Wazamani amerudi

Wazamani amerudi

Nyrum

Senior Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
124
Reaction score
41
Habari zenu wanajamvi, kuna rafiki yangu kaniomba ushauri nimeshindwa nimshauri vipi kuhusu tatizo lake, naomba tushirikiane kumshauri, yeye pia yumo humu anasoma ushauri wenu.

Yeye aliolewa miaka 6 iliyopita, mumewe amemnyanyasa sana, katika ndoa yao walibahatka kupata watoto watatu na walifunga ndoa ya bomani.

Waliposhindwana mwaka jana wakaachana kwa talaka.

Dada wa watu kalea watoto wake vzur tu bila kuwa na mwanaume, sasa wiki iliyopita kakutana na boyfriend wake wa primary na ni anampenda hatare afu hawajawah kugegedana! Jamaa hajaoa bt alikuwa anasoma nje, karudi ndo kafungua kampuni yake.

Walipokutana na huyo best yangu jamaa kamwambia best yangu bdo anampenda sana tu so anaomba wafunge ndoa ya kiislamu, mdada muislam jamaa mkristo bt jamaa yupo tayar kubadil dini amuoe mdada huyu.

Kasheshe sasa, mume walieachana nae amerud anaomba msamaha warudiane wakafunge ndoa upya walee watoto wao! Sasa rafik yangu amebaki dillema hajui afanye nini, yule wa primary ndo anampenda wanapendana tangu watoto wadogo, haya mume nae ndo karudi anaomba msamaha yaishe.

Mawazo yenu please wandugu
 
Atazame moyo wake....maana kipendacho roho......
 
Atazame moyo wake....maana kipendacho roho......

Nikwel usemacho ndugu, bt utata upo hivi, anampenda sana jamaa wa primary , na aliekuwa mumew ndo anataka watoto wasikose malezi ya baba na mama kwa pamoja!
 
Maamuzi ya staki nataka hua hayana mwisho mzuri...
 
Ha ha ha...Hapo 'kampuni' ya mshikaji imeleta mtanziko!!
Yaani Mwanaume anakwambia atalea Watoto watatu na mke juu!!
Mwambie rafiki yako aache tamaa, aangalie hatma ya Watoto kwa sasa, iwe ni kumrudia
Mume wake (kama amejirekebisha) au kukubali kuishi peke yake.
 
Huyo wa primary ana mapenzi mpaka hivi ukubwani dah!, mimi niliosoma nao primary hata sjui wapo wapi saivi, ila namkumbuka sana Mayasa, haya mwambie dada huyo kusuka au kunyoa nywele ni za kwake mwenyewe anajua afanyeje
 
Hii stori haiko sawa mahali. Kwamba bf wa primary karudi halafu amefungua kampuni (Hii ina uhusiano gani labda?). Halafu yuko tayari kubadili dini ili tu amuoe bidada alieachika na ambaye tayari ana watoto 3? (Inaonekana ana mapenzi makubwa sana huyu).

Hebu fanya marekebisho kidogo ili ifanane na ukweli nitachangia.
 
Si alishaolewa na mume wake yupo na watoto wanao tamaa ya nini??
 
ana 3 kids..kijana hana hata mtoto...sorry huyo kijana msukuma au mkurya? kama ni kati ya hayo makabila he could be for real...else atashaaa muda si mrefu....
 
Siku hizi ukitongoza unaingia na gia kubwa ya 'tufunge ndoa'. Ukishatoa papuchi unaisoma namba
ana 3 kids..kijana hana hata mtoto...sorry huyo kijana msukuma au mkurya? kama ni kati ya hayo makabila he could be for real...else atashaaa muda si mrefu....
 
hii hadithi mbona kama haina ukweli yaan too good to be true?
 
Hadithi haina ukweli hiyo. Kaachika na 3kids. Jamaa anarudi na atake kubadili dini kwa mtu mwenye watoto watatu?
Mwenye mmoja tu unajiuliza mara mia.
 
MBINGUNI HAKUNA KUOA KUOLEWA wote mwawa malaika na KUMTUKUZA MUNGuu....
 
Huyo mwanamke anahemea pumzi ya wanaume eeeh???
aachane na huyo kijana wa primary kwanza atakuwa kishaonekana mbibi kwake, kama anataka ndoa arudi kwa mme wake!!!
 
Amsome huyo jamaa wa primary kwa muda, watu hubadilika ati. Na usikute hata kawa deported kwa kosa kubwa tu i.e wizi etc
 
si umesema huyo wa primary hawajawai kula tunda eeeh?
basi mwambie ampe alafu sikilizia then utarudi kutupa updates kama bado msimamo wa huyo kijana uko palepale?
 
Mwanaume aninyanyase bado aje aombe msamaha halafu ndoa ya bomani my god katokea kijana yupo tayar nisietaka kutuliza akil nan najisogeza tartibu huyo walieachana kwa talaka naona akimrudia n sawa na kurudisha matapishi mdomoni uliyokwisha tapika
 
Back
Top Bottom