Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411

Zaidi ya kilogramu 730 za dawa za kulevya za aina mbalimbali ikiwemo Bangi,Mirungi na Heroine zimekamtwa katika matukio 409 huku watuhumiwa 564 wakikamatwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla ameyasema hayo wakati akipokea mwenge wa uhuru ambao umeanza mbio zake mkoani humo ukitokea mkoa wa Iringa.
Akitoa ujumbe wa mwenge kuhusu utumiaji wa dawa za kulevya,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,George Jackson Mbijima amesema dawa za kulevya zimekuwa na athari kubwa kwa jamii hasa vijana ambao wanapotumia hupoteza mwelekeo wa maisha yao.
Mwenge wa uhuru ukiwa katika siku yake ya kwanza mkoani Mbeya umekimbizwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mbarali ambako umezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni tano.
Chanzo: Capital Radio