Wazabuni wamlilia Rais Magufuli, tunadai Shilingi milioni 600

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Wazabuni wamlilia Magufuli kupata fedha walizo tumia kulisha shule ya sekondari ya ilboru iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha kiasi cha shilingi million 600.

Wakizungumza na vyombo vya habari wazabuni hao, Elipendeza Mushi amesema kwamba kwa muda takribani miaka 7 walitoa huduma za kulisha wanafunzi shuleni hapo lakini mpaka sasa hawajapata chochote .

Elipendeza amesema kwamba madai hayo wamekuwa wakifuatilia kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha lakini wamekuwa wakipata majibu kwamba halmashauri hiyo haiwezi kulipa fedha hizo kutokana na kuwa makusanyo ya mapato ya halmashauri hayo hayatoshi .

Mzabuni mwingine Sabasi Swai ameomba Mheshimiwa Rais kusaidia waweze kupata fedha zao kwani walifanya kukopa fedha benki kupata mtaji wa kulisha wanafunzi hao.

Amesema kuwa, fedha hizo zimewaletea changamoto kubwa ikiwemo kutaka kuuziwa kwa nyumba zao na benki na baadhi ya mali wanazomiliki ili waweze kulipa madeni hayo jambo ambalo mpaka sasa wanaishi katika mazingira magumu ya kuendesha familia zao .

Aliongeza kuwa,mpaka sasa wamesha zungunga wizara ya fedha pamoja na tamisemi bila kupata majibu ya kulipwa fedha zao na kuomba Mh Rais kuingilia kati kupata fedha hizo

"tunaomba Mh Rais atusaidie kupata fedha zetu kwani tunaishi maisha magumu sana, tunashindwa kusomesha watoto maana nguvu kubwa tuliweka katika biashara hiyo na Sasa hivi tunashangaa hatulipwi hela zetu na Hali zetu zinazidi kuwa mbaya tunaomba Sana serikali itusaidie."alisema .

Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Alivera Ndebagoye alikiri kupata barua ya kulipa fedha hizo lakini ameshindwa kutokana na halmashauri hiyo kukusanya fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kujiendesha pamoja na kulipa madeni .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro amekiri kutambua madeni hayo na kuomba wananchi hao kuwa na uvumilivu kwani swala hilo limesha fika mikononi mwake na halmashauri imeshindwa kulipa kutokana na kukusanya mapato kidogo na deni hilo kuwa kubwa .

Muro amesema katika serikali ya awamu ya tano ya John Pombe Magufuli hakuna mzabuni atakaye kosa pesa zake maana tayari Mh Rais alielekeza madeni yote kufanyiwa uhakiki na wizara ya fedha kufanyia malipo .

"Nakiri hizo fedha ni za muda mrefu hivyo niwaombe tu mama zangu na baba zangu kuvuta subira kulipa hizo fedha kwani uhakiki wa Madai yameonekana hayana tatizo nitaongea na wizara ya tamisemi pamoja na wizara ya fedha tuone tunapataje mwongozo wa kulipa fedha zenu pia nitaongea na Mkurugenzi wa halmashauri pamoja na watendaji wake waanze kulipa fedha hizo kidogo kidogo ."alisema Muro.

IMG_20200529_154207_5.jpg
IMG_20200529_152516_6.jpg
IMG_20200602_131226_8.jpg
IMG_20200529_152343_0.jpg
 
Serikali yetu yafaa kulipa madeni madogo madogo kama haya vinginevyo watu watashindwa kuelewa iwaje viongozi waseme serikali ina hela ila mtu anadai fedha miaka 7 asilipwe tena fedha ambazo hadi mkuu wa wilaya anakiri kuzitambua.

Sitaki kuamini halmashauri inakosa milioni 600 kwa miaka 7
 
Duh mbona barua inasema 189M na si 600M au wapo wadai wengi.
Waangaliwe walipwe haki yao.
 
Aisee , mbona hiyo pesa ni ndogo , yaani ndani ya miaka Saba halimashauri inashindwa kukusanya hiyo pesa sizani Kama kuna ukwel , hii inaweza kusbabishwa na mapato yote ya halimashuri kuelekea hazina badala ya kubaki kwenye halimashauri husika
 
Back
Top Bottom