Watumishi Wizara ya Ardhi wapora ardhi

Watumishi Wizara ya Ardhi wapora ardhi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wanatuhumiwa kutumia nyadhifa zao kupora shamba la hekari 74.2 mali ya Mwenegowa Mwichumu mkazi wa Kibada Kigamboni Dar es salaam.

Kabla ya uporaji huo shamba hilo lililokuwa na miti ya minazi, michungwa pamoja na miti mingine ambayo imeharibiwa na watu hao waliojimilikisha eneo hilo bila ya kufuata taratibu za kisheria.

Akizungumza na JAMHURI nyumbani kwake Kibada Mwinchumu anasema wafanyakazi hao kwa kuongozwa na ofisi ya kamishna wa ardhi kanda ya Dar es salaam kwa makusudi wameamua kupora eneo lake kwa kutumia vyeo vyao bila ya kufuata kama sheria inavyotaka.

Mwinjuma anasema katika tathmini hiyo mazao yake yalipewa bei ndogo tofauti na hali halisi na kupelekea eneo kufunguliwa jarada lenye kumbukumbu VAL/ PD/KB/1755 /Mgogoro namba 284 unatokana na mradi wa upimaji wa viwanja 20,000 katika Kata ya Kibada iliyopo katika Wilaya ya Kigamboni.

Anasema hayo yalitendeka mwaka 2004. Katika zoezi hilo maeneo mbalimbali yalifanyiwa tathmini na fidia kulipwa kwa kufuata taratibu za kisheria bila ya ubaguzi tofauti na hali ilivyokuja kutokea kwake.

“Cha ajabu walipofika katika eneo langu tathmini na upimaji ulifanyika kwa kiwango cha chini kwa kupunjwa eneo kubwa bila ya kuyafanyia tatmini hata mazao yaliyokuwemo ndani ya shamba hali ambayo sikukubaliana nayo,” anasema Mwinchumu.

Anasema pamoja na eneo lake kuwa na ukubwa hekari 74.2 lakini maofisa hao toka Wizara ya ardhi walibadili makadirio ya hekari 34 tu bila ya kutoa sababu za kuacha kupima eneo lote.

“Hapo ndipo mgogoro ulipoanzia nilipogoma kukubaliana upimaji wao ndipo wakaongeza hekari 10 kutoka za awali na kuwa 44 nilipo hoji sababu za kuacha kupima eneo lingine sikupewa majibu” anasema Mwinchumu.

Mwinchumu anasema maofisa hao mara baada ya kuona kwamba njama zao tayari amezishitukia wakalazimika kuahirisha zoezi na kupanga kuendelea siku nyingine.

“Baada ya mvutano wa muda mrefu na maofisa hao kwa mara nyingine upimaji ukapangwa kufanyika tarehe 21/3/2011 na mara hii upimaji wao ukaonyesha kuwa eneo hilo lina ukubwa wa hekari 74.2,” anasema Mwinchumu.

Anaeleza kwamba mara baada ya upimaji huo maofisa hao toka Wizarani walimuita ofisini na kuanza kumshawishi akubali kupokea hundi ya shilingi milion 148 tu ili aliache eneo hata hivyo akataa vilevile.

“Mara baada ya kuwakatalia niliwaomba nijaze fomu namba 70 ambayo hata hivyo sikupewa hapo ndipo nikaendelea kugundua kuwa kuna njama za makusudi za kutaka kunipora haki yangu,” anasema Mwinchumu.

Anasema mojawapo ya viwanja walivyogawiana ndani ya shamba lake kilichoporwa na watumishi hao ni kiwanja chenye kumbukumbu namba ID -228036 namba 332 chenye eneo la mraba 3,596, Kitalu namba 18 kilichotolewa Septemba 25 mwaka 2014 Kibada Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam.

Mbali na kiwanja hicho, anabainisha viwanja vyake vilivyoporwa ni kama ifuatavyo;

1. ID 230233 namba 206 kitalu 9 chenye eneo la mraba 56,955, kilichotolewa desemba 2, 2015 Kibada katika Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam.

2. ID 228034 namba 327 kitalu 18 chenye eneo la mraba 3,109 kilichotolewa Septemba 25, 2014 Kibada katika wilaya ya Temeke Mkoani Dar es salaam.

