Wavaa vimini na milegezo wavuliwa nguo hadharani jijini Mbeya

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wasichana wanaovaa nguo fupi za kubana na wavulana wanaovaa milegezo jijini Mbeya , juzi walipata wakati mgumu baada kundi la vijana kuwavua nguo zao na kuzichana hadharani, kutokana na gari la matangazo kupita jijini hapa likiwataka watu kuvaa nguo za heshima zinazoendana na maeneo husika.

Tangu Machi 7 hadi 9, gari la matangazo ya Kampuni ya Studio H ya Huruma lilipita mitaa mbalimbali ya jijini Mbeya, likiwataka wasichana kuacha kuvaa vimini na vijana kuacha kuvaa mlegezo.

Baada ya tangazo hilo, vijana walianza kuwavamia wasichana na wavulana waliovaa milegezo maeneo ya Uyole, Soweto, Kabwe na Mwanjelwa, huku wanawake waliokuwa wakiuza matunda wakiwarushia vitenge wasichana waliochaniwa nguo ili wajisitiri.

Ofisa Habari Jiji la Mbeya, John Kilua alisema uongozi hauhusiki na tangazo hilo.

Hata hivyo, Ofisa wa Kampuni ya Studio H ya Huruma, Siyata Mbua alisema walitoa tangazo hilo baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya jiji na kampuni yake.

Mbua alisema kazi ya kuzuia nguo zisizo za heshma inahusu Serikali, lakini kampuni iliamua kujitolea kwa makubaliano na jiji kwa mwaka mmoja.

“Lengo ni kuwahamasisha wananchi wavae nguzo za heshima. Hatuwahamasishi vijana wawavamie watu, bali tunawataka kila mmoja avae nguo kulingana na maeneo anayofanyia kazi,”alisema. Mabua alisema lengo ni kuelimishana zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema hajapata malalamiko na kuwataka vijana kuheshimu utu wao kwa kuvaa nguo za heshima.
 
Mmmmh hiyo kali. Ila kuhusu uvaaji nadhani ni kuingilia utu wa mtu. Mbona hawahamasishi wanaozalisha sigara na kuchoma viwanda. Maana sigara ina madhara makubwa kuliko sketi fupi na mlegezo
 
Mimi huwa napenda kuwaona mabinti wakiwa uchi, siku nyingine wakianza kuwavua nguo naomba uniite nije kuona
 
Natamani kuhamia Mbeya japo kwa muda,ili nishiriki hili zoezi directly yaani kwa mkono wangu mwenyeweee!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hii kitu ipo Meru kijana ukikutwa umevaa mlegezo fimbo sabini zinakuhusu.Haaa haaa wameru ni balaa.
Na si vijana tu na hata wanawake wanovaa vimini ama suruali zilizowabana nao wanakula viboko 70 tena hadharani..
 
Hii kitu ipo Meru kijana ukikutwa umevaa mlegezo fimbo sabini zinakuhusu.Haaa haaa wameru ni balaa.

Hivi wanafahamu haki za binadamu wameru hawa?Kimsingi hawajavunja sheria kwanini wanaadhibiwa?
 
Watu wote waliohusika katika uvunjaji wa sheria wakamatwe na waadhibiwe ipasavyo. Huu ni uvunjaji wa haki za binadamu (freedom of expression). Wanasheria mnasemaje?
 
Back
Top Bottom