Watu zaidi ya milioni 4 wapoteza maisha kwa maambukizi ya Virusi vya Corona duniani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Watu zaidi ya milioni 4 na laki tano wapoteza maisha kwa corona duniani

Aug 31, 2021 03:46 UTC

[https://media]

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa jumla ya watu milioni 217 laki tatu elfu 67 na 883 wamepatwa na maambukizi ya corona duniani hadi sasa huku wengine milioni 4 na 518,030 wakiaga dunia kwa ugonjwa wa UVIKO-19 duniani kote.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Reuters, hadi sasa watu milioni 194 na 299,697 wamepona UVIKO-19 duniani. Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corna na pia kwa watu walioaga dunia.

Marekani, India na Brazil kwa utaratibu zinaongoza kwa kuwa na idadi ya juu ya watu walioaga dunia kwa corona kufikia sasa. Hans Kluge Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Ulaya amesema kuwa, idadi ya maambukizi ya corona barani Ulaya wiki iliyopita yaliongezeka kwa asilimia 11; na utabiri kwamba hadi kufikia tarehe Mosi Disemba watu 236,000 barani Ulaya watapoteza maisha kwa ugonjwa wa UVIKO-19 ni sahihi.

Wakati huo huo Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimeripoti kuwa, hadi kufikia juzi mchana bara hilo lilithibitisha kesi milioni saba 721,121 za maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19 barani humo.

Kituo hicho cha Africa CDC kimeeleza kuwa, idadi ya watu walioaga dunia kwa UVIKO-19 barani Afrika hadi sasa ni 194,160 huku wagonjwa milioni 6 na 854,726 wakipona corona. Afrika Kusini, Morocco, Tunisia na Ethiopia ni kati nchi zenye kesi nyngi za UVIKO-19 barani Afrika.

[https://media]
 
Sisi Tanzania sijui hata kama tunajua ni maeneo gani hatarishi, tunaishi kwa kudra za Mungu...
 
Back
Top Bottom