wauguzi wanyanyapa waathitika wa UKIMWI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wauguzi wanyanyapa waathitika wa UKIMWI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaFalsafa1, May 31, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  `Kuna wauguzi wananyanyapaa waathirika wa Virusi vya ukimwi`
  Mwandishi Wetu
  Baadhi ya vituo vya afya nchini, vimelalamikiwa kwa unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kutokana na taarifa kuwa huwakwepa watu hao pindi wanapofika kwa ajili ya kutaka huduma.
  Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya watu wanaoishi na virusi kutoka kwenye chama cha Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi mkoani hapa (WAVUMO).
  Wametoa malalamiko yao hivi karibuni katika semina ya siku tatu iliyoandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya HPI kwa kushirikiana na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT).
  Aidha, Bi. Fatuma Jafari, ambaye ni mmoja wa wanachama wa WAVUMO, amesema kuwa mara nyingi amekuwa akienda kwenye vituo vya afya ambapo anapoonyesha tu kadi yake, wahudumu humsononesha kwa kumkwepa.
  Amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikimvunja moyo kiasi cha kumfanya ashindwe kuhudhuria vyema kliniki, akihofia unyanyapaa wa aina hiyo anaoukumbana nao mara kwa mara.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama hicho cha WAVUMO, Bi. Keleni Mpesa, amesema kuwa ugumu anaoupata zaidi ni ule wa kunyanyapaliwa na jamii inayomzunguka, ambapo baadhi ya watu humpachika majina ya ajabu.
  Amesema kuwa hali ya uchumi pia kuwa ngumu na kuwafanya kushindwa kumudu matibabu pale wanapopata magonjwa nyemelezi.
  Naye Dk. Aisa Muya kutoka taasisi ya Elizabeth Glezer, inayojishughulisha na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi amekanusha kuwepo kwa vituo vya afya vinavyowabagua wenye VVU na badala yake akasema kuwa unyanyanyapaa na ubaguzi upo pia wao kwa wao.
  "Nashangaa kusikia kuwa kuna wahudumu ambao wanawanyanyapaa wenye VVU kwa kuwa wahudumu wa vituo vya afya kwa sasa wana elimu ya kutosha juu ya tatizo hilo, ila ninachofafahamu ni kuwa unyanyapaa upo pia kati ya sisi kwa sisi," amesema.
  Hata hivyo, akasema ni vyema tabia hiyo ikaachwa.

  ALASIRI
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kazi Kweli kweli;

  Ukimwi bado ni ngoma nzito. It will take so much time watu kuacha Kunyanyapaa wagonjwa hawa. Si elimu tu inayotakiwa, bali pia Utashi wa kweli na upendo kama walivyoapa katika taaluma yao.
   
Loading...