Waume kazi tunayo

Waume kazi tunayo

Mi nafikiri ni hisia zako tu zinakudanganya, usikute hata hawazii hayo unayoyafikiri!

Inawezekana! Honey Faith, mtoto wa kike (mke wa mtu) akimfanyia hivi m' me huwa ana maana gani?
  1. Kaniomba nitafute hotel ya mbali, nje ya mji, ana mazungumzo na mimi (nilipokuwa mbishi, akasema atagharamia yeye kila kitu)!
  2. Ananipa ratiba zake na za mme wake (zinazohusu kutokuwepo nyumbani kwa mtu wake)
  3. Kabla sijakata mawasiliano nae, sijawahi kumuona kavaa nguo ndefu, wala kufichwa matiti yake!
  4. M - pesa yangu ilirushiwa elfu 80, siku 1 kabla ya 8 8 (long w.end), kutoka kwake, nikauliza ya nini? Nikajibiwa wee kaa nayo ntakuambia baadae! Jioni akaniuliza kuhusu ule mtoka aliotaka! Nikairudisha ile pesa, alinuna kama 3 days!

ana vituko vingi sana, hivo ni vichache! Nisaidie ana maana gani mpaka hapo?
 
Last edited by a moderator:

Na maadili haya wangekuwa nayo viongozi wetu, tusingepata madhara ya ten percent katika mikataba. Nakuomba usiishie kwenye mapenzi tu, uadilifu wako huu uwe pia katika shughuli zako za ujenzi wa taifa!
 
Nimekusoma rpg
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa kubaki njia kuu nadhani kama wanaume wote wangekuwa na ujasiri kama wewe michepuko ingekoma
 
CHONA wa CHILONWA!

Tuliooa tuna kazi kubwa!

Ni hivi, kuna mdada mrembo na ana shule yake ya kutosha kichwani, mke wa mtu, ana kazi yake, kuna magumu anayapitia, nikawa ni miongoni mwa washauri wake (kwa yeye mwenyewe kuja kunitaka ushauri!)

Kutokana na yale magumu anayopitia na zile shauri zangu, kukatokea mawasiliano ya mimi na yeye ya mara kwa mara tofauti na mwanzoni, tukajenga mahusiano ya kawaida sana, mchanganyiko wa aina ya kaka-dada ama urafiki, ambao haukunitisha hata!

Sijui ikawaje, yale mazoea yamekuwa tabu! Sasa bidada analazimisha mahusiano ya kingono na mimi. Wala hakuwa na ugumu wa kuficha, alionyesha hisia na baadae akatamka kabisa. Nimeshindwa kuamini kinachontokea! Kiukweli sina interests nae, na kadri ninavozidisha kumkwepa ndio anazidi kuja! Simfahamu mumewe wala hamfahamu mke wangu! Nakiri kosa la kukubali kumsaidia ktk yale magumu yake, leo nayaona majaribu dunia - mke wa mtu! Hatua nilizochukuwa:
  1. Nimeshamtakia kuwa hatuwezi kuwa wapenzi! Nina ndoa yangu!
  2. Nimekata aina zote za mawasiliano (simpigii, sichat nae)!
  3. Sikubali offer yake yoyote ile!
  4. Nimemueleza hatari za jambo analolitaka, (ndio kwanza kasema sisi ni watu wazima)

Kwa wale tuliooa, nawasihi tuwe karibu na wake zetu, wawe ni zaidi ya marafiki zetu, zaidi ya ndugu, sina ushahidi lkn nahisi huyu bidada ana vitu vidogo vidogo mno, anavikosa kutoka kwa mwenza wake. Bado hakuna dalili ya kumuweka MBALI na mimi! Na ktk vitu nilivomsaidia hakuna hata kimoja interms of cash, ilikuwa ni ushauri tu!
Nipo ktk majuto huku nikitafuta dawa ya kujinasua!
una roho ngumu bro unaweza ukalala na chatu kitanda kimoja wewe mmmmmmmh
 
Back
Top Bottom