Watu wengi wasio na kazi wanaopitia vipindi vigumu na wana elimu ya juu, huwa wanachanganya shida zao na tabia

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,586
15,369
Tabia ni kama ngozi, haivuliki kirahisi.
Hata mwenye tabia ya wizi, akikaa bila kuiba na akaishiwa kabisa hadi pesa ya kula, atakuwa mpole ila ukimsaidia akichangamka atakuibia tu.

Watu wengi sana leo hawana kazi, wanasema wako tayari kufanya kazi hata mochwari za marehemu wa ajali mbalimbali lakini wanasahau kuwa bado wanatabia za wizi, utapeli, uvivu, majungu, uhuni zimefichwa na ukusefu wao wa mchongo wa ajira.

Kipindi huna kazi ni kipindi pia cha kushughulikia tabia ambazo zitakugharimu hata ukipata hiyo kazi.

Amka mapema

Heshimu watu unaowazidi na wanaokuzidi.

Jijengee uqminifu na kuaminika

Fanya kitu zaidi ya ulivyoelekezwa (jiongeze)

Epuka majungu na masengenyo
 
sahihi,

au watalaumu uchawi, na kuna ule msemo 'wakati wa Mungu haujafika'
Kuna mdau aliikoswa kazi ghafla alikuwa na stress hadi nguvu za kiume zikakata na familia kuparaganyika.
Mola amesikia kilio chake kapata kamchongo, jamaa ndio captain wa majungu, malalamiko mengi kuliko aliowakuta, mchelewaji, mapenzi kazini, hana umakini kila anachokifanya lazima kikaguliwe upya kisirisiri maana anaweza kuwaingiza chaka wenzake.
 
Aisee🤔
 
Tabia ni kama ngozi, haivuliki kirahisi.
Hata mwenye tabia ya wizi, akikaa bila kuiba na akaishiwa kabisa hadi pesa ya kula, atakuwa mpole ila ukimsaidia akichangamka atakuibia tu.

Watu wengi sana leo hawana kazi, wanasema wako tayari kufanya kazi hata mochwari za marehemu wa ajali mbalimbali lakini wanasahau kuwa bado wanatabia za wizi, utapeli, uvivu, majungu, uhuni zimefichwa na ukusefu wao wa mchongo wa ajira.

Kipindi huna kazi ni kipindi pia cha kushughulikia tabia ambazo zitakugharimu hata ukipata hiyo kazi.

Amka mapema

Heshimu watu unaowazidi na wanaokuzidi.

Jijengee uqminifu na kuaminika

Fanya kitu zaidi ya ulivyoelekezwa (jiongeze)

Epuka majungu na masengenyo

Well Said...Ushauri Konki.
 
Mkuu siku zote shida husigina na kukandamiza vijitabia vya kishenzi vya mtu and vice versa is true.
Wasiojua hili, ndio huwa wanalalamika. Nimemsaidia lakini sasa hivi kafanikiwa ananidharau.

Anasahau alimsaidia umasikini wake sio dharau yake.

Ukimpa first aid Koboko akipata nafuu kimbia. Atakuua tu.
 
Tunatakiwa kusaidiana bila kujali ubaya au uzuri wa mtu. Kumtoa mwanadamu mwenzako kwenye hali duni kwendq kwenye hali bora ni sadaka kubwa kwa mwenyezi Mungu.

Ila akibadilika hilo ni jukumu lake sio letu tena.
Nadhani ni muda muafaka sasa, kwa wajasiriamali wetu wale waliofanikiwa, wapewe vipindi katika vyuo vyetu ili waweze kufundisha watu wetu namna ya kujiajiri.
 
Back
Top Bottom