Kwamba dunia ni gereza la Lucifer? Maybe it's true kwa mawazo na analysis zako....kimsingi sina uelewa sana kwa mambo ya dini pia sina uelewa sana wa mambo ya ulimwengu
Nina maswali machache kwako mleta uzi-:
1.Asili ya ulimwengu ni nini?
2.Kama ni nature hiyo nature ilianzaje?
3.Hizo jamii za lucifer na ANU zilitoka wapi?
4.Huyo Mungu wa juu zaidi upi mwanzo na mamlaka yake?
5.Huyo ANU yuko wapi
6.Dunia iko sijui kikazi sijui cha ngapi kuanzia kwa huyu the so called Adam je unaamini story za
a.Gharika ya Nuhu b.Sodoma na ghomora?
7.Kwa mujibu wa maandiko ya imani zilizopo duniani kuna mitume kama Mohamad na Yesu je hawa walikuwepo kweli au fiction?
8.Kama mamlaka hizi za Dunia ni gereza la lucifer,haya maendeleo na vitu vingi vinavyotokea nani huvitengeneza?
9.Mvua,jua hutokea wapi na zipo kwenye mamlaka ya nani?
10.Miujiza inayofanyika duniani iwe ya kichawi au kiimani imekuwa powered na nani?
11.Uhusiano kati ya huyu Mungu wa juu na hawa wanadamu wenye nafsi ukoje na wataweza vipi kurudi huku juu mbinguni ikiwa wanakufa wanarudi mavumbini?
12.Nguvu za mizimu,frimason frimason n.k zinatoka wapi?
Karibu sana kwa mjadala nitajifunza Asante.
Asante mkuu kwanza una maswali ya kufikirisha hadi nimefurahi. Naanza kwa nukuu kutoka kwa mwanasayansi mashururi wa karne ya 21 ndugu stephen Hawkings kitabu chake cha mwisho kinaitwa Brief Answers to Big Qieation anasema
“There's 'No Possibility' of God in Our Universe”
Kiuhalisia hakuna mungu isipokuwa kuna energy au mionzi chanya na hasi ambayo mionzi hiyo hujiunganisha na maisha ya mwanadamu kupitia ubongo wake kwa namna anavyo waza au kufikiri. Mionzi hiyo ndio chanzo cha maisha ya vitu vyote hai na visivyo hai hapa duniani.
Asili ua ulimwengu ulitokea tuu hakuna aliye umba kila kitu kilikuwapo, kipo, na kitaendelea kuwepo. Jamii za lucifer na zingine nilizo taja hapo juu nao wapo katika safari ya kutafuta destiny yao ndio mana hawaamini kama kuna mungu.
Asili ya watu wanachoita mungu mfano wake ni gravitational force. Ni nguvu iliyoshikilia ulimwengu wote. Hii gravitation force inasema every particle attracts every other particle in the universe with a force that is directly proportional to the product of their masses and inversely proportional to the square of the distance between their centers.
Hiyo gravitation force ilikuwepo tuu na wala sio mungu aliumba kwani hakuna sehemu yoyote kwenye vitabu vyenu vya dini inasema mungu aliumba gravitational force.
Hizo jamii za lucifer nimeshajibu kwenye mada. Duniani hapa ni 3rd dimensiom reality viumbe wengine kama lucifer wao wanaishi 4th dimensio. Viumbe watakatifu wenye maarifa wanaishi kuanzia 5th dimension na kuendelea. Dimensions au timelines zipo 9. Kukuthibitishia hili ukiwa hapa duniani kuna kitu kinaitwa De Ja Vu kama hujawahi kukutana nayo huwezi elewa.
Mungu wa juu zaidi ni subconscious yako ambayo inakuunganisha na positive au negative energy kulingana na hisia zako. Like attract like. Analowaza mtu ndio linalo mtokea.
ANU ndio mkuu wa viumbe vya ulimwengo na msimamizi wa aheria za ulimwengu ambazo zipo saba na hizo ni Law of Attraction, law of Polarity, law of Rhythm, laws of Relativity, Cause and Effect, Gender/Gustation and Perpetual Transmutation of Energy. Hizi kuna mtu alishaziongelea hapa Jamii forum. Sheria hizi ndio mungu aliue juu zaidi. Kumbuka Mungu sio mbabu mwenye ndevu anaye ishi mawinguni kama dini yako inavyo kutengenezea picha bali mungu ni kufata sheria hizo zilizopo juu ya kila kitu.
Kuhusu garika ya nuhu unadhani pale mashariki ya kati nuhu alipata wapi tembo na simba na nguruwe na kuwajaza kwenye meli au safina kumbuka kuna aina zaidi ya milioni 8 za wanyama jiulize kuna meli inaweza kubeba wote hao? Hiyo story ya nuhu nilimuadithia mwanangu akacheka
Akasema namdanganya hakuna meli kubwa kama hiyo. Sodoma Na gomora mbona na mambo mengine ya biblia ni ya kutunga kwani katika historia ya watu karne ya 21 ndio sodoma yenyewe lakini mbona hamna moto?
Hao mitume unauhakika gani sio watumishi wa lucifer? Kumbuka muhamed wakati anapokea wahai alikiwa hajitambui na yesu ni mungu jua mkuu jina lingine la yesu ni Tammuz. Kwani Tammuz naye alizaliwa na mwanamke bikra kama yesu alivyo zaliwa na mwanamke bikra.