Watu wenye iPhone wanafaidi sana

Watu wenye iPhone wanafaidi sana

Job Richard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
3,875
Reaction score
2,201
Baada ya kujichanga kwa muda fulani nikajizolea iPhone 13 Pro Max pale Mlimani city sikutaka zile Kushoto nyingi Mara iphone za Mwenge fake Mara Kariakoo ukinunua ushapigwa tayari

BAADA YA KUJUA SASA
Hakuna iPhone fake labda zile zenye android ni copy kweli kweli ila mpaka upigwe duuuh wewe Hujui simu kwa kweli.

RAHA ZILIZOPO IPHONE
Nimegundua IOS ina sifa nyingi zaidi ya android

Mpaka sasa Ukiwa na iphone unaweza kupromote reels kwenye instagram Wakati hicho kitu android hakipo

Kwenye ufasta hapa iOS Kaua sana ni kuteleza tu kwa chochote utakachofanya iwe online au offline

Picha kali sana hapa mpaka Huyo google pixel akasome anasifiwa tu hana Hizo sifa (japo katika android ni simu kali sana Ila muonekano nao imenyimwaaa kuitoa Zaidi ya million mbili KISA CAMERA TU DUUUH)

Vingine tuongezee
View attachment 2536404
 
Hamna kitu hio simu ni kwajili ya fashion tu... Uhondo wote upo simu za Android tabaka la juu kama Samsung, lg, nokia, sony, Google pixel, xiaomi, n.k. yani hapa iphone anafunikwa, lakini pia kuna simu za android tabaka la kawaida zilizotengenezwa kwa vifaa vya bei rahisi kama vile tecno, infinix na itel hizi huwa zinapitwa kwenye speed na camera sababu ya vifaa vyake lakini vitu vingine iphone bado yupo nyuma.

-Iphone sio simu yenye kamera nzuri kuliko simu zote kama wengi wanavyo danganywa, Kwenye zile simu za android tabaka la juu zipo mashine kama google pixel na xiaomi zinamgaragaza iphone, tatizo la wabongo wanachokosea wanalinganisha camera ya iphone na zile simu za android daraja la kawaida.

-Cable za iphone zinachaji taratibu, zina kasi ndogo ya kuhamisha mafaili na zina ubora mdogo, kampuni ya iphone walishupaza shingo mda mrefu lakini hatimae wamekubali kuanza kutengeneza simu zitazotumia usb cable za android.

-iphone haina tundu la earphones, ni mpaka uwe na earphones za kuchaji zisizo na waya, simu za android unaamua mwenyewe utumie earphones zipi kusikiliza ziwe zenye waya au wireless, unaweza tumia za waya huku unachaji zisizo na waya.

-android kuna apps na games nyingi sana kuliko iphone,

-iphone haiwezi kurekodi simu unazopiga / kupokea

-iphone inatengenezewa vifaa vyake kibao na makampuni ya simu za android.

-iphone haina apps za kutumia internet bure, kwa android kuna apps kama ha tunnel, wire tun, nic vpn na nyingine kibao watu wanazitumia kufaidi internet bure bila kununua vifurushi, kuna kipindi flan hapo mwaka jana watu waliukamua kweli kweli mtandao mwekundu, kushusha gb 20 kwa siku ilikuwa kawaida.

-iphone haina memori kadi, yani simu yako ikiungua au ikifa inaenda na mafaili, android hata simu ikipata hitilafu unabaki na kopi ya mafaili kwenye kadi.

-iphone ni ngumu kuhamisha mafaili kwenda kwa computer, mfano mrahisi simu za android ukitaka kuprint kazi stationery, unachomeka cable, unaifungua simu kwa password, unafungua file la kuprint, yani zoezi la dakika tu, kwa iphone mambo ni mengi inabidi uingize kwanza software kwenye computer ili ufungue mafaili, waweza tumia dakika 10 kumaliza zoezi dogo.

