Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,430
Wauguzi wawili wa Hospitali ya wilaya ya Manyoni mkoni Singida wamesimamishwa kazi,baada ya kumwachia mtoto wa miezi minne kamba kwa muda wa zaidi ya masaa nane ,ambayo waliifunga mkononi kwaajili ya kumwekea dripu ya maji na kusababisha mkono kuoza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Bwana Charles Fussi ametoa uamuzi huo baada ya kujirizisha kwa kukaa vikao na uongozi wa hospitali na wao wauguzi Bi.Salima Mkoka na Bi.Specioza Mchunguzi kukiri kusahau kutoa kamba hiyo na kusababisha mkono wa mtoto Cecilia Dastani kuharibika na unaweza kukatwa.
Wakieleza daktari ambapo tukio lilipotokea katika hospitali ya wilaya ya Manyoni Daktari Nelson Bukuu Mganga mkuu wa wilaya amekiri kuwa wauguzi wake wamesahau kwa bahati mbaya hadi siku ya pili,huku Mganga mkuu wa Hopitali ya St Gasper Itigi alipolazwa baada ya kupewa rufaa daktari Anatori Lukonge amesema mtoto Cecilia anaweza kupoteza baadhi ya vidole au kukatwa mkono.
Kwa upande wake mama mtoto Bi Violet Ernest mkazi wa Sasilo wilayani Manyoni amesema hakujua kwanini mtoto wake alikuwa akilia sana tokea awekewe dripu saa saba mchana mpaka siku ya pili asubuhi alipoambiwa daktari na kuja kutambua tatizo hilo .
Chanzo; IPP media