3. ID 228038 namba 335 kitalu 18 chenye eneo la mraba 2,751 kilichotolewa Septemba 25, 2014 Wilayani Temeke Mkoani Dar es salaam na vingine vingi.

4. ID 228035 namba 329 kitalu 18 chenye eneo la mraba 3,376 kilichotolewa Septemba 25, 2015 Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

5. ID 228039 namba 337 kitalu 18 chenye eneo la mraba 1,553 kili chotolewa Septemba 25, 2015 Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.

Mwinchumu anasema katika kuhangaika ili kupata haki yake ameandika barua kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kamishna Mkuu wa Ardhi Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Mkurugenzi wa Halmashauri ya kigamboni pamoja na Diwani kata ya Kibada bila mafanikio yoyote.

“Hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alipokuja Kigamboni nilibahatika kumueleza tatizo hili akapiga simu ofisi ya ardhi kanda ya Dar es salaam kwa mtu mmoja anaitwa Nathaniel Mhonge lakini hakuwa na jibu kuhusiana na jambo hili bali alikiri kulifahamu na kujiuma uma tu,” anasema Mwinchumu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kibada Saidi Pazi amekiri kufahamu mgogoro huo na kusema kuwa wanachofanya watendaji hao wa Wizara ni sawa na kuamua kumdhulumu Mzee Mwinchumu haki yake.

Anasema Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne katika kuchangia maendeleo,vitu hivyo ni ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora..

Pazi anabainisha kwamba kutokana na msingi huo wa Mwalimu Nyerere ardhi ni miongoni mwa misingi madhubuti ya Maendeleo ambayo ni haki kwa kila mwananchi kuwa nayo.

“Hali iliyopo leo ni kinyume kabisa badala ya viongozi wenye dhamana kutuongoza kuitumia ardhi kujikwamua kimaisha imekuwa ni tofauti wanahangaika kuipora toka mikononi wananchi tena kwa kutumia madaraka yao,” anasema Pazi.

Anasema kwamba Mzee Mwinchumu ni mmiliki halali wa eneo hilo ambalo alilirithi kutoka kwa wazazi wake ambao walishaaga dunia, lakini baadhi ya watumishi wa Wizara wamegeuka madalali wa kuuza viwanja hivyo.

“Kuna haja ya Rais kuiangalia kwa jicho kali Wizara hii kwani kuna baadhi ya watumishi wake sio waaminifu kwasababu badala ya kufanya kazi ya umma wamegeuka kuwa madalali wa kuuza mashamba ya watu kwa kutumia nyadhifa zao,” anasema Pazi.

Anasema mgogoro kati ya Mzee Minchumu na watumishi wa wizara ya ardhi umechukua muda mrefu kwakuwa watuhumiwa ni watumishi wa wizara kila analolifanya mlalamikaji wanahakikisha halifiki sehemu husika huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile (CCM) anakiri kuufahamu mgogoro huo na kusema kuwa ni mgogoro wa miaka mingi ambao suluhu yake imekuwa ikikwamishwa na baadhi ya watumishi toka Wizarani wenye maslahi nao.

“Mzee Mwenegowa Mwinchumu amewahi kuja ofisini kwangu kuomba msaada wa suluhu ya tatizo lake lakini limekuwa likikwamia ngazi za juu huko wizarani,” anasema Ndugulile.

Anasema ofisi yake inaandaa utaratibu utakao muwezesha mzee huyo kukutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ili aweze kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kupatiwa haki yake.

Dk. Ndugulile anasema ardhi iliyopo katika maeneo na mipaka ya vijiji kama ilivyoainishwa na taratibu za tawala za wilaya na kisha

kupewa hati ya usajili ya Kijiji huwa ina utaratibu wake wa namna ya kubadili matumizi lakini siyo kwa kuipora toka mikononi mwa wahusika kwa kutumia ubabe.

“Siku zote ardhi imekuwa kisimamiwa kwa mujibu wa taratibu husika ikiwa ni pamoja na sheria ya vijiji ya mwaka 1999 sheria No. 4 ya mwaka 1999 huku ikitoa mwangozo wa jinsi ya serikali kuchukua ardhi toka mikononi mwa wananchi inapotaka kubadilisha matumizi yake sio kufanya kama walivyofanya kwa Mzee Mwinchumu,” anasema Dk. Ndugulile.

