Bei ya Petroli, Dizeli Oktoba sasa kitonga, sababu za kushuka zatajwa

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,554
4,175
Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Oktoba 2024 imeshuka nchini, ikilinganishwa na Septemba, huku sababu kadhaa zikitajwa, ikiwamo kushuka kwa gharama za soko la Uarabuni.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha bei za mafuta kuanzia leo Jumatano Oktoba 2, 2024 kwa yanayochukuliwa Bandari ya Dar es Salaam, Petroli imeshuka kutoka Sh 3,140 Septemba kwa lita moja hadi Sh 3,011 Oktoba, sawa na asilimia 4.1.
1727852508999.png
Pia, kwa petroli inayochukuliwa katika Bandari ya Tanga, lita moja imeshuka kutoka Sh3,141 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba na kwa Bandari ya Mtwara pia imeshuka kutoka Sh3,142 Septemba hadi Sh3,016 Oktoba.

Kwa upande wa bei ya dizeli, taarifa ya Ewura inaeleza bidhaa hiyo inayopokewa Bandari ya Dar es Salaam bei yake imeshuka kutoka Sh3,011 Septemba hadi Sh2,846 Oktoba.
Screenshot 2024-10-02 101339.png

Soma: Petroli na dizeli zashuka bei soko la dunia
 
Nilidhani imeshuka tangu Jana tarehe 1 Oktoba, nilitaka kukataa maana nimenunua Jana tu shilingi 3,140/Lita

Ni muda Serikali ikatumia akiba yake ya Fedha za kigeni kuagiza mafuta mengi zaidi wakati huu kabla athari za vita vya Israel na mataifa ya Kiarabu hazijaanza kujitokeza zaidi
 
Hatuna matenk kaka ya kuhifadhi, si hata kipinde kile cha corona, tungeweza agiza mafuta mengi sana, issue ikawa hakuna pa kuyahifadhi
 
Nilidhani imeshuka tangu Jana tarehe 1 Oktoba, nilitaka kukataa maana nimenunua Jana tu shilingi 3,140/Lita

Ni muda Serikali ikatumia akiba yake ya Fedha za kigeni kuagiza mafuta mengi zaidi wakati huu kabla athari za vita vya Israel na mataifa ya Kiarabu hazijaanza kujitokeza zaidi
Nchi yako ni kama familia masikini tu, unanunua kinachotosha kula leo tu coz uwezo wa kununua akiba ya mwezi huna.
 
Nchi yako ni kama familia masikini tu, unanunua kinachotosha kula leo tu coz uwezo wa kununua akiba ya mwezi huna.
Nchi inatupa pesa nyingi kusomesha watu, mifumo haitumii maarifa ya waliosoma, waliosoma ni mbumbumbu isipokuwa kwenye ulaji tu.

Misri ina hifadhi ya maji kwa miaka 30 ijayo; sisi hata tani 500 tu za dhahabu hatuna na ilhali inatoka hapa!
 
Namhurumia yule jamaa,juzi kaniambia mafuta yameisha kituoni kwake,nikaenda kingine,jana pia kaniambia tena kwa nyodo mafuta yameisha,sasa leo ndio akili itamkaa vizuri alijua bei itapanda...
 
Back
Top Bottom