chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,369
- 27,786
Watuhumiwa 25 wanaoshikiliwa kwa
vitendo vya ugaidi katika Tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro, wamepandishwa kizimbani.
Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Morogoro na kusomewa mashitaka tofauti ya kula njama, kujiandaa kuvamia kituo cha Polisi na kusudio la kutekeleza mauaji ya watu.
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani jana kwa nyakati tofauti, ambapo 12 walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya tatuwakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Walifikishwa kwa mara ya pili Mei 6, mwaka huu.
Watuhumiwa hao walisomewa mashitaka manne mbele ya Hakimu wa Mkazi wa mkoa, Erick Rwehumbiza, na Wakili na Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Sunday Hyera, akishirikiana na Edgar Bantulaki.
Mwendesha mashitaka alidai washitakiwa wote 12 wa awali, wanakabiliwa na makosa manne ikiwa ni pamoja na kula njama kwa nia kutenda kosa la kigaidi Aprili 14, mwaka huu Kitongoji cha Nyandeo Kijiji cha Chikago, Kata na Tarafa ya Kidatu, wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Wote wanakabiliwa na makosa ya ugaidi kinyume na Kifungu cha 27 C Sura Namba 21 ya mwaka 2002, kukutwa na silaha kinyume cha Kifungu cha Sheria Namba 246 cha mwaka 2002, kukutwa na sare za jeshi na milipuko kinyume na sheria wakiwa ndani ya Msikiti wa Suni Kidatu.
Aliwataja washitakiwa wa kundi la kwanza katika kesi Namba 16/2015 mbele ya hakimu huyo ni Majaliwa Mohamed Ngarama, Malick Abbas Kanju na Muhundi Omari Jambia, au kwa jina lingine kama Athuman Mkumba.
Wengine ni Juma Ismail Salum, maarufu kama ¡® Shebuka¡¯, Nassir Abdallah Musa ama kwa jina lingine ¡® Juru Kessy¡¯ na Ally Shaaban Athuman.
Watuhumiwa wengine ni Ramadhan Hamis, maarufu kwa jina la ¡®Wawa¡¯, Juma Ramashan Ibrahim, Hassan Ally Hamis, Hamis Hassan Ntuko na mmoja aliyeongezwa katika kesi hiyo, Maulid Hassan Seleman.
Kundi la pili lenye washitakiwa 13 walipandishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka saba tofauti yanayolingana na wengine 12 wa kundi la kwanza, isipokuwa mmoja akikabiliwa na shitaka la kufanya jaribio la kuua watu watano kwa bomu la mkono.
Mtuhumiwa huyo Khalid Omary Jumbe, katika shitaka hilo, anashitakiwa kwa kuwarushia bomu la mkono watu watano waliokuwa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi mwaka huu wakiwa eneo la Ofisi ya CCM Msolwa wilayani Kilombero kwania ya kuwaua.
Alisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Agripina Kimanze, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Sunday Hyera, alidai washitakiwa wote pia wanashitakiwa kwa kosa la kula njama chini ya Sheria ya Kupambana na Ugaidi ya mwaka 2002.
Mwendesha mashika huyo alidai kuwa Aprili mwaka huu na Mei Mosi mwaka huu katika maeneo tofauti ya Ruaha na Kidatu wilayani Kilombero, walikula njama kwa kufanya matendo ya ugaidi na kutaka kuwauawatu na kuwadhuru.
Mbali na Jumbe, Hyera alitaja watuhumiwa hao wengine ni John Wales au Abuu Majanga, Ridhiwani Issa Mwiru au Vosa, Fredrick Evarist Chamnungu au Abuu Mansour na Yusuf John Juma, kwa jina jingine Bikihayo au Abuu Beude.
Wengine ni Juma Abdallah, Shomary Singo, Ally Abdallah au Enzi Mngindo,Khamis Nahoda, Hamis Islam, Rahibu Msuya, Dawali Msuya na Athuman Jumbe.
Hata hivyo, baada ya kusomewa mashitaka yao, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezeo kisheria ya kusikiliza kesi za ugaidi isipokuwa Mahakama Kuu pekee.
Kutokana na maelezo hayo, kesi hizoziliahirishwa. Kesi ya kundi la watu 12 iliahirishwa hadi Juni 26, mwaka huu na nyingine hadi Juni 5, mwaka huu.
Chanzo : Habari Leo