Watu zaidi ya 20 wafariki kwenye ajali iliyohusisha magari 10

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Watu zaidi ya 20 wamefariki kwenye ajali iliyohusisha zaidi ya magari 10 kwenye eneo hatari la Sachangwan kwenye barabara kuu ya Nakuru - Eldoret

Taarifa zinaonyesha dereva wa lori lililokuwa linaelekea Nakuru alikuwa akikimbizwa na maafisa wa Mamlaka ya Usalama wa Usafirishaji (NTSA) na dereva huyo kupoteza uelekeo wa lori hilo na kugonga magari manne yaliyokuwa yanakuja upande wake, magari hayo ni basi aina ya Coast, Nissan Matatu nne, lori jingine na magari kadhaa ya binafsi

Hii inakuja masaa kadhaa baada ya watu 13 kufariki kwenye ajali mbaya iliyotokea usiku wa Jumatatu (Disemba 11) kweny daraja la Kamukuywa kwenye barabara kuu ya Webuye-Kitale

Jumamosi iliyopita (Disemba 9) ajali nyingine mbili zilisababusha vifo vya watu
25348819_10156144954734497_9193557907454594563_n.jpg
bus2.jpg
prado_accident.jpg
sachangwan2-768x432.jpg
sachangwanwitnesses.jpg
trucksachangwan.jpg


============================================================


At least twenty people are feared dead following a multiple car crash at the dreaded Sachangwan area on the Nakuru-Eldoret highway.

Reports indicate that a truck driver heading to Nakuru was being chased by National Transport and Safety Authority (NTSA) officials when he lost control of the truck and hit oncoming vehicles; a Modern Coast bus, four Nissan Matatus, a truck and several other private vehicles.

Survivors were rushed to MediHeal and Nakuru Level Five Hospitals in Nakuru town, with rescue teams indicating that the number of causalities is likely to increase.

This comes hours after 13 other people died in a gruesome road accident, which occurred Monday night (December 11) at the Kamukuywa Bridge black spot on the Webuye-Kitale highway.

Last weekend, 28 people died following two separate accidents that occurred on Saturday (December 9). One of the accidents killed 21 people in Baringo after an Administration Police (AP) lorry lost control and veered off the road, while the other, involving a Toyota Probox claimed the lives of seven musicians from the popular Kenene international band, a well known Kalenjin music group

Source: Citizen Tv
 
sasa hao walokuwa wanamkimbiza sijui wanajiskiaje

Pole kwa wafiwa
Kwa nchi za wenzetu, kukimbiza gari kwa kosa lolote wanaangalia usalama wa watumiaji wa barabara na kwa ujumla na hali ya barabara waliyopo. Sisi vichwa ngumu tunafukuza tu.
 
Duh, poleni majirani. Magari yana maliza watu kuzidi magonjwa ukanda huu.
 
Dahhh!! Poleni sana majirani zetu. Kunahaja kubwa sana ya kukagua ubora wa vyombo vya moto tunavyosafiria. Kununua mitumba iliyobadilisha wamiliki mara kumi halafu unaendesha kama limetoka kiwandani jana yake, tutamalizana maisha na viungo vyetu kwakweli.
 
tia ndani maafisa usalama huwenda hata lori lilibeba kichwa cha swala mmoja wameenda kusababisha mauti kwa waru wote hao
 
Back
Top Bottom