takribani mwaka mmoja toka leo bei ya mafuta kwa pipa moja katika soko la kimataifa lilikuwa zaidi ya $120. leo hii bei ya pipa moja la mafuta ni chini ya $36. mara ya mwisho bei ilikuwa chini hivi miaka 11 iliyopita. ndani ya mwaka mmoja bei ya mafuta imeshuka kwa asilimia 75. kipindi bei ya mafuta kwa pipa ikiwa zaidi ya $120 tanzania bei ya petroli ilikuwa zaidi ya tshs 2200. mwaka mmoja baadae bei mpya za ewura bado zinatupa mashaka ni taasisi hiyo. wasomi wa hii nchi wako wapi. EWURA ni jipu. tujiulize swali moja bei ingependa kwa asilimia 75 badala ya kushuka ingekuwa hivi hivi?