Watumishi hewa na mafisadi uchwara

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,168
8,142
Suala la watumishi hewa wa serikali linaelekea kuota mizizi!Kwamba Wiara ya Afya nako mabilioni yametafunwa ni suala la kusikitisha!! Ikumbukwe kwamba, Wizara ya Afya na Sekta ya Elimu tayari zimeshatafunwa zaidi ya TShs. 7 billion!! Aidha, mabilioni haya yametafunwa na yataendelea kutafunwa licha ya serikali kuamua kupitishia mishahara ya watumishi wake benki kama njia ya kudhibiti wizi huu!! Tatizo nini? Kwa maoni yangu, Mabenki na serikali wakiamua kushirikiana wana nafasi kubwa kabisa ya kudhibiti suala la mishahara hewa. September na Oktoba 2008 nikiwa nafanya kazi kwenye benki moja jijini, niliongezewa jukumu la ku-post mishahara ya wafanyakazi wa serikali pamoja na pensheni. Katika muda huo wa miezi miwili, nilifanikiwa kuzigundua akaunti tatu za waalimu ambazo zilitumika kuiibia serikali! Baada ya kufanya uchunguzi wangu binafsi, nikagundua mmoja wa wenye akaunti hizo alikuwa ni fundi seremala mitaa ya Keko!!!! Sina hakika endapo alishawahi kuwa mwalimu kabla ya hapo! Kwa kuzionea uchungu pesa za serikali (au nami ni JOKA LA MDIMU?!), nilikata shauri la kuzi-hold akaunti husika huku nikiamini kwamba endapo akaunti hizo ni halali kwao basi lazima wangekuja kulalamika. Hata hivyo, hadi natoka sikuona mteja aliyekuja kulalamika kwamba akaunti yake imekuwa-held!
Pamoja na yote hayo, ikumbukwe kwamba kipindi hiki ilikuwa tayari serikali imeshafanya uhakiki wa kugundua watumishi hewa katika sekta ya elimu! Hii maana yake ni kwamba pamoja na jitihada za sasa, lakini bado serikali itaendelea kupoteza mapato kupitia njia hii. Ingawaje nilifanya zoezi hili kwa siku chache, lakini tayari nilishazigundua akaunti tatu! Sina hakika, hadi sasa ningekuwa nimegundua akaunti ngapi!
Hata hivyo, serikali isijisumbue kuziagiza benki kutafuta ghost accounts kwani ni very complicated and boring practice inayohitaji umakini na committment ya hali ya juu wakati marginal productivity yake inaweza kuwa ndogo! Labda, hilo linaweza kuwa na matunda endapo tu kutakuwa na special task force kwa ajili ya shughuli hiyo peke yake; vinginevyo itakuwa ni sawa na kuwaagiza watafiti watafute dawa ya UKIMWI badala ya kuwaagiza wananchi waache kuendekeza ngono zembe na ngono kwa ujumla! Binafsi, sikuwa na fomula maalumu ya kugundua akaunti hizo!
Mambo yafuatayo ndiyo yanayochangia zaidi kuwepo kwa watumishi hewa:
LOOPHOLE 1: UHAMISHO: Nazani wafanyakazi wengi wa serikali wapo chini ya halmashauri. Na ilivyo, wengi wa wafanyakazi hawa mwajiri wao ni halmashauri husika ingawaje mlipaji wa mishahara na Hazina! Hivyo, mathalani Mr. Q anayefanyakazi kazi Halmashauri X anahamia Halmashauri Y, maana yake ni kwamba Mr. Q si mwajiriwa tena wa Halmashauri X. Sasa endapo Mr. Q ataangizwa kwenye payroll ya Halmashauri Y kabla Halmashauri X hawajaondoa jina lake, maana yake ni kwamba Mr. Q ataendelea kupata mishahara miwili ( from Halmashauri X na Y) hadi jina lake litakapoondolewa kwenye payroll ya Halmashauri X. Uzoefu unaonesha kwamba Mr. Q anaweza kuendelea kupokea mishahara miwili kwa zaidi ya miezi 3 !! Sasa assume, at any given month, mfanyakazi mmoja anapata uhamisho kwa kila halmshauri. Nazani TZ kuna halmashauri zisizopungua 200 ( consider namba ya wilaya zilizopo)! Hii maana yake ni kwamba at any given month, watumishi 200 watakuwa wanahama kutoka halmashauri moja kwenda nyingine. Kwa takwimu hizo, kwa wastani kwa mwaka mmoja angalau watumishi 2000 watahama kutoka X kwenda Y. Also assume, tukitoa PAYE inayorudi serikalini, serikali inalipa sh. 100,000/= kwa kila mtumishi! Hii maana yake ni kwamba, kwa mwaka mmoja pesa itakayopotea kwa wafanyakazi hawa (assume marekebisho ya payroll yanafanyika baada ya miezi mitatu) ni:
= 2000 x 100,000 x 3 = TShs. 600,000,000/ = kwa mwaka! Kutokana na utaratibu wa sasa wa kupitishia mishahara benki, pesa hizi huwa zinatafunwa na watumishi wenyewe kutokana na uzembe wa mwajiri wake.
SOLUTION: Kuokoa kiasi hiki cha pesa ni kazi ndogo kama kufumba na kufumbua!! Ni suala tu la Council Directors au Watunza Hazina kupeleka barua kwenye paying bank/branch kwamba Mr. Q is no longer an employee wa Halmashauri husika na hivyo kutoa order ya ku-hold ( sio kufunga akaunti) kiasi cha pesa equivalent to his Take Home Pay ! Aidha, wataagiza review iwe inafanyika kila wakati hadi Hazina watakapoacha kutuma mshahara kwenye former council!
