Watu wengi waliopo kwenye ndoa hawana furaha!

Huu uzi umetawaliwa na upweke wa kimaandishi.

Ukisoma tu comments za wachangiaji.....unaweza pata picha halisi, juu ya nini kiendeleacho kwenye ndoa nyingi.

Bila shaka Demiss umepata majibu yako...
 
Tupeni mrejesho kama mna furaha kweli!

Leo ukiangalia ndoa nyingi zimepooza na kufunikwa na wingu zito la mizozo kila kukicha

Ukiwauliza wanandoa wengi husema Mwanzoni mwa ndoa yetu tulipendana kwa dhati,lakini shauku na penzi letu siku hizi imepotea.

Hakuna urafiki mzuri kati yetu kama hapo awali wala hatufurahii kuwa pamoja,hata kucheka inakuwa tatizo pamoja na kulala kitanda kimoja na ushirika wao katika mambo mengi.

Ndoa zingine wana ndoa hawawezi hata kujadili matatizo yao kwa pamoja, mbaya zaidi kufanya mapenzi kwao imekuwa kama wajibu badala ya starehe.

Hii ni hatari maana hakuna mtu kati yao anayejisikia shauku ya mapenzi kwa mwenzi wake.

Ukichunguza sio kwamba kuna mtu anatoka nje ya ndoa hapana utawasikia wanasema ndoa yetu haina upendo.

Matatizo ya ndoa yapo mengi na yanatofautiana ndoa na ndoa,lakini vilio vingi vya ndoa vinafanana.

Nyongeza : Ambao hatujaolewa tunatamani kweli Kuingia kwenye ndoa .


Location: Napita kwa huzuni.


Kumbe hujaolewa bado, ila hongera maana hujasema umefanya utafiti wako namna gani lakini inaonesha unayajua yaliyopo kwenye ndoa, eti. Kwa mtazamo wako inaonesha hakuna furaha kwenye ndoa lakini eti bado unatamani sana kuingia humo hivyo hivyo, hongera pia kwa ujasiri huo mpana.

Umesema pia eti hakuna anayejisikia shauku ya mapenzi kwa mwenzake, japo pia umekiri wanafanya mapenzi kama wajibu na siyo starehe, sijui wewe unapenda nini zaidi kati ya mapenzi yafanyikayo ili kukamilishana na hayo unayoyaita ya starehe kwenye ndoa.

Natamani ungepata wa kukuoa soon ili tupate mrejesho toka kwa mwenyewe, maana ungekuja na pande zote mbili, mapenzi ambayo unafanya sasa kabla ya kuolewa ambako nahisi unastarehe zaidi na mapenzi baada ya kuwa umeolewa.
 
Daaah. Sakayo ningejua pa kukupata kila siku ningekupata, ila kama najua sijui, embu nidokeze basi niwe nakuzooom na mimi,
NB: PM hata sifungagi, si unajua joto mjini inatulazimu tulale mlango wazi, wewe je?
Mhenga wangu mimi, mbona mie huwa nakuzoom nakupata eti...

N.B: pm nimefunga, si unajua mjini wajanja wengi watanidukuaa?!
 
Mhenga wangu mimi, mbona mie huwa nakuzoom nakupata eti...

N.B: pm nimefunga, si unajua mjini wajanja wengi watanidukuaa?!
Najitaidi nikuelewe lakini...something missing, is like code uncoded, give me a root to follow. Nawasiwasi umenidukua wewe😂😂😂 .
 
Matatizo ya ndoa yapo mengi na yanatofautiana ndoa na ndoa,lakini vilio vingi vya ndoa vinafanana.
Wanaolalamika na kusema ndoa ni tatizo hawajitambui. Kwani
1. Walipata vyeti pengine hata hawajawahi kulala chumba, kitanda na shuka moja.
2. Cheti walipata kabla ya mitihani kuifaulu. Changamoto au vitimbi kwenye ndoa ndo mitihani yenyewe hiyo. Wasiolitambua hili ndo hulalamika na kuwatishe wengine ambao hawajaingia kwenye taasisi hii njema na furaha kuu!
3. Wengine waliingia bila malengo mahususi. Waliingia tu pasipo kujua wanakwenda kufanya nini na wataongeza nini kwenye kasha tupu la ndoa.

USIOGOPE. KARIBU. HUTAJUTA.
 
TAFITI UMEFANYA LINI MKUU UKAGUNDUA HIVYO
Ilo lipo wazi linajulikana wengi wako ndoani basi tuu kwa sababu wanahofia mengi wakitaka kutoka..aidha watoto..watu watasemaje..ntakaa wapi..nk..ila wengi ni mateso tuu..poleni ila mm binafsi Sintavumilia hata kidogo mambo ambayo yanarekebishika.
 
Najitaidi nikuelewe lakini...something missing, is like code uncoded, give me a root to follow. Nawasiwasi umenidukua wewe .
Mejikuta nacheka kwa sauti mimi jamani...

Sijakudukua bana mhenga, huwa nakuzoom tuu akii...

Nothing's missing, there's no code, everything is open, just zoooommm
 
Ilo lipo wazi linajulikana wengi wako ndoani basi tuu kwa sababu wanahofia mengi wakitaka kutoka..aidha watoto..watu watasemaje..ntakaa wapi..nk..ila wengi ni mateso tuu..poleni ila mm binafsi Sintavumilia hata kidogo mambo ambayo yanarekebishika.
Mfano unakuta mzazi mwenzio ni mkorofi vibaya yani akilianzisha ni atari huwa hajali. Na tayari mmezaa muna watoto wengine wadogo, wengine wapo skuli. Sasa hapo unafikiri hutavumilia kweli? Basi huna huruma na wanao.
 
If it's that way then it's not right , you deserve some loving, some romance, some romantic gateouts hata kama ni kwenye ka restaurant, you deserve some moment of two Alone,
Ni majukumu zaidi than romance
 
Back
Top Bottom