Wawakilishi wakusudia kufanya kweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wawakilishi wakusudia kufanya kweli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Apr 4, 2009.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Isles opts to go it alone in oil
  ISSA YUSSUF in Zanzibar, 4th April 2009 @ 02:24

  Zanzibar yesterday said it wants to be free on matters concerning oil and natural gas exploration and exploitation, arguing that the current Union structure denied the islands an opportunity to benefit fully from its natural resource wealth. “We need to have full authority over territorial waters and inland areas since land is not among the Union matters. We should also have equal partnership over the Exclusive Economic Zone (EEC),” the Zanzibar Minister of Water, Construction, Energy, and Land, Mr Mansour Yussuf Himid, said when presenting government proposal on ‘Oil and natural gas exploration’ in the Zanzibar House of representatives.

  He said in his presentation that took 70 minutes that although the Petroleum (exploration and production) Act of 1980 also applies in Zanzibar, the isles has not been benefiting from “any revenues from the production of natural gas on Tanzania Mainland and ongoing oil exploration.”
  Mr Mansour told the hushed House that the Zanzibar government’s proposals, which include Zanzibar’s independence in natural resources, are based on the "fact that Zanzibar has always been the loser as even the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) structure only appears to serve the mainland’’.

  The minister asked representatives to deliberate and support the proposals to clear the controversy that emerged after reports that there is a possibility of having oil reserves on Zanzibar territory. He argued that it is high time Zanzibar went it lone on matters concerning oil and natural resources, citing "prolonged period of violation of both Zanzibar and Union constitutions that has persisted despite frequent complaints from Zanzibar authorities.” Mr Himid called for the unity of all Zanzibaris in the matter to protect the isles’ interests and the speeding up of oil and natural gas exploration for the development of Zanzibar. He emphasized that no company would be allowed to search for oil in the isles territory without the permission of the Zanzibar government.

  He further argued that it is possible to remain in the Union despite the independent control over natural resources, citing examples of India and the United Arab Emirates (UAE) where each state has full control over its natural resources. “But on the other side, such unfair deals and unequal distribution of natural resources have created problems in some countries such as DRC, Sudan, and Algeria. We pray that our natural resources should not be the source of conflict between the two Union partner states,” Mr Mansour told the House.

  After the presentation, the Speaker, Mr Pandu Ameir Kificho, advised members of the House to discuss the government’s statement carefully and minimise emotion “in the best interests of the Union.” Oil and natural resources are currently among the top items on the agenda in the meetings between senior Zanzibar and Union government officials, with the isles pressing for independence on matters concerning its natural resources
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini wanazunguka kwa kutafuta visababu? kwa nini wasiseme kama serikali kuwa hawaridhiki na aina ya muungano uliopo ili ujadiliwe upya? Kwa nini?
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tafuta:
  Maskani
  Habari za Kitaifa
  Tahariri
  Makala
  Uchambuzi
  Michezo na Burudani
  Safu
  Majarida
  Ulingo wa Siasa
  Urithi wetu
  Jamii
  Sayansi na Teknolojia
  Blog
  Video
  Matangazo


  Jumamosi Aprili 04, 2009
  Habari za Kitaifa

  Z’bar yacharuka na mafuta
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 4th April 2009 @ 10:28 Imesomwa na watu: 56; Jumla ya maoni: 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetupilia mbali taarifa ya mshauri mwelekezi kuhusu mgawanyo wa mafuta na gesi asilia na kutaka suala hilo sasa kuondolewa katika mambo ya Muungano. Inataka masuala ya mafuta na gesi asilia kuondolewa katika Muungano, kwa madai yaliingizwa kinyemela huku Zanzibar ikidai haifaidiki na mgawanyo wa rasilimali za gesi za Tanzania Bara.

  Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid aliyasema hayo jana katika Baraza la Wawakilishi alipowasilisha ripoti ya mshauri mwelekezi kuhusu mgawanyo wa mafuta na gesi asilia. Himid alisema ripoti ya Mshauri Mwelekezi imetaka suala la mafuta na gesi asilia kubaki katika mambo ya muungano, lakini imeshauri kuwapo kwa wizara ambayo itaratibu masuala hayo katika Muungano.

  Aidha, katika ripoti hiyo imetaka kuundwa kwa chombo kipya kitakachoshughulikia na kusimamia pamoja na uchimbaji na utafutaji na utoaji wa leseni ya mambo ya mafuta.
  Himid alisema katika ripoti ya mshauri mwelekezi, imegundua kwamba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), halina sura ya Muungano. Kwa sasa shirika hilo yupo Mjumbe mmoja wa Bodi kutoka Zanzibar, hali inayodaiwa inaonyesha halipo kwa ajili ya maslahi ya Wazanzibari kwa ujumla.

