Waumini wa Mchungaji Gwajima waanza kumchoka. Wengi waonesha mashaka yao juu ya kuumwa kwake

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375

Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wamesali Jumapili ya tatu bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima,lakini wameshtushwa na taarifa kuwa kiongozi huyo wa kiroho ni mgonjwa na anapata matibabu nje ya nchi.

Waumini hao walisema wamekuwa wakisikia kuwa askofu wao anatafutwa na Jeshi la Polisi na juzi wamesikia kuwa anapata matibabu nje ya nchi wakati wao hawajatangaziwa rasmi kuhusu taarifa hizo.

Juzi, Wakili wa Askofu Gwajima, Peter Kibatala aliileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mteja wake hakufika mahakamani kwa kuwa yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Askofu Gwajima alitakiwa kufika mahakamani hapo anakokabiliwa na kesi ya kumtolea lugha chafu Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha.

Mbali na taarifa za kuumwa, pia Gwajima anatafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika katika utawala wake.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa atalizungumzia suala hilo leo Jumatatu.

Katika ibada ya jana, kama kawaida, Mchungaji Adriano Edward hakuwaeleza chochote waumini wa kanisa hilo kuhusu alipo Askofu Gwajima wala hali ya afya yake.

Mchungaji Adriano alipotakiwa kuzungumzia suala la afya ya Gwajima, alisema kupitia msaidizi wake kuwa hawezi kuzungumza chochote na vyombo vya habari.

Chanzo: Mpekuzi
 
pole yao...ila hiyo voice note kama ni kweli je?kama ni kweli kuna anayojua kuhusu jk si wamwambie ayaanike hlf tujue lipi la ukweli na lipi uongo then wamshtak kwa uongo kuliko kumtisha na kutumia nguvu ya polisi na mpaka kuwalipa interpol wamsake kulinda uovu wao??
napata picha halisi..ccm wako tayari kuingia gharama yoyote kwa pesa za serikali kulinda maslahi yao kuliko ya waliowaingiza madarakani(wananchi)...
 
Gwajima kachanganyikiwa
 
Waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wamesali Jumapili ya tatu bila kuwapo kwa Askofu wao, Josephat Gwajima,lakini wameshtushwa na taarifa kuwa kiongozi huyo wa kiroho ni mgonjwa na anapata matibabu nje ya nchi.

Waumini hao walisema wamekuwa wakisikia kuwa askofu wao anatafutwa na Jeshi la Polisi na juzi wamesikia kuwa anapata matibabu nje ya nchi wakati wao hawajatangaziwa rasmi kuhusu taarifa hizo.

Juzi, Wakili wa Askofu Gwajima, Peter Kibatala aliileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mteja wake hakufika mahakamani kwa kuwa yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Askofu Gwajima alitakiwa kufika mahakamani hapo anakokabiliwa na kesi ya kumtolea lugha chafu Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi, Cyprian Mkeha.

Mbali na taarifa za kuumwa, pia Gwajima anatafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika katika utawala wake.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa atalizungumzia suala hilo leo Jumatatu.

Katika ibada ya jana, kama kawaida, Mchungaji Adriano Edward hakuwaeleza chochote waumini wa kanisa hilo kuhusu alipo Askofu Gwajima wala hali ya afya yake.

Mchungaji Adriano alipotakiwa kuzungumzia suala la afya ya Gwajima, alisema kupitia msaidizi wake kuwa hawezi kuzungumza chochote na vyombo vya habari.

Chanzo: Mpekuzi

Kwa jinsi " anavyotiririka " na Waumini wake hasa wale " waliotubeba miezi kenda " sijui kama hapigi Gitaa la " Dally Kimoko ".
 
Gwajima anatakiwa awe makini hii serikali ya KAZI TU siyo yakuchezea hata kidogo
 
Back
Top Bottom