Waturuki wanataka Katiba kama yetu, wanataka strongman!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Wananchi wa nchi ya Uturuki wamemaliza kupiga kura ya maoni ambayo ilikuwa iamue kama Katiba ya nchi hiyo ibadilishwe na kumpa Raisi wa nchi madaraka makubwa kama ya Raisi wa JMTZ au ibakie kama ilivyo na madaraka madogo ambayo yako limited!

Sasa matokeo ya kura ya maoni yameonyesha kwamba wengi wao wanapendelea kuwa na Kiongozi mwenye madaraka makubwa yaani strongman dhidi ya Katiba ambayo madaraka ya Raisi yamevunjwa vunjwa kama waliyo nayo leo hii, matokeao ni 51.39% Ndiyo, na waliobakia Hapana!

Na tayari Raisi wa USA Donald Trump amempigia simu Raisi Tayyip Erdogan na kumpongeza kwa ushindi huo, sasa Uturuki inaongozwa na Katiba ambayo inampa Raisi madaraka makubwa sana!

Raisi Tayyip Erdogan sasa ni strongman wa nchi ya Uturuki!
89921635.jpg

Ndiyo madaraka makubwa ya Raisi au Hapana, kundi la ndiyo limeshinda!
89905455-600x400.jpg
 
Edogan is a dictator nadhani ndiyo maana hajajiunga na EU??? kama amjiunga amerekebisha kidogo
 
wewe acha upumbavu huyo erdogan ni dikteta uchwara kama mzee wako, tokea alipotaka kupinduliwa amekuwa muoga kila mtu ni adui kwake, sasa hiyo katiba mpya aliyoipitisha ndo kama yale mabadiliko mliyofanya kwenye katiba ya ccm!
 
Unachanganya mambo, Raisi wa Uturuki hajapitisha Katiba, bali Wananchi wa Uturuki ndiyo walioamua kubadilisha Katiba, kwani walipiga kura ya maoni!
 
Unachanganya mambo, Raisi wa Uturuki hajapitisha Katiba, bali Wananchi wa Uturuki ndiyo walioamua kubadilisha Katiba, kwani walipiga kura ya maoni!
una uhakika unachokinena? kuna tofauti gani kati ya mabadiliko ya katiba ya ccm na hayo ya uturuki yatakayo muweka madarakani erdogan hadi 2029?
 
una uhakika unachokinena? kuna tofauti gani kati ya mabadiliko ya katiba ya ccm na hayo ya uturuki yatakayo muweka madarakani erdogan hadi 2029?

Unaelewa nini kuhusu maana ya Demokrasia? Tuanzie hapo kwanza!
 
Lakini wao ndiyo wanaoutaka huo unaouita Udikteta na ndiyo maana wamepiga kura ya Ndiyo!
Ni kweli tuwapongeze uturuki kwa kupewa kile wanachotaka lakini huku kwetu wabunge dhalimu wa green party, waligomea sisi wananchi tusipate haki yetu ya kimaamuzi!
 
Wananchi wa nchi ya Uturuki wamemaliza kupiga kura ya maoni ambayo ilikuwa iamue kama Katiba ya nchi hiyo ibadilishwe na kumpa Raisi wa nchi madaraka makubwa kama ya Raisi wa JMTZ au ibakie kama ilivyo na madaraka madogo ambayo yako limited!

Sasa matokeo ya kura ya maoni yameonyesha kwamba wengi wao wanapendelea kuwa na Kiongozi mwenye madaraka makubwa yaani strongman dhidi ya Katiba ambayo madaraka ya Raisi yamevunjwa vunjwa kama waliyo nayo leo hii, matokeao ni 51.39% Ndiyo, na waliobakia Hapana!

Na tayari Raisi wa USA Donald Trump amempigia simu Raisi Tayyip Erdogan na kumpongeza kwa ushindi huo, sasa Uturuki inaongozwa na Katiba ambayo inampa Raisi madaraka makubwa sana!

Raisi Tayyip Erdogan sasa ni strongman wa nchi ya Uturuki!
89921635.jpg

Ndiyo madaraka makubwa ya Raisi au Hapana, kundi la ndiyo limeshinda!
89905455-600x400.jpg
Wananchi hawajui walivhokipigia kura na hawajaelimishwa vya kutosha hasa athari zake. Siku wakipata Rais mwendawazimu au hata huyu walienae akatumia mwanya wa mabadiliko haya watalia na kusaga meno.

Moja ya vipengele vibovu ni:
"He or she will be given sweeping new powers to appoint ministers, prepare the budget, choose the majority of senior judges and enact certain laws by decree."

"Parliament will lose its right to scrutinise ministers or propose an enquiry. However, it will be able to begin impeachment proceedings or investigate the president with a majority vote by MPs. Putting the president on trial would require a two-thirds majority."
 
Even Strong men/women dies but strong institution won't. WE want the latter.
 
Na wewe unaota hapa Tanzania tufanye kama walivyofanya waturuki eeeh..?

Kura ya maoni imeitishwa na mtawala mwenyewe, imesimamiwa na mtawala mwenyewe, na imetangazwa na mtawala mwenyewe.. Wenyewe waturuki wanalalamika faulo zimechezwa mubashara bila ya chenga, mradi mtawala apate kile atakacho..
 
Erdogan ameiba Kura na waangalizk wamesema by the way 51℅means a nation is divided
 
Punguza papara habari za hivi punde umoja wa Ulaya umetoa tamko uchaguzi umechakachuliwa sawa na ule wa Lubuva
Kura hewa kibao
Rais wa Uturuki mapovu yanamtoka Magu nyuma
Angalia BBC,ALJAZEERA na DW sasa hivi
 
Back
Top Bottom