti ya kilimo na incentive zake ni kuwafanya watu wavutiwe zaidi kwenye kilimo Serikali imetoa mashamba, imetoa ruzuku ktk mbolea na pembejeo, serikali imetoa mtaji kwa wakulima, serikali imehakikisha upatikanaji wa masoko ya bidhaa zitakazo zalishwa.

Ukitazama anachokifanya Rais Samia kwenye uchumi wetu ni jambo la kihistoria kuufanya uchumi unaoweza kumfaidisha kila Mwananchi mmoja mmoja na kuwa na Uchumi imara. Hakuna mwananchi hata mmoja atakayeachwa nyuma ni uchumi jumuishi na shirikishi wa kuwainua watanzania wote kwa pamoja.

Fursa za uwekezaji kwenye Kilimo utagundua kabisa Rais Samia ni mchumi halisi anataka tufike mahali atuagizi tena bidhaa za mafuta ya kula ambazo kila Mwaka tunatumia zaidi ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa ajili ya kuagiza mafuta ghafi ya kupikia. Lengo na sisi tuweze kuuza nje zaidi kuongeza pato la Taifa.

Unapofanya mageuzi ya uchumi kutoka chini na kati ni kuhakisha uchumi unaojenga unawanufaisha wote. Samia anatengeneza mifumo ya kisera ambayo inahakikisha nguvu kazi inalindwa na uzimamizi wa rasilimali na utawala ni wa kuheshimu utu wa watu pamoja na kulinda haki za kila mmoja wetu.

Sera ambazo zinatuvusha kwenye ukuaji wa uchumi wa 5.4 kwenda juu kwa kasi na kwa haraka. Sera zinazowainua wafanyakazi na maslahi yao kama alivyofanya kuondoa retention fee kwa wanufaika Elimu ya juu, kuongeza kikokotoo na asilimia 23.3 kwa kima cha chini.

Kwa haya machache ni wazi utaona Rais Samia ni mchumi wa hali ya juu ni kweli angeweza kuachana na miradi mikubwa kama SGR, Mwalimu Nyerere HEP, sababu ni gharama ila ameona ipo haja na umuhimu wa kumaliza hii miradi. kutoka kwenye mbinu pekee iliyotumika kwa mtangulizi wake kuijenga kwa ukwapuaji, mikopo iliyofichwa kwa propaganda ya fedha zetu za ndani. Kama nchi kiuchumi tulikuwa pabaya kama nchi.

Samia tunaweza tukasema ni Economist Architect, fundi sanifu hasa ametuondoa kwenye mkwamo pasipo kupiga kelele nyingi kuondoa mifumo kandamizi ya ukusanyaji wa kodi na mapato mengine kisheria, Amelinda watu wa hali ya chini kutoka kwenye madhila ya ufukara Ujenzi wa madara 15000 nchi zima vituo vya afya 400 na sasa anakwenda kujenga madarasa 8000 mapya hapa utaona ni namna gani revolving fundi inavyokuwa kubwa hapa zungumzia na miradi ya maji miji ishirini na nane. Utengenezaji wa Filamu ya Royal Tour na Utalii ukarejea.

Usanifu wa Samia kwenye kujenga uchumi ni pamoja na kuhakikisha Public Investment hazidondoki kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati hadi kwa wawekezaji wakubwa na wale wadogo Maarufu kama machinga wanapata haki yao.

Matarajio makubwa ya Rais Samia ni kuona kama nchi wafanyabiashara wadogo wanainuka juu kwa kuhakisha mamilioni ya shilingi kutoka mfuko wa uwezeshaji Vijana, Wanawake na Wazee yanatolewa kwa wakati kuchangamsha supply chain.

Ufundi Sanifu wa kiuchumi wa Rais Samia ameongeza incetives zinazotanua Public Investment kwa kuhakikisha utawala unajenga mazingira mazuri ya ulipaji kodi na kuzuia wakwepa kodi.

Chini ya Rais Samia Uchumi wetu hauwezi kurudi kule tulipotoka ndiyo maana anataka kutimiza 4Rs - Reconciliation, Resiliency, Reforms, na Rebuilding
 
Back
Top Bottom