Watumishi 102 hawajaripoti kazini

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WATUMISHI wapya 102 kati ya 216 waliopangiwa kufanya kazi katika wilaya ya Biharamulo kwa mwaka wa fedha wa 2010/11, hawakuripoti kazini.Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Ernest Kahindi, alisema juzi kuwa, hali hiyo imeifanya wilaya kuwa na upungufu wa watumishi, hivyo kuzorotesha utendaji kazi.

Alisema serikali iliidhinisha ajira kwa watumishi hao wapya, lakini mpaka sasa, walioripoti ni 114. Mkuu huyo wa wilaya alisema sababu kubwa iliyowafanya watumishi hao kushindwa kuripoti ni mazingira ya wilaya kuwa katika sehemu ya pembezoni.

Alisema kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wanapokumbana na mazingira kama hayo wanaamua kutafuta sehemu zingine ambazo wanadhani kuna unafuu, ikilinganishwa na Biharamulo au wilaya zingine zilizoko pembezoni.

Kahindi alikuwa akitoa taarifa kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Nassor Mnambila kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, katika ziara ya mafunzo kuhusu mabadiliko katika utumishi wa umma awamu ya pili wilayani humo.

Kahindi pia alisema katika kuhakikisha watumishi wanafuata kanuni, taratibu na maadili ya kazi, wilaya yake imechukua hatua mbalimbali dhidi ya watumishi wanaokiuka miongozo hiyo.

Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja, watumishi 30 wamechukuliwa hatua za kinidhamu kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya kudai na kupokea rushwa.

Kwa mujibu wa Kahindi, miongoni mwa wa watumishi hao ni maofisa watendaji wa kata na vijiji na baadhi yao wamefikishwa mahakamani.
 
mi sishangai maana uzembe upo kuanzia ngazi ya juu,hakuna mtu anayefikiria, kila mtu amebaki akifikiria jinsi anaweza kuingiza bomu lake, na usishangae na mishahara watalipwa kama kawa,
 
Back
Top Bottom