wwww
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 350
- 252
Wanajamvi nimepata taarifa kutoka chanzo changu ndani ya Jeshi la Polisi kuwa watumishi raia wote waliopo huku wanatakiwa kwenda depo kuhenya ili atimaye kutekeleza amri ya Rais aliyoitoa siku alipokuwa anawapandisha vyeo Makamishina wa Polisi aliposema hataki kuona Raia yeyote kwenye majeshi ya Tanzania.
Hivyo naambiwa tarehe 09.08.2016 kulifanyika kikao Makao Makuu ya Polisi (PHQ) chini ya Kaimu Kamishina wa Utawala akiwapa taarifa hiyo Raia ili waendelee kutafakari kuhusu suala hilo wakati wao wakisubiri maelekezo mengine kutoka Ikulu. Kwa mujibu wa mtoa taarifa Kamishina wa Utawala aliwaahidi watumishi hao kuwa watazingatia vitu vifuatavyo katika kutoa vyeo kwa watumishi raia watakaokwenda depo na hatimaye kuwa askari polisi;
1. Muda wa utumishi wake Serikalini / Polisi
2. Cheo alichonacho sasa cha uraia
3. Mshahara anaolipwa kwa sasa
4. Elimu aliyonayo
5. Nafasi aliyopo kwa sasa
Vigezo hivi vitalinganishwa na askari Polisi ambaye anafanya kazi kwa sasa
Kwa taarifa niliyopewa ni kwamba mwitikio ni mdogo sana hasa kwa watumishi wenye elimu kubwa lakini kwa wahudumu na makatibu mhutasi mwitikio umekuwa mkubwa sana.
Pia mkumbuke kuwa hata huko JWTZ nako kuna kitu kama hiki kilishafanyika na kinaendelea kufanyika.
My Take: Rais Magufuli ametafakari kwa kina kuhusu jambo hili au hana washauri, itakula kwake. Ebu tusubiri tuone hii sinema.
Naomba uzi huu usiunganishwe na uzi mwingine ili watu waweze kujadili suala hili kwa kina na kwa usalama wa nchi yetu.