Watumishi 9000 wapya kuajiriwa Wizara ya Afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watumishi 9000 wapya kuajiriwa Wizara ya Afya

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 5, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda​


  Nora Damian
  JUMLA ya watumishi wapya 9,000 wanatarajiwa kuajiriwa mwaka huu katika sekta ya afya kuziba pengo la uhaba wa watumishi linalozikabili halmashauri nyingi nchini.

  Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa 12 wa wadau wa sekta ya afya kuhusu tathmini ya huduma za afya nchini, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda alisema wizara hiyo ina uhaba wa asilimia 42 ya watumishi. “Tunaandaa mazingira ya kuweka vivutio vya ziada kama mishahara posho na nyumba, ili kuwafanya watumishi wetu wasikimbie vituo vyao vya kazi,”alisema Dk Mponda.

  Alisema wizara yake ina changamoto nyingi katika kutoa huduma zilizo na uwiano, zitakazomfikia kila mtu na kwamba wameongeza udahili kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya afya na wataajiriwa watakapomaliza masomo yao.

  Alisema kwamba, maeneo mengi yenye mazingira magumu nchini ndiyo yanaongoza kwa kuwa na uhaba mkubwa wa watumishi.
  Hata hivyo, alisema watumishi wengi wamekuwa hawaripoti kwenye vituo wanavyopangiwa hasa katika maeneo hayo ambako kati ya mwaka 2007 hadi 2010 asilimia 37 ya watumishi hawakuripoti kwenye vituo vyao vya kazi.

  Waziri huyo alisema changamoto nyingine inayowakabili ni vifo vya uzazi pindi mama anapokuwa mjamzito hadi anapojifungua na mtoto wake.

  Licha ya changamoto hizo, waziri huyo alisema pia wamepata mafanikio makubwa hasa katika kupambana na magonjwa mbalimbali kama malaria, kifua kikuu, virusi vya ukimwi na ukimwi ambapo maambukizi yamepungua kutoka asilimia 12 mwaka 1990 hadi asilimia 5.6 mwaka huu.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama (Sikika) Irenei Kiria akizungumza kwa niaba ya asasi za kiraia, aliitaka serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama ya sherehe safari na posho na kutenga fedha za kutosha katika sekta ya afya ili kuokoa wananchi.

  Katika bajeti ya mwaka huu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetenga Sh 515 milioni kwa ajili ya sherehe fedha ambazo zinatajwa kuwa zingeweza kuhudumia afya za wananchi.

  Alisema serikali imekuwa haitengi fedha za kutosha katika sekta ya afya kwa kisingizio kwamba ina wafadhili wengi ambapo katika bajeti ya mwaka huu, asilimia 97 ya fedha zimetolewa na wafadhili huku serikali ikichangia asilimia tatu.
  “Kama serikali inawaachia wafadhili maana yake inajiondoa katika jukumu lake la kikatiba la kuhudumia wananchi,”alisema Kiria.

  Alisema serikali inakwenda kinyume na mkataba wa Abuja wa mwaka 2001 ambao unaelekeza nchi wanachama kutenga asilimia 15 ya bajeti katika matumizi ya sekta ya afya.

  Alisema pia bajeti ya afya imekuwa ikishuka siku hadi siku ambapo kwa mwaka 2010/11 ilikuwa asilimia 11 lakini mwaka 2011/12 imeshuka hadi kufikia asilimia 8.9.

  Asasi hizo pia zililalamikia serikali kwa kushindwa kuajiri watumishi wa afya wa kutosha kama inavyoombwa na halmashauri husika na uhaba wa mashine za kupima chemchembe za damu kwa waathirika wa virusi vya ukimwi maarufu kama CD4.

  Kiria alisema baadhi ya wilaya nchini kama za Misenyi, Sumbawanga na Temeke zilipelekewa watumishi wachache tofauti na idadi waliyoomba.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  wapuuzi hawa yaani watumishi wanaongelewa hapa ni medical attendants na sio watumishi wenye kiwango kikubwa cha elimu.kati ya hao 9000 ni chini ya 300 ndio wana elimu ya udaktari(M.D).kwa mwaka tanzania inazalisha zaidi ya madaktari ya 400 sasa hawa wengine waende wapi?nasikitika kuona hospitali za mikoa ambazo sasa zimepewa hadhi ya rufaa bado zinaendelea kuwa na clinical officers na AMOs wakati kuna M.Ds wa kutosha mpaka wanaenda rwanda.sitegemei kuona mabadiliko yakiletwa na hawa attendants wanaoingia kwenye field ya afya baada ya kufail form four,hawa ndio hujivika title na kujiita madaktari na mara nyingi wamekuwa source ya kutoa misleading health education.kama yule clinical officer wa loliondo aliyesema dawa ya babu imetibu ukimwi.kama serikali inaona attendants ni muhimu katika kuendeleza afya ya mtanzania basi ni vizuri isipoteze hela kusomesha graduates ambao wanatumia rasilimali nyingi.mlichakachua elimu sasa mmeanza kuchakachua afya.ngoja nitafute hela nikaishi india!!!
   
 3. wajaleo

  wajaleo Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hii wizara ni ya afya na ustawi wa jamii ila marazote nasikia afya tu hawa watu waustawi wajamii'sociology'hawatajwi kabisa hata katika nafasi za kazi wala takwimu zao hatupewi..Kama vipi wangepewa wizara yao hapa naona kama wamekuwa wanasindikiza wanashindwa kuwajibika.
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Hapo umesema mkuu. Unaposoma sasa hivi untakiwa kuwa makini sana na aina za kozi. Ktk wizara nyingi hao watu wa sociology wamekuwa wakitumiwa kama boosters tu, kwenye miradi mingi. Sijawahi kuona kazi au mradi ambao unajisimamia wenyewe kama purely social project. Utaona mara nyingi wanatumiwa kwa muda tu then kwishnei
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Sasa kama wenyewe hawako creative and aggressive nani atawakumbuka? Hata maofisini,ukiwa mvivu wa kufikiri na limitation kibao wote mnataka kubanana dsm hauwezi kusonga mbele wala kupata heshima. Ni muhimu watu kuwa creative,ukiingizwa kama sociologist kwenye project,ukafanya kazi uliyoitiwa ukiimaliza inabidi upishe waendelee. Ukiwa creative unahakikisha unafunua opportunity zote na ku-reccomend issues za kukutaka uendelee kuwepo. Ndo maana unakuta wenzenu project inaanza mwanzo tu wanaiita 'phase 1' manake wanajua 2 lazma itengenezwe! Stukaaa!
   
 6. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Acha hasira bro!
   
 7. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hasira zikowapi dogo?
   
Loading...