Anabainisha kuwa, mamlaka ya serikali za Mitaa zina mamlaka ya kutoa maelezo yoyote yanayohusu ardhi kupitia kamati zake au maafisa wake waliochaguliwa kisheria kwenda kwa Kamishna wa ardhi wa eneo husika lakini juhudi zote hizo zikuwa zikikwamishwa na watendaji wa wizara.

JAMHURI liliwasiliana na Kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es salaam Nathaniel Mhonge ili kupata ufafanuzi kuhusiana na madai hayo ambaye amesema kwamba hawezi kuyaongelea kwa madai kuwa nje ya ofisi yake Mkoani Morogoro kikazi na kumtaka mwandishi kwenda wizarani.

Gazeti hili limefika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuweza kupata ufafanuzi kutoka ofisi ya msemaji wa Wizara Mboza Lwandiko aliyetaka kuandikiwa maswali ambayo yalipelekwa kwa Katibu Mkuu.

Lwandiko aliliambia JAMHURI kwamba Katibu Mkuu amesema hawezi kuzungumzia suala hilo, bali anayeweza kuongelea ni Kamishna wa Kanda.

Chanzo: Jamhuri
 
Salaam !!! Stori yetu ni hii.

Tajiri ‘ambipu' JPM

Na Mwandishi Wetu

MCHAKATO wa ufutaji wa vibali vya ardhi ambazo hazitumiki unadaiwa kuingiliwa na baadhi ya matajiri ambao hutumia ushawishi wao serikalini kufuta vya wanyonge ili wavitumie kwa matumizi yao.

JAMHURI lina taarifa kwamba katika orodha ya vibali vya ardhi vilivyowekwa mezani kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya kufutwa, vipo vya watu ambao hadi sasa hata hawajui kwamba umiliki wao wa ardhi unakwenda kufutwa.

Gazeti hili linafahamu kwamba jambo pekee linalowaokoa wale ambao hawajafutiwa vibali vyao hadi sasa ni umakini wa Rais Magufuli ambaye zoezi hili hulifanya kwa uangalifu.

"Hao wanaotakwa kuvuliwa vibali vyao wanatakiwa kumshukuru sana Ras John Magufuli kwa sababu halifanyi jambo hili kwa haraka. Anajipa muda na ana vyanzo vyake vya taarifa.

Angekuwa ni mtu wa kupokea tu taarifa na kusaini, watu wengi wangekuwa wanaumia kila mwaka. Yeye sasa ndiye tegemeo la wanyonge wengi ambao wangeumizwa na tabia hii mpya ya matajiri kungilia mchakato huo wa ardhi ili watumie maeneo ya watu wengine kwa faida yao.

JAMHURI lina mfano wa kiwanja chenye hati namba 35871, kilicho katika kitalu namba 270 kilichopo eneo la viwanda la Mbez Beach jijin Dar es Salaam ambacho sasa kimewekwa mezani kwa Rais kwa ajili ya kufutwa matumizi kwa maelezo kwamba hakijaendelezwa na aliyekuwa akikimiliki.

Hata hvyo, JAMHURI limefanya ziara katika eneo kiliko kiwanja hicho na kukuta kuna shughuli zinaendelea, kuna makontena yamewekwa kwa ajili ya shughuli za baadaye za mmiliki halali wa kiwanja hicho lakini ndiyo tayari umiliki wake uko hatarini kufutwa.

Wasamara wema ambao wanaishi katika eneo hilo ndiyo waliotoa taarfa kwa gazeti hili kwamba kuna mchezo mchafu unataka kufanywa na mmoja wa matajiri walio na ardhi katika eneo hilo kutwaa eneo la mwenzake ili kujinufaisha mwenyewe.

“ Sisi tunamjua mmiliki wa hili eneo. Huwa anakuja hapa na ni jirani yetu. Sasa tumetonywa na watumishi wasafi wa Wizara ya Ardhi kwamba umiliki wa hicho kiwanja unaweza kubadilishwa wakati wowote na Mhe Rais na kwamba faili liko mezani kwake Ikulu.

