Watumishi wa serikali wengi elimu hawana ila wana vyeti.

365

JF-Expert Member
Nov 28, 2014
1,377
1,456
Haiwezekani mtu una elimu kuanzia diploma mpaka phd lakini unaendelea kulia lia mbele za watu eti serikali inaninyanyasa haitaki kunilipa stahiki zangu mara mishahara mara likizo mara kupanda cheo n.k.
Kama kweli una elimu ndani yako toa masharti (ultimatum )kwa mwajiri wako,akishindwa kutimiza masharti acha kazi maramoja.

Ila kwa kua wengi elimu kichwani ni zero ila vyeti 100,mtaendelea kudai mpaka mnazeeka mwisho wa siku mnakosa uzalendo wa nchi kwa ajili ya kinyongo cha muda mrefu.

Kwenye maisha kitu pekee cha hatari ni muda,sasa kama wewe unadai toka 2016 ukaja kulipwa 2020 mwezi wa saba,hayo malipo yatakusaidia nini?

Tafakari kwa kina kisha amua
 
Mleta mada sijui umekula maharage ya wapi.
Umejiharishia hadi umejichafua.
 
Watumishi Wengi Wa Serikali Wana Vyeti Vya Marehemu (wamebashite). Ndiyo Maana Taasisi Na Mashirika Ya Serikali Havifanyi Vizuri.

Angalia shule, hosp, wanasheria, na mashirika mbalimbali ya serikali vyote hoi.

Kwahiyo Hata Kugoma Hawawezi
 
Mtoa mada una tatizo tena tatizo kubwa kichwa ni huo sasa ni ugonjwa kwa title uliyoitoa.

Nchi iko makini na watumishi wako makini na wana elimu zao na hawana shida unazozifikiria wewe.

Mambo ya madai ni ya kawaida tu kwa Serikali yoyote duniani wala hakuna shida.

Usijaribu kuona wewe ndiyo una akili sana tuna vichwa vilivyo tulia na vinafanya mambo yake ndani ya Serikali kila kukicha.

Wape heshima yao usitoe maneno ya kudhihaki
 
  • Thanks
Reactions: 365
Haiwezekani mtu una elimu kuanzia diploma mpaka phd lakini unaendelea kulia lia mbele za watu eti serikali inaninyanyasa haitaki kunilipa stahiki zangu mara mishahara mara likizo mara kupanda cheo n.k.
Kama kweli una elimu ndani yako toa masharti (ultimatum )kwa mwajiri wako,akishindwa kutimiza masharti acha kazi maramoja.

Ila kwa kua wengi elimu kichwani ni zero ila vyeti 100,mtaendelea kudai mpaka mnazeeka mwisho wa siku mnakosa uzalendo wa nchi kwa ajili ya kinyongo cha muda mrefu.

Kwenye maisha kitu pekee cha hatari ni muda,sasa kama wewe unadai toka 2016 ukaja kulipwa 2020 mwezi wa saba,hayo malipo yatakusaidia nini?

Tafakari kwa kina kisha amua
Pia wengine wamefoji vyeti...maana kupata ziro sio tatizo kufoji vyeti ndio utata unapo anza
d9dc82fa6196c5c82d99f45e29ed96c7.jpg
 
Back
Top Bottom