Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,157
- 31,334
Kuna rafiki yangu mmoja, kati ya mwishoni mwa miakaya 90 na mwanzoni mwa mwaka wa 2000 alizamia kwenda Ulaya. Safari za kipindi hicho ilikuwa za kibabe kweli mtu anaanza safari hana hata passport. Safari ilimpeleka mpaka Libya lengo ni kwamba ilikuwa aingie Morroco then wavushwe kuelekea Spain.
Katika safari hiyo alikutana na majanga mengi sana sana. Amenusurika kufa zaidi ya mara 20 tena akiwa ameshaona kaburi.
Sasa anadai akiwa Libya, anadai walibya ni wabaguzi sana hasa kwa Waafrika wenzao weusi. Anadai ukipanda usafiri wa umma wanawake walikuwa wanaziba pua. Anasema muda mwingine ulikuwa ukipita mtaani unaona mama anaokota jiwe anampa mwanae akurushie.
Anadai sasa kimbembe uje ukutane na vijana walikuwa wanajiita Aska Boys (sina hakika kama nimewapatia). Anasema walikuwa wanatabia wanakuja na magari wanakuweka mtu kati, wanafungua boot wanatoa marungu, watakupiga mpaka ufe.
Sasa anasema akiwa Libya, alikuwa hana pesa kabisa na kutoka Libya ili uvushwe uende Morocco mpaka upande boat kuendelea na safari, ilikuwa inahitajika pesa nyingi. Yeye kwa muda huo aliikuwa ashageuka kuwa kama chokoraa. Na kipindi hicho mauaji kwa wageni yakawa yameongezeka.
Anadai katika kundi lao allikuwepo jamaa katoka Ethiopia ni Muorthodox alikuwa akisali sana sana. Jamaa akamfuata akamwambia amsaidie pesa kidogo ili aweze kuondoka pale maana wenzake walikuwa wengi wao wana mpango wa kuondoka baada ya hali kuwa mbaya.
Jamaa eti akamuuliza, huna mtu anayeweza kukutumia pesa. Jamaa akamwambia sina ila kuna kaka yangu ana pesa nyingi sana ila hawezi kunipatia pesa maana hata hii safari nimeianza kwa kumkumbia yeye alikuwa anataka kuniua. Jamaa akamwambia, usiku njoo nikufanyie maombi, lakini iwe saa tisa usiku.
Kweli usiku wa saa tisa akaenda, eti jamaa akachora chora mviringo sakafuni akamwambia aingie kati, kisha wakaanza kumuombea yeye na wenzake.
Baada ya maombi akamwambia asubuhi kampigie simu kaka yako, mwambie akutumie dollar 2000, atakutumia. Usipunguze na wala usiongeze. Jamaa anadai kesho yake akaenda sehemu ya kupiga simu akampigia simu kaka yake, alipomueleza hakubisha kabisa ila akamwambia atamtumiaje ile pesa.
Kipindi hicho anasema Libya kulikuwa hakuna huduma za Western Union, wala Money Gram. Anadai watu walipokuwa wakitaka kupokea pesa, kulikuwa na mzungu raia wa Spain pale ana ofisi iko kisiwa cha Lampedusa, hivyo pesa inatumwa kwenda Lampedusa, akiconfirm imefika kule unaenda kwake anakupa cash pale Libya.
Basi jamaa akawa ametumiwa pesa akaondoka pale. Japo huko mbele alipata majanga mengine.
Jamaa alifanikiwa fika Mexico, Equador na huko pia alipata majanga hadi akapoteza korodani baada ya kuanguka mikononi mwa drug dealers.