  Aidha, alisema shirika hilo limeundwa kwa mujibu wa amri ya rais mwaka 1969 na kuundwa tena kwa mujibu wa sheria ya mashirika ya umma, lakini hata hivyo halijapata baraka na kupitishwa na chombo kinachotunga sheria cha Baraza la Wawakilishi, hivyo ni batili na haliwezi kufanya kazi zake Zanzibar.

  Huku akishangiliwa kwa makofi na wajumbe wa pande mbili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wapinzani CUF, Himid alisema kitakuwapo chombo chenye mamlaka ya kutoa leseni ya uchimbaji wa mafuta kwa kampuni mbalimbali za nje kitakachofanya kazi Bara na hivyo Zanzibar kukosa mapato. “Katika hili, tumegundua Zanzibar itakosa mapato yake makubwa kwa makampuni ya kuchimba mafuta ambayo yatasajiliwa Tanzania Bara...hili litainyima mapato mengi Zanzibar,” alisema.

  Alisema Zanzibar haikubaliani na baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na mshauri mwelekezi kutokana na kuwapo kwa upungufu mwingi huku Zanzibar na Tanzania Bara ikiwa na sheria zinazotofautiana, ikiwamo ya mambo ya umilikaji wa ardhi. Alisema mapendekezo ya SMZ kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, suala la mafuta kuondolewa katika mambo ya muungano kwani hapo awali halikuwa katika orodha hiyo kwa mujibu wa sheria.

  Alisema hadi sasa Zanzibar haijafaidika na mapato yanayotokana na mauzo ya gesi asilia ambayo tayari inazalishwa Tanzania Bara, ikiwamo katika maeneo ya Songosongo na Mnazi Bay. “Suala la mafuta na gesi ni mambo ya muungano, lakini hadi sasa Zanzibar haijafaidika na mapato yanayotokana na uzalishaji wa gesi na mafuta,” alidai Himid ndani ya Baraza la Wawakilishi.

  Alisema Tanzania Bara zipo maliasili nyingi ambazo hazijaorodheshwa katika mambo ya muungano na Zanzibar haifaidiki nayo ikiwamo almasi, tanzanite, mafuta na gesi. Alisema ushauri wa mtaalamu aliyeletwa kwa ajili ya kufanya mgawanyo wa mafuta na gesi ambaye anataka suala hilo kuwa la muungano, lakini linaweza kusababisha matatizo makubwa na linaweza kuleta mvutano wa hali ya juu.

  “Kama itakuwa suala la mafuta ni bora kubakia katika mambo ya muungano basi suala la marekebisho ya Katiba linahitajika kwa sababu Zanzibar haifaidiki na mafuta na gesi iliyopo Bara,” alisema. Alitahadharisha na kusema suala la mafuta katika nchi zenye muundo wa muungano au shirikisho limeleta matatizo makubwa na ugomvi wa watu kuuana, ikiwamo Nigeria na India.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na SMZ ilitafuta mshauri mwelekezi kwa ajili ya kupata mgawanyo mzuri wa rasilimali za mafuta na gesi itakayozalishwa nchini. Mshauri huyo kutoka Uingereza, Aupec Limited alimaliza kazi yake na ripoti hiyo kuiwasilisha kwa serikali zote mbili.

  Miongoni mwa mambo yaliyomo katika orodha ya muungano wa nishati na mafuta ya gesi inayopatikana katika sehemu yoyote ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini Zanzibar inadai mambo ya mafuta na gesi yaliingizwa kinyemela bila ya kupata ridhaa kwa upande wa Zanzibar.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mwanzoni waliwatuliza wananchi wakawaambia subirini ripoti ya mshauri itaweka mambo yote sawa. mshauri amesema wasivyotaka wanamponda!
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Wawakilishi walishapinga mapema matokeo yoyote ya Mshauri kwani mshauri mwenewe alikubali kuwa alikuwa misled kwa kunyimwa habari muhimu kuhusu mfumo wa Muungano.
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nafikiri taarifa ya Serikali aliyoieleza Mansour kwenye Baraza inajieleza vizuri tu na inajitosheleza. yanayopendekezwa ni sahihi. Na nafikiri Baraza la Wawakilishi litatafakari na kutoa tamko muwafaka ambalo ni lazima liheshimiwe kwa mujibu wa ustaarbu na taratibu zetu za kuendesha mambo. (Yaani isitokee kina Mwakyembe tena wasimame pembeni kubeza tamko hilo).
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kama nyie Tanganyika mngekubali upumbavu huu! Mtu achimbe zahabu,almasi,tanzanite zake peke yake. Lakini leo mafuta yetu sote. Wazenj si wapumbavu kiasi hicho
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Apr 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tuwaachie tu mafuta yao jamani. Mbona haya ni kama ya Alinacha!?
   
