Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 482
- 969
Wasalam mabibi na mababu...
Hili kundi linaloitwa watumishi wa serikali lina safari ndefu sana kutoboa kimaisha, hili kundi thamani yake inayochukuliwa na wanasiasa ni ndogo mnoo, sijajua linashushwa hadhi kwa vile halina desturi ya kuandaamana na kufanya migomo!
Niki kumbuka kipindi cha magufuli halilifutia hili kundi annual increment ambazo Zipo kisheria kabisa, hakuna nyongeza alowahi kuifanya katika utawala wake na alidiriki kusema wazi hadharani kuwa 'kama unaona mshahara haukutoshi basi acha kazi' mpk mtu anafikia kusema hivi manake amekumudu na haufurukuti.
Nikija kipindi cha huyu mama mwaka jana kaweka 23% ambayo kimsingi ni kama iliwabeba wachache tu, na ilipofika mwaka huu katoa porojo nyingi sana za kurudisha annual increment km ilivyo miaka ya nyuma na kujinasibu kuweka nyongeza ya kimya kimya lkn kilichotokea leo kwa watumishi hakuna ata thumni iliyo ongezeka hii manake nini n kuwa hili ni Kundi ambalo linaweza kufanyiwa chochote kile mana halina madhara kwa serikali, Yani wanajua kulimudu kutokana na kundi hili kutojua kusimamia haki zake pamoja na kujitambua.
Mama hana presha kabisa na hili kundi mana washauri wake kina mwigulu washampa mbinu za kucheza na hili kundi imagine sasa hv watumishi watatoa matusi ya kila namna kutokana na uchungu wa kutoongezewa kitu tena ikiwa Rais wa nchi kaahidi kabisa lkn ikifika kipindi cha kukaribia uchaguzi kukiongezwa kidogo au lile kundi kubwa la watumishi likipewa posho za kusimamia uchaguzi baaasi matusi yoote tunasahau na kuanza kujikomba komba kwa Mwenye nchi.
Mzee jakaya kikwete historia ITAENDELEA kumtambua kwa juhudi zake na mapenzi yake alokuwa nayo katika kundi hili la watumishi kwani alijua kuwapa morali na motisha ya watu kufanya kazi bado hajatokea Rais kumpiku kikwete hususani katika maslahi ya watumishi.
Hivi Mama samia unadhani kuanzia jumatatu watu watafanya kazi kiufanisi na kwa morali kwa Kitendo hiki ulichowafanyia kweli??? Yani nyie mnalipana maposho ya kufa mtu ila kuwaongezea wenzenu ata hii keki ya taifa tuifaidi wote hamtaki!!! Aya masononeko ipo siku mtalipa tu...