unatumia mtandao gani?
Za weekend wana jukwaa,
Napenda kutoa uzi huu tushirikiane kwa pamoja najua ni wengi wanakumbwa na hili tatizo na hawana ufumbuzi
Tatizo: Mara kadhaa nakutana na tatizo la kutokuwa hewani yani mtu anapo nipigia simu anaambiwa sipatikani kwa muda hivi, ilihali simu ipo ON wakati mwingine napatikana.
Wenye kufahamu utatuzi wa hii ishu na chanzo chake nini mnakaribishwa.
hilo tatizo na mimi linanikuta mtu akinipigia kwa kutumi namba yangu ya VODA hanipati ila akipiga kwa kutumia TIGO ananipata
Android smartphones sometimes zinapata tatizo la Network bands..Inaweza ikaonesha 3G au HSPA/HSDPA kumbe kwa wakati huo signal strength ipo chini.. Cha kufanya, endapo upo maeneo yenye poor network shusha network hadi 2G/GSM only kwa kutumia Mobile network settings options au Phone Testing Code *#*#4636#*#*(baadhi ya Simu).... Kama walivyosema wengine, kuna wakati mtandao unakua na shida, so usiipigize simu yako buree!