Wauguzi wawili Manyoni wasimamishwa kazi kwa kusababisha mkono wa mtoto wa miezi minne kuoza

Pamoja na uzembe wa wauguzi sikatai lakini huyo mama wa mtoto kama mtoto muda wote analia kweli huwezi kumuangalia mwanao maungoni kwanini analia tu!!?

Hakuweza hata kutoa taarifa kwa waauguzi kuwa mtoto toka awekewe drip analia tu muda wote!!?
 
wangekuwa ni walimu hapo nadhani thread hii had sasa ingekuwa na comment 700,000 na kati ya hizo 699,999 yangekuwa ni matusi na kejeli za kutosha kwa walimu

Lakin kwa vile ni wauguzi naona watu wana toa comment za upole wakati uzembe huo umepelekea mtoto kupata ulemavu wa kudumu. coz wanaona hata wao wataugua na kuwarudia hao hao tena,laki.n mwalimu alisha kuvusha lasaba hata ukimtukana una hakika hukutani naye tena so hata ukimtusi poa tu.
samahan sijatoka nje ya mada!
POLE MTOTO MUNGU TENDA MUUJIZA WAKO MKONO HUO USIKATWE
 
Upo sahihi sana. Mama wa huyo mtoto naye hajitambui. Kwani mwenye uchungu sana na mtoto ni Nurses au Mama?
Ni vizuri unapomuuguza mgonjwa uwe karibu naye. Doctors na Nurse wana wajibu wao wanapotua huduma kwa mgonjwa lakini pia hata anayemwangali mgonjwa naye anasehemu yake. Mama hakuweza kuona kuwa mkono wa mtoto umevimba na anauhangaisha? Sitetei uzembe wa Nurses lakini hata Mama anabeba sehemu ya huo uzembe.
 
Singida kuna tatizo gani siku hizi? huko si ambako yule mwanamke alichoma moto nyumba, dah aisee poleni sana
 
Wauguzi kama hawa, unashika, peleka buchani, unamlipa mchinjaji 500 wanalazwa kwenye kile kigogo cha nyama mikono inakatiwa mabegani, (shoka, au kitu chochote chenye ncha kali), wanafungwa tambara wanawahishwa hospitali kwa matibabu
Nina imani hakuna anayependa kufanya hayo makosa lakini hutokea as a human errors.

Na comment kama zako huwa zina backfire mlemle kwa DNA za asili yako kama si wewe basi kwa blood related relative.
 
Nakumbuka Kuna mwaka Temeke hospital Kuna mtoto alipokelewa kutoka kituo kidogo cha Afya akiwa hoi alipofika Temeke akapewa huduma

Lakini kumbe huko alikotoka wasisahau kamba mkononi na Temeke hawakuiona, mtoto usiku akazidiwa akapelekwa Muhimbili.

Na huko Muhimbili wakagundua mtoto ana kamba mkononi na mkono umepata gangrene au kufa then Muhimbili wakaukata mkono wa mtoto na wale wauguzi na daktari wakasimamishwa kazi.

Katika kazi Kuna human mistake inatakoea Katika Fani yoyote ile iwe ya uhasibu,sheria, elimu,madini n.kk

Lakini kwa Huduma za binadamu makosa yake kiungo kinakatwa au roho inaacha mwili

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. Human errors zinatokea sana tu.
Human error inapotokea kwenye vitu visivyokuwa na uhai e.g. uhasibu etc. inaweza isikuumize sana kama error inayojitokeza kwenye mwili wa mwanadamu. Errors zitokanazo na kujisahau zinatokea sana.

Ni sawa hawa watumishi kuwajibishwa na liwe fundisho, ila human errors hazitaisha kabisa, never.

Kufanya "multiple documented checks" inasaidia kupunguza errors.
 
Na wabunge wote walioitikia ndio kwenye mikataba wangesimamishwa kwa wakati haya makosa yasingekua yanatokea
 
Human errors kwenye mwili wa binaadam, angekuwa mwanao anayekatwa mkono kwa 'human error' comment ingekuwa ya tofauti kidogo...tuzidi kumwomba Mungu wanaokwenda kwenye hiki kitengo cha kushughulika na miili ya binaadam iwe ni kwa wito wa kweli...
Nimeshapoteza mtoto na alifariki kwa kwasababu ta human errors sembusa huyo kukatwa mkono au vidole kwahiyo najua uchungu wake usifikiri naandika kwa kujifurahisha tu.

Sijapenda tu comment yako ya kusema hao wauguzi wapelekwe kwa muuza nyama na wao wakatwe mikono tena kuanzia kwenye mabega kwa kutumia mashoka ya buchani...sijapenda.

Hizi ni taaluma za watu ni lazima tuziheshimi na makosa hapo ila hayakubaliki ndiyo maana likitokea kosa wanataratibu zao za kulishughulikia kwa mujibu wa taaluma zao.

Wapo watu wamefungwa gerezani na hakustahili kufunga na wapo wengine wamenyongwa kama hukumu yao mahakamani na hawakustahili kunyongwa as a human errors Katika kazi zao.

Fuatilia ushahidi wa taarifa mbalimbali duniani utayajua mengi zaidi.
 
wangekuwa ni walimu hapo nadhani thread hii had sasa ingekuwa na comment 700,000 na kati ya hizo 699,999 yangekuwa ni matusi na kejeli za kutosha kwa walimu

Lakin kwa vile ni wauguzi naona watu wana toa comment za upole wakati uzembe huo umepelekea mtoto kupata ulemavu wa kudumu. coz wanaona hata wao wataugua na kuwarudia hao hao tena,laki.n mwalimu alisha kuvusha lasaba hata ukimtukana una hakika hukutani naye tena so hata ukimtusi poa tu.
samahan sijatoka nje ya mada!
POLE MTOTO MUNGU TENDA MUUJIZA WAKO MKONO HUO USIKATWE
Umeongea point nkuu,
 
Back
Top Bottom