Serwa yangu ni kama ifuatavyo:
1. Sasa hivi kila siku wanakamatwa watanzania kuanzia wawili na kuendelea kila kona ya dunia, wanakamatwa na madawa ya kulevya, na wanaondokea pale dar airport; hii sio news wala aibu wala kuvunja amani na utulivu. Ni sawa, so long wamefanya watanganyika. Mpaka Rais wa nchi, Kikwete amekaa kimyaaaaa, kama hakuna kitu.
2. Kuna makontena mengi ya madawa ya kuelvya yamekamatwa nchi Fulani (xxx) yametokea bandari ya dar na mengine Zenj (serikali zote mbili, kimyaaaaaaaa), hili ni la jana na juzi tu, sio yale ya miaka ileeeee. La hasha, jana na leo Bob Ally.
3. Kuna wafanyabiashara wanapigwa risasi kama mithili ya kuuwa popo, na yule mhadhir wa UDSM jana tu, ameuwawa kikatili (polisi kimya, na Said Mwema bado ni IGP) though haya yote yanamgusa yeye moja kwa moja na Nchimbi bado anabaki kama waziri wa mambo ya ndani. Nakumbuka Mwinyi, Natepe na wengine wengi walijiuzulu kw amakosa madogo madogo tu, seuze kama haya.
4. Sheikh mmoja ametiwa acid kule Arusha (nadhanu arumeru) kimyaaaa.
5. Intelligence ya hapa na polisi yake, imejifunga pahala pamoja tu: Uamsho au udini kwa nini wasiende mbali katika uchunguzi wao (watuambie cause ya mauwaji wa padre Evarist Mushi, kupigwa risasi kwa padre Mkendo, na hawa waingereza wawili: nini kinaendelea ndaini ya kanisa hapa Zanzibar, kwani makosa wanafanya muslim extremists tu, je, hakuna extremism katika christianinty, au hakuna dirty game ndani ya kanisa, foul play
..)? hebu polisi mtuambie mlinasa nini siku ya maziko ya padre Mushi (funueni pazia kidogo tujue): ukimya wa taasisi zetu ndio inafanya wengine tuendelee kuwa na shaka na utendaji wenu.
6. Mfanya baishara dar ametiwa acid, jana yule tajiir wa mererani pia alipigwa risasi ishirini polisi kimyaaaaa, na bado Said Mwema yupo, bado nchimbi yupo
.hee jamani huu uoza umeanza top-down ndani ya uendeshaji wa serikali.
7. tukumbuke kuwa tumeruhusu vikundi viovu vingi hapa Zanzibar kwa jina la vyama vya siasa, na tusisahau kuwa tumekuwa na eti na polisi jamii kila kona hapa Zanzibar, lakini uhalifu unazidi? kwa nini, na hasa mji mkongwe
..hawa polisi jamii ni nani, tumewaamini vipi sawa trust them, but also control them, tumewaachilia sana, na hasa mji mkongwe, mpaka sasa wameota pembe wanakusanya kodi, malipo kila kona ya mji under different names. Tunaachilia uzoa wa kila aina katika jamii yetu, matokeo yake ndio haya. Tumeruhusu uvunjaji wa sharia, sasa tunavuna matokeo yake. n.k n.k n.k nk