LOOPHOLE 2: PLACEMENT (Case I): Hapa pesa zinatafunwa kwa namna mbili. Namna ya kwanza zinatafunwa na watumishi wenyewe na namna ya pili zinatafunwa na watendaji wenye dhamana! Assume serikali imeajiri wataalamu wa kilimo 2000 kupitia halmashauri zake. Hii inavyotokea ni kwamba wengi wao wanaenda kuripoti kwenye maeneo yao ya kazi. Lakini baada ya kutoridhishwa na sehemu waliyopangiwa baada ya kuona mazingira ya huko, wengi utakuta wanaaga wanafuata mizigo yao nyumbani ili waje kuanza kazi rasmi! Miongoni mwa hawa, si wote ambao wanarudi tena lakini tayari wanakuwa wameshaingia kwenye govt payroll! Kwavile Directors wanashindwa kuchukua hatua mapema, utakuta mtu huyo anaendelea kuingiziwa mshahara hata miezi mitatu hadi sita mbele wakati si mfanyakazi wake tena! Fanya kukisia ni watumishi wangapi wanaaga kufuata mizigo halafu hawarudi tena (abconded) wakati wapo kwenye payroll na ndipo utakapopata picha ya pesa zinazopotea.
SOLUTION: Directors wanatakiwa ku-discourage ruhusa za namna hii ( za kufuata mizigo) wakati wa kukaribia mwisho wa mwezi na badala yake ruhusa za namna hiyo ziwe zinatolewa mwanzo wa mwezi. Na mara ruhusa zinapotolewa, paying bank/branch iagizwe ku-hold akaunti ya mtumishi husika na kuwa released pale tu atakaporejea!
PLACEMENT (Case II). Hii inatokea zaidi kwenye halmashauri zenye idadi kubwa ya watu. Wakati wanaotafuna pesa kwenye Case I ni watumishi wenyewe, wanaotafuna pesa kwenye Case II ni wafanyakazi wa halmashauri kwa kushirikiana na watu wao. Katika Case II, unakuta mtumishi aliyeajiriwa na halmashauri husika anaacha kabisa kuripoti kituo cha kazi! Wanapoacha kuripoti, mafisadi uchwara wa halmashauri wanawatumia ndugu/jamaa/rafiki zao na kuwapatia barua za utambulisho pamoja na vitambulisho ili wakafungue akaunti benki (paying branch) kwa majina ya wale wafanyakazi ambao hawajaripoti! Hebu fanya kufikiria, ni watumishi wangapi wanaacha kuripoti vituo vyao vya kazi ndipo utakapopata taswira ya fedha zinazopotea kwa mtindo huu!!! Mbaya zaidi, hawa ndio haswa ghost employee kwavile wataendelea kuzitafuna pesa hizi kwa muda mrefu sana!!
SOLUTION: 1. Serikali iwe inatuma photos/passport size specimen in advance kwenye expected paying bank/branch. Nimeeleweka? Assume serikali inatarajia kupeleka waalimu 50 wilaya ya Lindi Vijijini. Kwavile imezoeleka wafanyakazi hawa wanafungua akaunti NMB, basi kabla hawajaenda kuripoti, serikali ipeleke photos/passport size specimen NMB Lindi Branch! Kwa staili hii, hakuna fisadi uchwara atakayempandikiza ndugu yake kwenda kukomba mshahara wa mtumishi yeyote ambae hajaripoti.
SOLUTION 2: Bankers, acheni watu wawaite mna usumbufu ili mradi tu wanaokusema hivyo wanaona unafuata utaratibu. Mara kwa mara nilikuwa nawaona waalimu (hususani wa sekondari) particularly kutoka wilaya ya Mkuranga. Unakuta mwalimu ambae ni mwajiriwa mpya anakuja na barua ya utambulisho wa mwajiri ambayo wala haina picha, na hata kama picha inayo, unakuta haijapigwa muhuri!! Utamu zaidi, unakuta mtumishi huyo anakuja na cover la kitambulisho ambalo nalo halina picha!! Ukimuuliza kwanini hamna picha, utakuta anatoa picha kwenye pochi ili abandike mbele yako!!! Ukimwambia kitambulisho chako hakina sifa za kuitwa kitambulisho, atalalamika dunia nzima, kwamba benki/NMB mnasumbua!!! SHIT! Ni kweli, mtu aliyekusudia ku-foji hawezi kuja kizembe namna hiyo, but always wajanja wanakesha kutafuta loophole!! Wakati nikiwa bank, ningeweza nisiwe strict sana wakati nafungua akaunti ya raia wa kawaida, lakini ile tu kuniambia ni mfanyakazi wa serikali, ungenifanya niwe more attention kuliko otherwise!!
Kuna mengi ya kueleza lakini najihisi kukosa utaalamu wa ku-summarise matokeo yake thread imekuwa ndefu kiasi kwamba itashindwa kufikisha kilichokusudiwa! Hatuna utamaduni wa kusoma aya ndefu ndefu kama hizi!! But all in all, tuungane kupiga vita ufisadi huu!!
 
Mishahara yenyewe laki moja hata akipokea miwili ni sawa na hukuna kitu mbona mafisadi wanavuna bilions bila hata kuvuja jasho achana na hawa wakikutwa na hizo ngekewa wazifaidi kodi zao!
 
Back
Top Bottom