 9. I

  Ipole JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao wazenj wana matatizo kila kitu wanapata toka bara hakuna wanachojitegemea
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ndio ,nasema ndio kwa sababu Zanzibar inataka kuonyesha njia ,njia ambayo itawafungua macho WaTanganyika na kuona ni jinsi gani rasilimali zinaweza kutumika na kuiendeleza nchi na sio watu wachache ,Dunia nzima Tanzania ni nchi ya mwanzo kwa utajiri na uzuri ,kijiografia,maliasili na namna ilivyo ukizingatia wanyama wengi wanapatikana Tanzania kuliko nchi nyengine yeyote ile ,sema wanatoweka kwa kasi kuliko nchi nyingine.

  Tanzanzia kama ingekuwa na utawala mzuri wenye kujali hazina za nchi basi utalii peke yake ungeliweza kuitajirisha nchi hii kwa kiasi kikubwa sana.Madini hapo haina haja hata ya kusema wazungu wanaondoka na viroba huku mtaalamu mzalendo anaendesha kijivespa na shati linapeperuka utazani anaenda kuuza madafu.

  Zanzibar wakifanikiwa kuyachimba mafuta basi itakuwa ni changamoto kwa utwala wowote ule utakaokuwepo Tanzania na hili linaweza kuifanya Tanzania kimikoa kujijenga ikiwa kila mkoa utakuwa unashughulikia mali asili yake na percrntage fulani inabaki kwenye mkoa na percentage nyengine inaingia katika hazina ya Taifa ili kushughulikia ile mikoa ambayo haina uzalishaji wa aina yeyote ,mikoa hii inaweza kugeuzwa kuwa ya viwanda na uekezaji huru.

  CCM wamelivuruga Taifa hili na kulifanya lishike mkia kwa umasikini ,wafuasi wa CCM walioko juu au kwa maarufu hujulikana kama vigogo kila mmoja ana mradi wake ,miradi ambayo leo hii inaibuka na kujulikana na walala hoi ,nani akijua kama akina Mwakiembe wanamiliki ,akina Rostamu na wengine tele,kila mmoja amejijenga kikweli kweli huku wananchi wakiumia ,WaZanzibari wameliona hilo na kuona watakufa masikini kwa kuelemewa na Muungano kwa ufupi wamechoka kuulinda Muungano maana wanaototonoka ni vigogo wa CCM bara .Let the winds prevail and Zanzibar decide its own path.
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kwa nini Wawakilishi wasichachamae hivyo Visiwani kulipia deni umeme na kukubali bei ya soko badala ya kuendelea kubebwa na bara?
   
 12. D

  Darwin JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama ni ya alinacha kwanini wabara wayashikilie bango?
  Wewe bado hujaona kasoro hapo?

  Siku nyingine unaongea points lakini siku nyingine najiuliza je ni yuleyule anayeitwa Mzee Mwanakijiji?

  Au siku nyingine unapopost umelewa na siku nyingine uko mzima?

  Zanzibar ikijitenga itajiweza yenyewe bila kutegemea umeme wa bara, alimasi au dhahabu kutoka bara na wabara wanalijua hilo ndio maana wanakazania kuing'ang'ania.

  Wabara ndio wanaogopeshwa kirahisi, mwisho wake nikuambiwa hoja za uongo lakini wazanzibari hawadanganywi kirahisi kama Wadanganyika.
   
 13. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Jawabu ni Komoro kujiunga na Mainland!
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hata kama Kinibu!!!!
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Ndoto za alinacha indeed! Kwani mafuuta yamegunduliwa Zanzibar? Jamani kila sehemu in potentilaity ya kugundundua mafuta lakini huweza kuiita hiyo potential ndio mafuta...mmh mambo ya kizenji hayo! Wameshaona ndio deal..si unajua akina yahe wanajua mafuta ndio mkombozi kula, kupiga bao na kupata urojo!...mmh yetu macho.
   
 16. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Yaani mimi katk umri wangu hakuna siku nimesoma postive aspects za Muungano toka Visiwani!

  Ni malalamiko ya kuonewa tu kila siku!!!
   
 17. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waacheni wazanzibari wajitenge jamani, hawaoni faida ya muungano,sanasana wanabanwa tu na mambo ya 'muungano'. Hayo mafuta yamewalewesha na hawaoni sababu ya kuendelea na Muungano.
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Apr 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa wazenj waachieni hayo mafuta yao; lakini itabidi walipe madeni yote ya umeme na pia itabidi wajilipie mambo ya ulinzi; tuone kama watagangamara!! Hawa jamaa wanajifanya wako pamoja kwenye mambo haya ya mafuta lakini hawajui kuwa hayo mafuta wanayopigia alinacha yanaweza kuwa ndio laana yao wakachinjana kama kuku!!
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Tujikite na kutafuta mafuta yetu na gesi yetu ............
   
 20. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #20
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Duh! Umeme imekuwa nongwa? tunalipa umeme kwa bei mnayotaka basi chukueni wenewe hasa kwa vile haukutosheni nyinyi wenyewe.
   
Loading...