Watu wenye pikipiki wamuua kwa risasi Mkuu wa Idara ya Kilimo Ilala

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
UJAMBAZI DAR: Watu wenye silaha wakiwa na pikipiki wamemuua kwa risasi mkuu idara ya kilimo Ilala, F. Luambano na kumpora mkoba Tabata.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 
Aisee kama ni kweli so sad hawa wafanyakazi wa benki nao ni jipu , na inatupasa kuangalia njia zingine za ubebaji wa vitu vya thamani
 
So sad, jamaa kafariki!!!?? jana nilikuwepo eneo hilo tunakula gambe, wakamuwahisha hospital. Kumbe kafariki!!! hawa majambazi walaaniwe.
 
UJAMBAZI DAR: Watu wenye silaha wakiwa na pikipiki wamemuua kwa risasi mkuu idara ya kilimo Ilala, F. Luambano na kumpora mkoba Tabata.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Sasa mimi ninae kuja mara kwa mara Dar na briefcase ya nguo si wataniparamia wakijua nimetoka mererani na tanzanite!! hapa kuna kitu na polisi hawana budi kujipanga upya na kukomesha hii tabia.

Kwa upande mwingine sijui tutafanyaje maana hizo pikipiki ni msaada sana kwa watu wa kipato cha chini na huwezi kumgundua yupi ni mwema na yupi ni mwizi!
Kama ni kweli basi ni so sad.
 
Miaka 20 iliyopita tulitahadharisha athari za kuruhusu biashara ya silaha Tanzania wakati ule hakukuwa na mitandao ya kijamii, kelele zetu tuluzipiga kupitia magazetini, makala zile zilipata upinzani wa kutosha hasa toka jeshi la polisi leo hii madhara yako dhahiri na jeshi liko kimya
 
Halafu hili la ujambazi na uporaji linaonekana sio hoja ya msingi kwa hii serikali ya awamu ya tank maana hakuna anayeongelea kiasi sasa hivi wanakwapua mchana kweupe na kutokomea
 
Wakati wa JK ujambazi ulipungua sana sijui kwa nini sasa umerudi kwa kasi
 
UJAMBAZI DAR: Watu wenye silaha wakiwa na pikipiki wamemuua kwa risasi mkuu idara ya kilimo Ilala, F. Luambano na kumpora mkoba Tabata.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

yesu wangu hizi bunduki wanapata wapi,,,

rip
 
Miaka 20 iliyopita tulitahadharisha athari za kuruhusu biashara ya silaha Tanzania wakati ule hakukuwa na mitandao ya kijamii, kelele zetu tuluzipiga kupitia magazetini, makala zile zilipata upinzani wa kutosha hasa toka jeshi la polisi leo hii madhara yako dhahiri na jeshi liko kimya
Hakika hali ni mbaya
 
na
Hakika hali ni mbaya
pia huuko mipakani kupo loose ma ak 47 yapo kwa majambazi aisee hatari saaana hii nji si salama kabisa kwakweli kwa sasa ukiwa uko maeneo ya bank unajipitia uwe makini unaweza shtuka risasi imekuingia wakati huna hata mia mfukoni
 
tatizo la haya yote ni ukosefu wa Ajira ..

70% ya vijana wanaomaliza mafunzo yao JKT hukosa ajira na kuishia kuranda randa mitaani.

Serikali ijipange upya
 
Back
Top Bottom