Watz na BUNGE!

Watz na BUNGE!

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
11,004
Reaction score
19,131
Hivi ni kwa nini sisi Watz tunafwatilia sana mambo ya Bungeni? Nimebahatika kutembelea Nchi nyingi Duniani lkn sijawahi kuona Nchi ambayo watu wake wanafwatilia sana kinachoendelea Bungeni kama sisi, hata ukienda Uganda au Kenya au hata Afrika kusini wakati wa Bunge wala watu hawajui kama kuna Bunge lkn sisi kwetu hata mtoto mdogo anajua, hivi ni kwa nini?

Ni Tanzania yetu tu ndio unaweza ukawa unaongea na mtu akakwambia hana Muda kwa kuwa anaangalia Bunge, sijawahi kuona sehemu nyingine yoyote ile yaani wakati wa Bunge ndio inakuwa sasa watu wamepata cha kuongelea, Je ni kukosa kuwa Wabunifu wa jinsi ya kutumia muda wetu vizuri?

Sababu hasa ni nini? Ni je Watu kukosa kazi? yaani watu hawako busy hivyo kutwa nzima wameshinda kwenye TV au Redio wanaangalia au kusikiliza Mbunge fulani kasema nini?

Kwa Mfano swala la kuonyeshwa Bungeni moja kwa moja kwenye TV ni Tanzania tu ambapo ni ishu kubwa, kwanza Nchi nyingi wala hakuna huo utaratibu na wala huwezi kusikia watu wakilalamika, hivi ni kwa nini hasa!
 
Back
Top Bottom