“ Kuna tajiri anapambana hili eneo la mwenzake liwe open space (eneo la waz). Yeye tumeambwa anataka kufungua Super Market hapa na lengo lake anataka hiyo open space itumike kama eneo la kuegeshea magari ya watu watakaokuwa wakija kununua vitu kwake.

“ Kinachotutisha ni kwamba huyu bwana leo kaanza na mwenzetu hapa. Akifanikiwa, hatujui atafanya nini kwa sisi majirani zake wenzake. Unajua taba mbaya haina dawa na ndiyo sababu tumeamua kukuita ndugu mwandishi ili muandike na hatmaye Mhe Ras ajue kwamba kuna watu wanamtegeshea mabomu, alisema mmoja wa majirani hao.

Eneo hilo ambalo JAMHURI lilifanikiwa kuliona lina ukubwa wa mita za mraba 885 na taarifa kutoka Wzara ya Ardhi zinaonyesha lilinunuliwa mwaka 1989 kwa kibali cha miaka 99 kuanzia Julai Mosi, 1989.

Taarifa hizi kutoka katika eneo moja tu la Tanzania, linazua maswali mengi kuhusu namna zoezi zima la ufutaji wa vibali vya umiliki wa ardhi kwa watu; hasa wale wanyonge linavyoendeshwa.

Kama eneo lililo barabarani kabisa jijiji Dar es Salaam linaweza kubadilishwa matumizi na kufutwa, itakuaje kwa maeneo yaliyo mbali na Dar es Salaam na kwingine ambako kuna matajiri wenye tamaa ya ardhi za wanyonge.

Majirani waliozungumza na JAMHURI kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa maelezo kwamba inaonekana tajiri anayetaka eneo la mwenzake ana marafiki katka ngazi za juu na anaweza kuhamishia hasira zake kwao, wameeleza kwamba Rais na watendaj wake wanatakiwa kuwa makini kwenye kufuta vibali vya umiliki ardhi vya wananchi.

“ Ras wetu anatetea sana wanyonge lakini hawezi kujua kila kitu. Ni kweli kwamba kuna maeneo mengi hapa nchini ambayo watu wameyanunua lakini hayatumiki na ni vizuri kugawa kwa watu wengine wenye uwezo wa kuendeleza.

“Lakini, kwa hapa kwetu, mtu anamiliki eneo halali, analiendeleza na amelipa kod zote kwa serikali kila mwaka kama anavyotakiwa na serikali inapokea kodi. Leo serikali kufuta kibali na kukifanya kuwa eneo la kuegesha magari, si kwamba itapoteza kodi inayopata kila mwaka, lakini itakuwa pia imemfukarisha mtu aliyenunua eneo.

“ Huu ni uonevu. Sisi tunaumia kwa sababu tabia hii ni mbaya na haifai. Watu watakuwa wanamchuka Rais wao pasipo sababu wakati kosa ni la watu wengne kabisa. Kwanza tuna bahati kwamba haya mambo yako mezani kwake Dodoma lakini bado Rais anafanya mapitio na hajaanza kufuta bado.

“ Jambo baya ni kwamba mwenye kiwanja hajapewa taarifa rasmi kwa maandishi kwamba eneo lake litafutwa na kubadilishwa matumizi hadi sasa. Barua tu hajapewa. Ile kuambiwa tu bwana wewe kuna hili linakuja. Ni kama vile anaviziwa. Sasa na sisi majirani tuna wasiwasi nini kitafuata, alisema mmoja wa majirani wa eneo lenye mgogoro.

Jambo lingine ambalo gazeti hili limeambiwa na wasamaria wema hao ni kwamba eneo lao hilo ni la viwanda na kwamba ujenzi wa kitu kama maduka ni tofaut na matumizi sahihi kwa sababu duka si kiwanda.

Gazet hili linaendelea na uchunguzi wake kuhusu jambo hili kwa kuzungumza na wahusika wote na kuona nakala halisi za vibali lakini kwa sababu ya ukweli kwamba Rais anaweza kubatilisha vibali vya sasa wakati wowote, limeona umuhmu wa kutoa taarifa hii mapema.
 
Back
Top Bottom