Waunguja wawabagua Wapemba

Hamna lolote!!

Kazi ya TISS hii!!!
Chezea wabara wewe!....Hivi mlipokuwa mnapanga mipango hii ya kuvunja muungano kupitia dini UAMUSHO
mlikua mnafikiria nini? Sasa hapa ni full propaganda alafu tuone kama mtakaa kwa amani kwenye hako kanchi
 
MODS mpo wapi?

Huu ni uzushi wa hali ya juu kuwahi kupostiwa hapa kwenye jukwaa

1
Aaanh! leo yamekua hayo? wewe si ndiyo ulikuwa kinara mkubwa hapa jamvini kwa kushadidia uonevu ule?
Sasa nyinyi mmejua upande huu na sisi tumejua upande wa pili! Hapa ni full propaganda...chezea wabara weyee
 
Kazi kwelikweli.Yaani tutasia mengi sana...kwenye hili sakata.
 
ni propaganda tu hizi. mwandishi ni mmoja tu alijifungia chumbani kwake na mkewe akadraft. ingelikuwa rasmi, kungelikuwa na saini za watu wengi kudhihirisha kuwa ni waunguja wamesema. kinachoonekana hapa ni kuwa, watetezi wa muungano wamejaribu kudesign hiki kipeperushi ili kuonesha kuwa baada ya kuukataa muungano, kitakachofuata ni kukataana wenyewe kwa wenyewe (unguja na pemba) - kama alivyosema nyerere. acha tuwe na tanganyika yetu.
 
Hicho kipeperushi mbona kama kimeandikwa na mtu ambaye shule ilikua kituo cha polisi, halafu imejaa gadhabu mno!
 
...Dhambi ya UBAGUZI, Dhambi ya UBAGUZI, WaTanzania wenzngu Dhambi ya UBAGUZI .....!!!

Kama si kesho, keshokutwa WaTanzania tutaanza kusikia 'Mataifa' ya ajabu ajabu ndani ya mipaka yetu kama vile:

1. Jamhuri ya Watu wa Pemba Kaskazini;
2. Muungano wa Ukoo wa Shirazi Chake Chake Kusini;

... nasema DHAMBI YA UBAGUZI wa aina yoyote ile ... WaTanzania, DHAMBI YA UBAGUZI!!!

Vipeperushi hivi vimesambazwa kwa kasi jana katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar vikiwa na ujumbe unaowataka Wapemba waondoke Unguja na kurudi kwao Pemba wakajipange huko kuukataa Muungano. Sehemu ya waraka huo - angalia kiambatanisho....
 
Leo utataja majina yote ya wana UAMUSHO lakini sisi hatujali na mtajua wenyewe....hili mmeshalikoroga na lazima
mlinywe! Wabara kama wamarekani'huwa hatukurupuki kama nyinyi...Sasa tumewatupieni scud hilo kwanza...mkilitegua
hilo tunawatupieni na jingine, sasa tuone kama kutakalika kwenye hako kanchi. Chezea wabara wewe
 
Viongozi wetu wa Dini za Kikristo,

Kaeni mbali kabisa tena kimya kama maji mtungini KUTOKUJIBU UCHOKOZI WA DHAHIRI kule kwa ndugu zetu Tanzania Visiwani.

Kama serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezi kulinda Wakristo na Ukristo wetu Visiwani basi wanatukosea kikatiba maana walikula kiapo juu ya hili.

Namwonea huruma sana Dr. Shein, huu mziki ni mzito sana kwake!
 
Vipeperushi hivi vimesambazwa kwa kasi jana katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar vikiwa na ujumbe unaowataka Wapemba waondoke Unguja na kurudi kwao Pemba wakajipange huko kuukataa Muungano. Sehemu ya waraka huo - angalia kiambatanisho....
Wapemba watarudije kwao Pemba,Wakati raisi wa ZNZ Shein ni Mpemba,makamu wake Maalimu Seif vile vile ni Mpemba,na hao Woote mliwachagua kwa kula nyingi, sasa mbona mnanichanganya jamani!!!!Ninawasiwasi na hicho kipeperushi
 
kuitafuta haki kuna gharama zake ndugu zangu, yatasemwa mengi sana ya uzushi ili kudhoofisha nguvu. waswahili husema ''UKITAKA KUONEKANA MBAYA DAI CHAKO''
 

sasa ccm inahusika vipi kwenye hii issue ya muungano? Zanzibar kuna vyama viwili vikubwa vya siasa ambavyo ni ccm na cuf. Kwa maana hii ina maana cuf ndiyo wanapinga muungano? Na kama ni hivyo basi cuf ndiyo iko nyumba ya mashehe.

Kimsingi tu watu wa tanzania visiwani wanatakiwa kukumbuka tu bila ya muungano hakuna sisi ni wazanzibar na wao ni wabara. Nyerere alishasema siku nyingi na huko ndiko zanzibar inakoelekea sasa.

 
Hizo ni propaganda.
Huo waraka umeandaliwa na wanaunguja wangapi?
Wana mamlaka gani ya kuwasemea wenzao?
 
Mkuu ishu ni Muungano na sio dini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…