nyamalagala
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 744
- 675
Amani iwe kwenu ndugu zangu wanaJF. Natumai mnaendelea vema na harakati za kuisaka riziki ya kila siku ili kutootesha nyasi kwenye njia iendayo msalani.
Kama kichwa cha andiko langu kisomekavyo, mimi ni kijana wa kiume miaka yangu 27 mwalimu wa shahada ya awali hasa katika masomo ya KISWAHILI na HISTORIA nimehitimu mwaka huu 2018. Napatikana kijiji cha Magole- Kilosa Morogoro. Najitokeza kwenu kuomba kushikwa mkono kwa yeyote atakayeguswa na ombi langu. Naamini kuwa jukwaa hili lina watu wa kada mbalimbali na viwango mbalimbali. Katika hili sijajuta kuwa mwanachama hakika. Katika msingi huo naamini humu kuna wamiliki wa shule, walimu wafanyao kazi katika shule za binafsi na wengine wana uhusiano ama mawasiliano ya namna moja ama nyingine kati yao na wamiliki wa shule hizi.
Tafadhali ndugu zangu naomba mnisaidie kuniunganisha ili nipate japo riziki ya kila siku. Niko tayari kufanya kazi popote pale kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ya upili kwa moyo wangu wote hata kwa dau dogo. Ninachoangalia ni mazingira ya kazi yaniruhusu mimi kuonesha ujuzi wangu wote kwa uhuru kwani naamini katika kile nilichojaaliwa na Mola. Katika hili, atakayenipokea hatajutia uwepo wangu kwenye taasisi yake.
Si lengo langu kuwachosha sana, napatikana kwa 0769796425 au barua pepe sadockgerald3@gmail.com.
ASANTENI SANA WAUNGWANA.