Watu wengi wanakula ila hawalimi.

Mwenyewe nataka mwakani niingie kwenye kilimo Cha mbogamboga sijui ndo kizungu mnaita hotculture. Soko nimeona lipo nje nje msimu wa kiangazi
Safi sana mkuu.

Utapiga pesa sana kwasababu mbogamboga siku zinavyo zidi kwende zinazidi kuwa hadimu sio kiangazi tu. So idea yako ni nzuri sana usipuuzie.
 
kilimo kina gharama sana mkuu yaani utafte mashamba,wafanyakazi,mbegu,mbolea na mwisho wa siku kuna suala la ushuru si unaweza kufa na madeni
Ni kweli mkuu kilimo kina gharama.

Lakini inategemea unataka kulima nini mfano mtu akitaka kulima viazi, maharage, njegere, mahindi, njugu au karoti hayo mazao hapo juu hayahitaji pesa nyingi ili wewe uweze kulima.

Muhimu ni kuwa na Nia plus information sahihi kuhusu mazao unayotaka kuyalima then kila kitu kitawezekana tu.
 
Ogopa sana mtu anae ona, watu nyuma ya Sreen ya laptop wanacheza/Chezea ila yeye na jembe lake ndo anafanya kazi.

Kilimo chenyewe kila siku wana lialia, mara Mvua, mara mbegu, mara bei ya soko, mara wadudu.

Nway, nyie limeni sisi tutakuja kununua, na muache kuwasema sema wateja wenu.
 
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
 
Unfortunately hilo haliwezi kutokea mkuu .

Kila mmoja inatakiwa apambane kwa njia anazo ziweza yeye pamoja na familia yake.
Ndo maana nikisikia kiongozi anataka kupunguza umaskini huwa najiuliza anamlenga nani, amejipangaje mwisho wa siku wanatoa hela vijana wakauze mitumba na sendo za kina dada kariakoo
 
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
Hoja ya jamaa ni kwamba ratio ya ofisini vs shambani haiko sawa maana vijana wengi wanakimbilia maofisini sasa mtakuwa wote ma afsa kilimo.?
 
😀 hakuna alipo semwa mtu mkuu ni mtazamo wako tu.

Unaweza ukalima huku ukichezea laptop yako ofisini naona kama haujaelewa mada.
 
Ni mgawanyiko wa kazi, kuna kukaa ofisini na kulima shambani. Huko ofisini unamsaidia mkulima kuhusu kilimo bora, na udongo unaofaa kisayansi. Mkulima nae anakupa chakula ili uendelee kufanya utafiti.
Of course mkuu mada haijasema watu waache kazi zao nyingine ili wakafanye kilimo.

Unaweza kuwa Doctor lakini pia mkulima, unaweza kuwa askari magereza lakini pia ukafanya kilimo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…