Wazaliwa wa kwanza wenzangu njooni

mamkuu5

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,139
716
Salama watu wa Mungu,
Poleni na mihangaiko ya maisha baada ya hayo kama kichwa kinavyoeleza,mwenzenu ni mkubwa kwetu nahitaji msaada maana wadogo zangu wanataka kunirusha akili.
1.anaenifuatia ni binti ameolewa akiwa mdogo tu miaka 19 aliozeshwa baada ya kutaka kuolewa na jamaa ambae Mlezi Wetu hakumuelewa hivyo walizubaishwaje sijui akaozwa kwa family friend ,sasa jamaa wa kwanza karudi na nguvu ya ajabu anamtaka tena bila kujali amezalishwa au VIP,anasema atarudisha mahali anataka mwanamke wake,dogo kanyamaza hasemi kitu Ila nahisi Jana alienda kumpa tunda,maana tulikua kwenye party akapotea gafla akarudi after one hr akiwa valuvalu,waliomuona wanasema alichukuliwa na gari kwa maelezo baada ya kubana alianza kulia akisema siwezi kumuacha..nipo njia panda Shemeji ni mstaarabu hata sijui jinsi ya kumuangalia sielewi.
2.Huyu ndo nahisi ntarukwa akili kabisa ,ana hela ya ajabu,Jana kama na hati tatu moja ya eneo la heka 5 mkuranga na mbili za Nyumba zote nikiwa original mpya na zina majina Yake,ni binti wa chuo kikuu anamaliza this year pacha wake ni mwanaume nae wapo wote chuo huyu akaunti Yake INA hela ndeeefu sijui nimetoka wapi nilifikiri labda kwanza tabia za ushoga nilipomwambia kwenda hospital alijiskia vibaya akanionesh mwanamke wake Ila hakutaka maswali zaidi ,anashirikiana na pacha wake nawalipia ada wote wawili sijui Mimi mwenzenu hela ilipotoka wote hawasemi.nimefuatilia mirathi wala haijaguswa IPO vizuri tu sielewi,biashara haramu hawana yaani....
3.hawa ni mapacha pia wote wanaume Ila wameondoka nyumbani wana mwaka wapili nawasiliana nao Ila sikua nimewahi kua walipo na wana fanya nini walimaliza form six ,Jana katika group la kilimo nililopo aliungwa mmoja akaanza kutangaza biashara ya Kuku wa kienyeji amewapiga picha anasema anao 3000 sielewi namsihi arudi nyumbani na mwenzie,
Kama wapo humu naomba warudi tuyaongee ,naelemewa hisia
 
Mbona tulifundishwa somo la Mwandiko (Drs la 1 & 2), Kuandika Imla (Kuanzia Drs la 3..), Insha nk?.

Kwanini unashindwa kuwasilisha mada ili isomeke na kueleweka vizuri?.
 
Ingawa nimesoma kwa tabu ila nimekuelewa kidogo, una wadogo 5 ambao pacha mara 2 na 1 kazaliwa peke yake.

Hao wanaosoma chuo kikuu wana hela ndefu na hujui wamezitoa wapi? Mkuu naamini wewe ni mtu mzima unaeza kuwaita ukaongea nao au ukawaita watu wazima wakawauliza kama una wasi wasi sana na vyanzo vyao vya mapato.

Kuhusu hao mapacha wa 2, Kwanini unawasihi warudi nyumbani wakati wapo wanatafuta kipato na umeona kabisa hapo wanauza kuku?

Mwisho, siku nyingine andika vizuri.
 
Umeandika kitu gani wew.,, Yani hata cjakuelewa, Jua kupanga aya zako na mawazo kwenye vizuri bhn unapotaka msaada.
 
Mkuu, hariri habari yako kabla ya kuiwasilisha humu. Binafsi nimeelewa kidogo.
 
Back
Top Bottom