-iphone haina radio, kusikiliza radio ni mpaka uwe na data, ukienda sehemu haikamati internet ama hakuna internet huwezi sikiliza radio.

n.k,,,,

mimi nimeandika kwa uchache tu, kuna pozt ipo humu humu jamiiforums imeelezea mapungufu kibao, kama unataka kuisoma >> minya hapa <<

iphone ni kama vile vimbwa mbwa wadogo kama yule wa wema sepetu wanauzwa milioni 3 ila ni kwajili ya mapambo tu (sijui kama wana kazi nyingine), wale mbwa hata kumtisha paka ni ngumu, ila kuna mbwa waliopitia mafunzo wanauzwa laki 8 wana miili wenye afya, wakibweka hata kama unapita nje mwili unasisimka, wana mbio, hawaumwi magonjwa hovyo hovyo, mwizi akiruka ukuta anashughulikiwa na hata kwenye urafiki ni mbwa anaekuchangamkia.
 
Unajua kwanini Pixel 7 pro anatakiwa alinganishwe na the next iphone series na sio hii 14 pro max!!? Still zote zimetoka mwaka mmoja?

Na kwanini 14 analinganishwa na 6 xl!!? Iphone yupo vizuri ila sio complete kama hivyo unavyomsifia Pixel amewachakaza vibaya sana iOS na androids wenzake
 
Nilitumia iphone 12 pro max kwa mwaka mmoja na nusu nikaona hakuna jipya kwangu nikampasia mwanangu wa kike na kurud kwenye Samsung S10 yangu ya siku zote nadhani ni kutokana na fact ya kuwa mimi si mpenz wa picha(Photogenic) japo siku hizi siwez kutumia simu yoyote ya Android bila kuwa na launcher ya iphone..
 
Nilitumia iphone 12 pro max kwa mwaka mmoja na nusu nikaona hakuna jipya kwangu nikampasia mwanangu wa kike na kurud kwenye Samsung S10 yangu ya siku zote nadhani ni kutokana na fact ya kuwa mimi si mpenz wa picha(Photogenic) japo siku hizi siwez kutumia simu yoyote ya Android bila kuwa na launcher ya iphone..
Ni lazima upate ka uraibu wenyewe wanaita ‘IOS’ effect’😂
 
Vp mkuu.
Nna flash hapa simu yako naweza nkachomeka nkacopy mafaili??
Vp nna video nataka hapa vipo nkipeleka library yule mcheza musics anaweza kukopi akaniwekea kwenye sm ya iphone
Au umenunua kitu kinachokutesa boss
 
Vp mkuu.
Nna flash hapa simu yako naweza nkachomeka nkacopy mafaili??
Vp nna video nataka hapa vipo nkipeleka library yule mcheza musics anaweza kukopi akaniwekea kwenye sm ya iphone
Au umenunua kitu kinachokutesa boss
😅😅 kwanza tu ukiconnect tu Laptop then utafute picha au document flan ni utakesha.

Maana vinakuwaga havina majina

Au mie ndio siwezi?
 
Ni lazima upate ka uraibu wenyewe wanaita ‘IOS’ effect’😂
Aisee kumbe🤣🤣hapa nakuunga mkono mkuu,yaani imefikia kipindi mpk nikiona display ya Android nakasirika eti,hata screenshot za Chart za WhatsApp naenjoy nikitumiwa ambazo ni dark theme au za WhatsApp ya IOS😂😂😂na hata simu yangu kwa ujumla ni lazima iwe na Launcher ya iphone hili kuipa muonekano wa iphone bila hivyo naboreka sana yaani
 
Nilitumia iphone 12 pro max kwa mwaka mmoja na nusu nikaona hakuna jipya kwangu nikampasia mwanangu wa kike na kurud kwenye Samsung S10 yangu ya siku zote nadhani ni kutokana na fact ya kuwa mimi si mpenz wa picha(Photogenic) japo siku hizi siwez kutumia simu yoyote ya Android bila kuwa na launcher ya iphone..
Mwaka mzima na nusu? Ni uliipenda wewe
kitu chenye hakina maajabu uwa hatumalizi nacho miezi mi3.


Unakumbuka ile nilipewa na bro? Lenie haikumaliza masaa matatu mkononi mwangu nikamrudishia
 
Back
Top Bottom